Unapokuwa na uvimbe wa Bartholin Cyst
Ilianza na sehemu ndogo sana karibu na uke wangu ukihisi kama sehemu ngumu. Ilikuwa chungu sana na sikuitilia maanani; ila kwa siku ya tatu, ilianza kuuma na pia ilikuwa imeongezeka kwa saizi.
Nilidhania ni uvimbe tu ulio ibuka kufuatia sababu yoyote, hatakama ilikaa jambo lisilo la kawaida kwani hii ingekuwa mara yangu ya kwanza ningekuwa na uvimbe katika sehemu kama hiyo. Siku shughulika kuona daktari na niliamua kungoja hadi uvimbe huu utoboke.
Ilikuwa na uchungu mwingi sana. Kukaa na kutembea kulikuwa kwa uchungu sana na iwapo ningetaka kutumia choo, lazima ningejitayarisha kiakili, baada ya siku tano, nilihisi kitu cha maji na kutosheka- uvimbe ulikuwa umetoboka!
Yote yalikuwa sawa hadi mwisho wa mwaka uliopita, nilipohisi kitu kikiwa kigumu kwenye sehemu ndogo, na kufanya hali iwe mbaya zaidi, nilikuwa na mimba! Arrgh… Wakati huu, niliambia mtaalum wangu wa afya ya uke, (ila baada ya kutoboka) na hapo ndipo niliposikia jina hilo kwa mara yangu ya kwanza- kilicho kuwa kikinisumbua ni uvimbe wa Bartholin Cyst ambao ulikuwa na maambukizi. Aliniambia kuwa iwapo ingetokea tena, nimjulishe. Alinielezea kuwa kulikuwa na utaratibu unaojulikana kama Marsupialization ambao ungefanywa ili cyst hiyo isitokee tena.
Bila hata kusema, cyst hiyo ilitokea tena kabla ya mwaka mmoja kuisha na nikaenda kwa upasuaji bila kukawia.

Bartholin Cyst Ni Nini?
Bartholin’s glands zinahusika kwa kutoa maji yanayo saidia uke. Bartholin cyst ina umbwa pale ambapo Bartholin glands zina zibwa, huenda ikawa ni kufuatia maumivu ama maambukizo. Maji haya huziba gland na kuwa cyst. Wakati ambapo cyst inapata maambukizo, inajazwa na pass na kuwa abscess ama kuvimba kwenye uchungu.
Bartholin’s gland abscess/infection. (Image credit: clincalgate.com)
Matibabu yana husisha:
Sitz baths:
Kaa kwenye bafu moto kwa dakika 10-15 mara nyingi kwa siku wakati wa mchana kwa siku 3 hadi 4. Pia unaweza kunywa dawa za kupunguza uchungu unao hisi.
Kufinya kwa joto (Warm compress):
Shika taulo iliyo pashwa joto na maji moto kwenye cyst hiyo. Unaweza fanya hivi mara nyingi kwa siku.
Upasuaji
Utaratibu wa upasuaji ili kutibu Bartholin cyst iliyo ambukizwa ni kama vile:
Balloon Catheter Insertion – Mchakato huu unahusisha kukata na kukausha cyst hiyo. Baada ya hapo bomba ya plastiki iliyo na balooni ndogo inaingizwa kwenye cyst iliyo kaushwa na kujazwa na kiwango kidogo cha maji ya chumvi.
Seli mpya zinakua karibu na catheter ya balooni hiyo na kutengeneza njia ya kutoa maji. Mchakato huu huenda ukachukua wiki nne ama zaidi baada ya hapo, balooni hiyo itakaushwa na catheter hiyo kutolewa.

Marsupialization – Utaratibu huu unahusisha kukausha cyst hiyo na kushona sehemu za mwisho wa ngozi ili kutengeneza ‘kangaroo pouch’ ndogo, na kufuatia jina hilo la marsupialization. Pouch ama mfuko huu unakubalisha maji mengine kutiririka nje.
Kutolewa kwa Bartholin’s Glands – Huenda ukaamua kutolewa Bartholin’s glands iwapo matibabu ya hapo awali hayakuwa na mafanikio.
Kuzuia Uvimbe wa Bartholin Cyst
Zingatia usafi wa mwili na ufanye mazoezi ya ngono salama ili kuzuia kuambukizwa kwa Bartholin’s cyst.
Vyanzo:
Mayo Clinic
NHS UK
Pia ungependa kusoma: Woman had surgery to remove massive 26kg ovarian cyst
Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Syreeta Akinyede kisha yakatafsiriwa na Risper Nyakio.