Katika miezi ya kwanza miwili ya mimba, mwili wa mwanamke hupitia mabadiliko mengi. Kwani mimba inakua kwa kasi, hata kama huenda akakosa kung'amua mabadiliko yanayofanyika kwenye uterasi yake. Hata hivyo, kufuatia mabadiliko ya homoni mwilini, mwanamke anaweza anza kuhisi kichefu chefu ama ugonjwa wa asubuhi. Ni muhimu kwa mwanamke kuendeleza mtindo wenye afya wa maisha. Kuna baadhi ya vitu ambavyo anaweza fanya kuhakikisha kuwa anazidi kuwa na afya katika mimba. Tazama utunzaji katika mimba kwa mama.
Utunzaji Katika Mimba: Jinsi Ya Kujitunza Unapokuwa Na Mimba
- Zingatia lishe yenye afya

Lishe ni muhimu katika ujauzito. Chakula ambacho mwanamke anakula kina nawisha afya yake pamoja na ya mwanawe. Kwa sababu hii, ni muhimu kuhakikisha kuwa anakula chakula chenye manufaa kiafya. Baadhi ya vyakula muhimu kwake ni kama vile:
Matunda na mboga. Kikundi hiki kina wingi wa vitamini zilizo muhimu mwilini. Matunda kama machungwa, tufaha na parachichi, mboga kama kabichi, mchicha na sukuma wiki. Kulinda dhidi ya magonjwa.
Protini. Vyakula vyenye protini ni kama mayai, nyama, maharagwe, samaki na maziwa. Muhimu katika ukuaji wa mtoto. Hata hivyo, ulaji wa mayai mbichi na samaki ambaye hajapikika kuna athari hasi kwa afya ya mama.
Nafaka nzima. Nafaka nzima ni kama vile mchele wa hudhurungi, mkate wa hudhurungi na oatmeal.
Ufuta wenye afya unaotokana na vyakula kama njugu, parachichi na mafuta ya olive ni muhimu.

Sukari ya kuongeza inahusishwa na magonjwa mengi kama vile kisukari. Ni vyema kwa mama mwenye mimba kupunguza ulaji wa sukari, badala yake anaweza kutumia asali.

Kufanya mazoezi katika mimba kunasaidia na afya ya mama na kusawasisha uzito wake katika kipindi hiki. Pia yanasaidia kumwepusha mama na maumivu ya miguu na mgongo kufuatia uzito zaidi wa mimba.
Kunywa maji angalau glasi nane kwa siku, kisha upunguze unywaji wa soda na kafeini.
Kabla ya kuchukua dawa zozote katika ujauzito, mama anastahili kuwasiliana na daktari wake. Kuna baadhi ya dawa ambazo huenda zikawa na athari hasi kwa afya yake na ya mtoto.
Mama mwenye mimba anastahili kuhakikisha kuwa anaongeza uzito ipasavyo, usiwe chini ama juu kupindukia. Kuongeza uzito wa chini huenda kukamfanya ajifungue mtoto mwenye uzito wa chini. Kuongeza uzito mwingi huenda kukamfanya mtoto kuwa na uzito mwingi na kuifanya iwe vigumu kujifungua kwa njia ya kawaida. Njia ya kipekee ya kupata mtoto aliye na uzito mwingi ni kupitia upasuaji.
Mbali na mambo haya, ni muhimu kwa mama kufanyiwa kipimo cha kubaini iwapo mtoto aliye tumboni ana changamoto za kuzaliwa. Kipimo hiki hufanyika baada ya wiki ya kumi ya ujauzito. Baada ya hapo, mwanamke anastahili kuzingatia ushauri kutoka kwa daktari wake na kuenda kliniki anavyohitajika.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Vidokezo Muhimu Vya Kufanya Mazoezi Kwa Wanawake Wajawazito