Mwanamke anaweza kufanya uamuzi wa njia ya kujifungua ambayo angependa kupitia. Kujifungua kupitia kwa uke ama kwa upasuaji haikufanyi kuwa mama bora ama mdogo kuliko mwingine. Kilicho muhimu ni kuwa ulijifungua mtoto salama na mwenye afya. Hata hivyo, kuna baadhi ya wakati ambapo mama huenda akajipata akijifungua kupitia kwa upasuaji ili kunusuru maisha yake na ya mtoto. Tazama baadhi ya utunzaji baada ya c-section.
Mambo ya kutofanya baada ya kufanyiwa upasuaji wa C-section

- Usijilaumu ama kuhisi vibaya kwa sababu umejifungua kupitia upasuaji. Kilicho cha muhimu ni kuwa maisha yako na ya mwanao yako salama
- Safari ya kwanza kuelekea nyumbani baada ya upasuaji haitakuwa yenye raha. Hasa ikiwa mnapitia mahali pasipo nyooka, utahisi uchungu. Ni vyema kumwuliza mliye naye atumie mwendo wa chini na kuilinda tumbo yako kwa mto
- Kumbuka wakati wote kuwa na mto mkononi mwako
- Jaribu kadri uwezavyo usicheke ama kuchemua. Kwani, kila mara unapofanya hivyo, kidonda kile cha upasuaji kitauma sana
- Epuka kula vyakula ambavyo hukupa gesi, kwa mfano, baadhi ya watu hupata gesi baada ya kula maharagwe. Epuka chakula hiki na vingine vinavyo kupa gesi
- Usile vyakula vyovyote vinavyo kufanya uvimbiwe
- Mama huwa na mawazo mengi anapopata mtoto wake. Huenda baadhi ya wakati akazidiwa na mawazo na kujipata akilia kila mara. Hata ingawa ni sawa kulia mara kwa mara, kumbuka kuwa, kulia kwa nguvu kutakufanya uhisi uchungu kwenye kidonda chako cha upasuaji wa C-section
- Upe mwili wako muda wa kupona. Baadhi ya wakati, huenda mama akawa na shaka nyingi kwa nini tumbo yake haijarudi kama ilivyokuwa hapo awali punde tu baada ya kufanyiwa upasuaji. Itachukua muda kwa tumbo lako kurejelea shepu yake ya hapo awali, ila, usiwe na shaka kwani baada ya muda litazidi kupungua

- Ikiwa una muuguzi anaye kuchunga, mwache akiangalie kidonda chako. La sivyo, mpe bwanako jukumu la kukiangalia kidonda chako. Pumzika.
- Kwa wanawake walokuwa wakifanya mazoezi kila siku, huenda wakahisi kana kwamba kidonda wanapaswa kurejelea mazoezi baada ya muda mfupi. La hasha, kufanya hivi kutakifanya kidonda kiume sana. Ni vyema kwa mama kungoja hadi anapopatiwa ruhusa ya kurejelea mazoezi na daktari wake
- Kwa mama anayeishi kwa nyumba yenye ngazi nyingi, tafuta chumba chini ambapo hauhitajiki kupanda ngazi nyingi
- Usifanye kazi za nyumba, hasa zinazo kuhitaji kuinama sana. Kuinama kutakifanya kidonda chako kipasuke na kusababisha maumivu mengi
Hongera mama kwa kupata mtoto wako mwenye afya na kwa njia salama. Kamwe usiwahi hisi kana kwamba wewe sio mama kwani ulimpata mtoto wako kupitia kwa upasuaji. Wewe ni mama, kama wengine, na mtoto wako ni sawa na watoto wengine. Hakikisha kuwa unaangazia afya ya mwanao na yako kwa makini. Kisha, hakikisha kuwa unaenda hospitalini unapopaswa kukiangalia kidonda chako.
Kila la heri katika safari yako mpya ya kuwa mama! Kumbuka kuangazia vidokezo hivi vya utunzaji baada ya c-section.
Soma Pia: Jinsi Kunyonyesha Kunavyo Athiri Tendo La Ndoa Baada Ya Kujifungua