Jinsi Ya Kumtunza Mtoto Mchanga Baada Ya Kuzaliwa

Jinsi Ya Kumtunza Mtoto Mchanga Baada Ya Kuzaliwa

Utunzaji wa mtoto baada ya kuzaliwa huanza hospitalini na kuendelea nyumbani, na kuangaliwa na mama. Haya ndiyo unayo paswa kujua baada ya kujifungua.

Punde tu mtoto anapo zaliwa, anakoma kumtegemea mamake na mabadiliko ya kifizikia huanza kutendeka, hata mwendo wa hewa, mzunguko wa damu na lishe. Utengano kutoka kwa mfumo wa mama una hitaji kuwa laini ili mtoto aishi. Utunzaji wa mtoto baada ya kuzaliwa huanza hospitalini na kuendelea nyumbani, ukiangaliwa na mama.

Utunzaji wa mtoto wako baada ya kuzaliwa

Madaktari hufanya hivi punde tu mtoto wako anapo zaliwa:

 • Kumsaidia mtoto wako kupumua

Jinsi Ya Kumtunza Mtoto Mchanga Baada Ya KuzaliwaDaktari hutoa kamasi kutoka kwa mapua ya mtoto wako na mdomo wake na kumsaidia kupumua mara ya kwanza. Kisha anasugua mgongo wake ili apumue kwa nguvu. Usiwe na shaka mtoto wako anapolia kwa sababu kunasaidia kutoa maji yoyote yaliyo baki kwenye mafua, mapua na mdomo wake. Walakini, baadhi ya watoto hupumua bila kulia, na hilo ni sawa pia. Kisha kwa watoto walio zaliwa kabla ya wakati kufika ama kupitia upasuaji wa C-section, kupumua huenda kukawa na ugumu mwanzoni, kwa hivyo wata hitaji msaada zaidi kutoka kwa daktari.

 • Kushika na kukata kitovu

Mtoto amekuwa akiishi tumboni mwako na msaada wa kitovu, kikiwa sehemu iliyo kuwa inapitisha hewa na chakula. Walakini, anapofika duniani, anakoma kuhitaji kitovu ili kuishi. Daktari wako atakishika na kisha kukikata. Huenda akakubalisha sekunde 30 hadi 60 ili kukubalisha damu kutoka kwa placenta yako kuingia kwenye mtoto wako kabla ya kukata kitovu.

 • Kuweka mtoto na joto

Mtoto wako hufika akiwa amelowa na amniotic fluid, ambayo huenda ikamfanya kuhisi baridi, kwa hivyo daktari atamkausha mtoto wako. Pia, mtoto wakati mwingine huja amefunikwa na vernix, kitu cha rangi nyeupe kisicho kubalisha maji kupita ambacho kimekuwa kikilinda ngozi ya mtoto akiwa tumboni. Vernix inakubalika kubaki kwa sababu inamlinda mtoto kutokana na baridi na vitu vingine kama vile jaundice na kupoteza uzito wa mwili. Hii ndiyo sababu kwa nini mtoto wako huenda akakosa kuoshwa hadi baada ya masaa machache.

 • Kupima Apgar score ya mtoto wako

Hiki ni kipimo ambacho daktari huchukua kuona jinsi mtoto wako anavyo endeleza maisha nje ya tumbo la mamake. Kila herufi katika Apgar husimamia kitu ambacho daktari anapaswa kuangalia, na kufanyika dakika moja na dakika tano baada ya kuzaliwa. Daktari huweka grade 0,1 ama 2 kisha kuongeza kwenye matokeo ya mwisho. Watoto wanao kuwa na matokeo ya chini kwenye Apgar watahitaji kuangaliwa kwa makini kwenye sehemu ya utunzi wa dharura hospitalini.

