Yote Unayo Hitajika Kujua Kuhusu Utunzaji Baada Ya Kujifungua

Yote Unayo Hitajika Kujua Kuhusu Utunzaji Baada Ya Kujifungua

Utunzaji baada ya kujifungua ni muhimu katika maisha ya mama na mtoto na kuhakikisha kuwa afya yao iko salama.

Utafiti uliofanyika mwaka wa 2012 na Shirika la Afya Duniani kuhusu utunzaji baada ya kujifungua, ulidhihirisha kuwa kulikuwa na visa milioni 2.9  vya watoto walio fariki baada ya kuzaliwa. Nusu ya vifo hivi vilifanyika katika watoto ambao wange faidika kutokana na mpango mzuri wa baada ya kujifungua. Nambari hizi za juu zina onyesha kuwa utunzaji tosha ni muhimu kwa maisha ya mama na mtoto kwa wiki zinazo fuata baada ya kujifungua.

Utunzaji kabla ya kujifungua

utunzaji baada ya kujifungua

Utunzaji wa mimba unahusisha utunzaji kabla na baada ya kujifungua. Utunzaji kabla ya kujifungua ni utunzaji wa afya unao wakinga wanawake katika safari ya mimba na kuongeza nafasi zao za kujifungua salama. Katika safari yao ya mimba, kumtembelea daktari mara kwa mara kutamsaidia daktari ama mkunga kufuata mimba ili kuepuka ama kugundua matatizo na kuweka hatua za kusaidia kutatua tatizo hilo.

Utunzaji kabla ya kujifungua unatengeneza tofauti kati ya kubaki hai ama kukata kamba baada ya kujifungua, hasa katika nchi zilizo na nambari za juu za vifo vya wamama baada ya kujifungua. Kulingana na Healthline.com, wanawake wasio pata utunzaji kabla ya kujifungua wako katika hatari ya kujifungua watoto walio na uzito mdogo wa mwili. Na watoto hawa wana nafasi za juu za kukata kamba ikilinganishwa na watoto wanao zaliwa na uzito wa kawaida.

Utunzaji wa mimba una husisha:

 • Vipimo vilivyo ratibishwa vya damu kuangalia shinikizo la juu la damu, kukosa damu tosha mwilini na ukimwi
 • Kuangalia ukuaji wa mtoto
 • Kutengeneza mpango wa kujifungua
 • Kuepusha na kudhibiti matatizo ya ujauzito kwa mama na mtoto
 • Kuangalia na kudhibiti nafasi ya mtoto unapo tayarisha kujifungua
 • Na darasa spesheli kukutayarisha kwa maisha baada ya kujifungua

Utunzaji baada ya kujifungua

Utunzaji baada ya kujifungua ni maendelezo ya utunzaji kabla ya kujifungua. Una husisha afya ya mama na mtoto wake katika wiki za kwanza chache baada ya kujifungua. Katika utunzaji baada ya kujifungua, lengo ni kutengeneza mazingira salama na yanayo egemeza afya njema ya mtoto na mama. Na ili kufanikiwa katika lengo hili, timu ya matibabu na familia yote.

Katika wakati huu, mwanamke anapaswa kushauriwa na kufunzwa jinsi ya kujitunza pamoja na mtoto wake. Pia, kufanya hivi kutawasaidia watu kuingilia kati matatizo ya kiafya yanapo ibuka.

Utunzaji baada ya kujifungua una husisha nini?

Wiki za kwanza 6-8 baada ya kujifungua ni muhimu sana. Kwa hivyo, madaktari wengi wata ratibisha utunzaji wa mama baada ya kujifungua kando na vipimo vya mtoto wiki 6-8. Daktari atauliza maswali na kufanya vipimo ili kujua:

 • Afya ya kiakili ya mtoto ili kudhibitisha ikiwa kuna hatari ya kukwazwa kimawazo baada ya kujifungua
 • Shinikizo la damu kuona kama kuna mabadiliko makubwa
 • Utaulizwa kuhusu kuvunja damu baada ya kujifungua na uchafu wa uke
 • Ikiwa ulifanyiwa upasuaji wa C-Section, daktari ata angalia ulivyo shonwa kuhakikisha unapona inavyofaa
 • Wamama walio na uzito mwingi wa mwili watapata ushauri wa lishe na mazoezi ili wawe na BMI ya kawaida

Unacho hitajika kufanya katika kipindi baada ya kujifungua

utunzaji baada ya kujifungua

 1. Pumzika

Mapumziko ni muhimu kwa wamama wote walio jifungua. Unahitaji kutafuta wakati wa kupumzika, mara nyingi mtoto anapo lala. Familia na marafiki wanaweza mlisha mtoto kutumia chupa unapo lala.

2. Tunza uke wako

Ikiwa ulijifungua kwa njia ya kawaida, utunzaji wa uke ni muhimu sana. Hii ni kwa sababu ya kuraruka kunako fanyika. Ili kuhakikisha kuwa uke wako uko kwa umbo linalo faa baada ya kujifungua, unapaswa kumtembelea daktari wako wiki sita baada ya kujifungua. Pia, kujitenga na ngono ni muhimu ili kuupa uke wako wakati tosha wa kupona.

Ripoti visa hivi kwa daktari wako:

 • Kuumwa, hasa kama uliraruka ukijifungua
 • Kuhisi uchungu baada ya kujifungua
 • Uchafu wa uke usio wa kawaida, ambao huenda ukawa na damu
 • Kukojoa bila fahamu yako
 • Kujichafua na kinyesi

3. Kula unavyo paswa

Huenda ukahitajika kula lishe bora na kuishi mtindo bora wa maisha ukiwa na mimba, na ikiwa hiyo ndiyo kesi, unahitajika kuendelea kula chakula chenye afya.

Ili kuhakikisha kuwa haukuli chakula kingi wakati wa kiamsha kinywa, unapaswa kula unapo hisi njaa peke yake. Lishe yako inapaswa kuwa na matunda na mboga, wanga yenye afya, ufuta wenye afya, protini, na vinywaji vingi. Kula vyema kutakusaidia kupunguza uzito wa ujauzito.

Utunzaji baada ya kujifungua ni muhimu sana kwa wamama wote baada ya kujifungua. Na kumwegemeza mama aliye jifungua ili kuishi maisha yake mapya.

Chanzo: World Health Organisation

Soma Pia:Vitu Muhimu Vya Kununua Kabla Ya Kujifungua

Written by

Risper Nyakio