Kidonda cha c-section kinapaswa kutunzwa vizuri. Kutokuwa makini huenda kukamfanya mama kuugua maradhi na kukaa muda mrefu kabla ya kidonda chake kupona. Tuna angazia utunzaji wa kidonda cha c-section ili kuboresha uponaji na kupunguza uchungu kwa mama.
Ishara za maambukizi kwenye kidonda cha upasuaji wa c-section

- Kuvimba kwenye sehemu karibu na kidonda
- Sehemu hiyo kubadilika kuwa nyekundu
- Kuwa na homa kali
- Maumivu makali chini ya tumbo
- Nyuzi za kidonda kuanza kutokana
- Kuvuja damu kutoka kwenye kidonda
- Kidonda kuanza kutoa uvundo
- Usaha kutoka kwenye kidonda
- Kuvimba miguu
- Kuhisi uchungu mwingi unapokojoa
Vyanzo vya maumivu kwenye kidonda cha upasuaji
Kuna mambo mengi yanayomfanya mama kupata matatizo kwenye kidonda cha upasuaji wa c-section. Kama vile:
- Kuongeza uzani mwingi kwa kasi
- Kukosa kumwona daktari ifaavyo
- Kujifungua zaidi ya mara moja kupitia upasuaji
- Kutochukua dawa kama inavyo shauriwa
- Kuvuja damu sana baada ya upasuaji
- Ugonjwa wa kisukari
- Operesheni ya upasuaji iliyochukua muda mrefu
Jinsi ya kuzuia maambukizi kwenye kidonda

- Kutumia dawa hasa ulizoshauriwa kununua
- Kuchukua dawa kama ilivyoshauriwa na daktari wako hadi utakapo zimaliza
- Kisafishe kidonda mara mbili kwa siku kwa kutumia kijitambaa kisafi. Kisha kukikausha vyema
- Epuka kuvalia mavazi yanayo kubana mwili na kushinikiza kidonda
- Mtembelee daktari wako baada ya muda aliokushauri
Maambukizi kwenye sehemu ya kidonda hicho yanaweza kutatuliwa kwa kutumia antibiotiki. Bakteria kwenye kidonda hiki zinaweza kusababisha matatizo kama vile kidonda kutoa usaha ama kukifanya kidonda kutopona.
Maisha baada ya kufanyiwa upasuaji wa c-section yatakuwa na panda shuka zake. Mama anaweza kupunguza kuhisi uchungu sana na kufurahia wakati wake na mtoto mchanga kwa kufanya haya.
Kula chakula bora. Kula lishe bora kunamsaidia kujitenga na kuongeza uzito wa mwili kwa kasi. Uzito uliopitiliza utafanya kidonda kisipone kwa kasi. Ni vyema pia kula viwango tosha vya chakula, sio chakula kingi sana.
Kufanya mazoezi mepesi. Mama anaweza kufanya mazoezi mepesi kama vile kutembea mara kwa mara. Kuboresha kuwa na afya bora na utendaji wa kazi mwilini.
Kutofanya kazi ngumu. Mama aliyejifungua anashauriwa kuwa na watu wa kumsaidia kufanya kazi za kinyumbani. Hasa kazi zinazohusisha kuinama. Kuinama kunashinikiza kidonda na kufanya iwe vigumu kupona. Utunzaji wa kidonda cha c-section ni muhimu kwa mama, na walio karibu naye wanaweza kumsaidia.
Chanzo: healthline
Soma Pia:Usifanye Vitu Hivi Baada Ya Kufanyiwa Upasuaji Wa C-section!