Nini mtoto anaweza fanya katika hatua hii?

utunzaji wa mtoto baada ya kuzaliwa

Baadaye, daktari anapo kuwa na uhakika kuwa mtoto ako sawa, wanampatia mamake. Kwa sasa mama atamshika mtoto ngozi kwa ngozi kwa njia inayo fahamika kama utunzi wa kangaroo. Kwa njia hii wanakuwa na utangamano na mtoto na kumtayarisha kunyonya, na jambo hili lina himizwa katika saa moja baada ya kuzaliwa. Walakini, baadhi ya watoto huenda wakatumia wakati kwenye incubator, kwa hivyo mama hawezi mshika hadi atolewe. Kwa wanawake walio kuwa wame amka wakati wa upasuaji wa C-section, wanaweza washika watoto wao ikiwa mtoto hana matatizo yoyote. Na wanawake wanao jifungua kwa njia asili, watafunikwa na blanketi huku wakishika watoto wao ngozi kwa ngozi.

Huku waki kumbatiana, daktari bado ana haya ya kufanya:

 • Kupima uzito wa mtoto, urefu na saizi ya kichwa ili kuwa na uhakika ana afya sawa ya umri wake
 • Kumpa mtoto sindano ya Vitamini K kwa sababu chache zifuatazo mtoto hataweza kutoa Vitamini K yake
 • Dawa ya macho kulinda mtoto kutokana na maambukizi ya macho ambayo yana wezekana wakati wa kuzaliwa kupitia kwa uke

Utunzaji wa mtoto baada ya kuzaliwa na kutoka hospitali

taking care of the baby at home

Baada ya daktari kumpa mama ruhusa ya kuenda nyumbani, utunzaji wa kimsingi ni msingi wako kama mamake. Vidokezo hivi vita kuongoza:

 • Kumsafisha

Mtoto wako huwa na vernix baada ya kuzaliwa, ambayo huisha peke yake baada ya siku chache, kwa hivyo hauhitaji kumwosha mtoto mara kwa mara. Pia, kuosha mtoto wakati mdogo baada ya kuzaliwa kumweka katika hatari ya kupata baridi. Wakati wa pekee ambao huenda likafanya ni pale ambapo kinyesi cha mtoto kina chafua ama kina uchafu wa mama. Usimwoshe mtoto aliye na matatizo ya kiafya baada ya kujifungua.

Walakini, ikiwa lazima mtoto aoshwe, anapaswa kuoshwa baada ya masaa machache. Tumia sabuni nyepesi na uhakikishe maji yana joto.

 • Kinyesi cha mtoto

Baada ya kujifungua, kwa siku za kwanza chache, mtoto mchanga atapitisha meconium, ambacho ni kinyesi cha rangi ya kijani. Chenye harufu isiyo kali, na rangi huenda ikibadili rangi. Mtoto wako huenda akakosa kutoa kinyesi kwa siku za kwanza chache na huenda aka kunya kila mara unapo mlisha. Mara unazo mnyonyesha hazijalishi hapa, bora kinyesi kisiwe kigumu.

 • Nepi

Nepi sita zinapaswa kutosha kwa siku ya kawaida kwa mtoto wako. Ikiwa anatumia chini ya nepi sita kwa siku, angalia unywaji wake wa maziwa iwapo anakunywa maziwa tosha.

 • Utunzi wa kitovu

Kusafisha kitovu kwa kutumia bidhaa zinazo faa kunapaswa kuwa kwa ratiba yako. Weka bidhaa za kusafisha kwenye kila sehemu iliyo jikunja ya kitovu. Hapa ni pahali ambapo viini vinaweza kua kwa urahisi, kwa hivyo chukua muda wako kusafisha kwa umakini. Safisha kitovu baada ya kila masaa matatu ukigundua kuwa kuna harufu ama bado iko laini baada ya masaa 24. Kitovu kitaanguka baada ya wiki moja ama mbili baada ya kujifungua. Ni vyema kukumbuka kuwa haupaswi kufunika sehemu hii kwa kutumia kitu chochote.

Mtoto mdogo anapaswa kupokea chanjo za B.C.G na Polio siku tano baada ya kuzaliwa. Tazama ratiba hii ya chanjo ya Kenya. Kwa nchi zingine, tafadhali ongea na daktari wako kuhusu ratiba ya chanjo.

 

Soma pia: Ni Kipi Kinacho Tendeka Mtoto Anapokosa Mojawapo Ya Chanjo Zake?

Vyanzo: March Of Dimes, Better Care

Written by

Risper Nyakio