Njia 8 Mwili Wako Una Dhihirisha Kuwa Una Uzalishaji Bora!

Njia 8 Mwili Wako Una Dhihirisha Kuwa Una Uzalishaji Bora!

Iwapo unajaribu kutunga mimba, tizama ishara hizi zinazo dhibitisha kuwa una uzalishaji bora.

Miili yetu inaweza kutujulisha mengi iwapo tutakuwa makini.  Inaweza kuonyesha wakati ugonjwa unapoanza; inaweza kutuonyesha tunapofaa kupumzika na pia inaweza kutukumbusha kunywa maji mengi mara kwa mara kwa siku. Iwapo tutauangalia vizuri, pia tunaweza kudhibitisha nafasi zetu za uzalishaji bora bila ya uchunguzi.

Hizi ndizo njia mojawapo ambazo mwili wako hukujulisha kuwa una uzalishaji bora

steady period dates

1. Vipindi vyako vya hedhi na PMS hutabirika ipasavyo

Iwapo una uzalishaji bora, mzunguko wako wa hedhi hutabirika vyema. Mzunguko wako huwa wa kati ya siku 25 hadi 35 tukinakiri hauko kwenye mpango wowote wa uzazi.  Ata kilicho cha mno, mzunguko mrefu unaweza kumaanisha kuwa una “strong ovarian reserve ama mayai mengi yaliyowekwa. PMS zinaweza kuwa mbaya, lakini pia inaweza kuwa jambo nzuri kwa vile ishara kama vile kulainika kwa matiti na uchungu unaweza kumaanisha kuwa wewe ni mama mwenye uzalishaji bora.

2. Wingi wa maji ya uke

Katikati ya mzunguko wako wa hedhi, unaweza gundua kiwango kikubwa cha unyevu usio na rangi wala kunuka. Huu ndio wakati uko bora zaidi. Pia inaashiria hali ya tezi zako za mlango wa uzazi na hali bora ya toleo la oestrogen.

3. Huwa hauna kipindi cha hedhi kizito

Ingawaje, kila kipindi cha hedhi cha mama huwa tofauti kwa kiwango na pia wakati. Ilihali wengine hupatwa na kipindi kizito kwa siku chache, vipindi vingine hutokea kwa wiki nzima na huwa nyepesi.  Ili wewe kuwa mjamzito, tabaka lako la tumbo la uzazi linafaa kuwa pana na laini vizuri. Iwapo utapata kuganda kwa damu ama kipindi kizito hili humaliza mwili wako, tumbo la uzazi kwa binafsi na huwa pingamizi kwa uterasi yako kuwa yenye afya na iliyo tayari kwa kutungwa mimba.  Wanawake walio na uzalishaji bora zaidi kwa mara nyingi huwa na vipindi vinavyotabirika.

4. Huwa una nguvu juu ya mizunguko ya kina mama wengine

Kina mama walio bora zaidi huwa na hii njia ya kujilainisha na mizunguko ya kina mama wengine. Pia, inayojulikana kama menstrual synchrony, hii huwa kwa sababu ya pheromones ambazo huwaathiri kina mama wengine ambao hukaa mara nyingi nao. Kuweza kutoa pheromones za nguvu pia ni njia mojawapo ya kuonyesha uzalishaji bora.

5. Matiti yaliyo umbika vizuri

Umbo na saizi ya matiti inaweza kusababishwa na hali ya homoni zako. Kwa hivyo kuwa na matiti yenye umbo nzuri humaanisha homoni zako zinafanya kazi vizuri kumaanisha una afya bora. Ni vyema kujua, ingawaje, ikiwa matiti yako iko kwenye upande wa umbo ndogo haimaanishi kuwa huwezi kuwa mjamzito.

pelvic pain

6. Uchungu mwingi wa pelviki? Hapana.

Ingawaje uchungu wakati wa hedhi  ni ishara njema ya afya, kupatwa na uchungu uliopita mipaka kwenye nyonga inaweza maanisha wewe si mwenye afya ulivyotarajia. Kilicho cha mno, uchungu wa muda mrefu kwenye nyonga unaweza kuwa ishara ya matatizo kama vile ovarian cysts na endometriosis.

7.  Umeshika mimba hata bila kujua kwako

super fertile women

Kushika mimba ata unapotumia upangaji wa uzazi kama vile IUD ama kutumia dawa inaweza kumaanisha kuwa mwili wako una afya. Kwa mfano, tembe za kumeza huwa na umaarufu wa asilimia 99% inayomaanisha kuwa kuna wakati kina mama walijifungua wakitumia hizi dawa.

8. Historia yako ya kimatibabu ni safi kabisa

Iwapo umeweza kutibu maambukizi ya njia ya mkojo ama pia magonjwa ya zinaa hapo awali una nafasi kubwa ya kuwa na uzalishaji bora. Iwapo umekuwa mwaminifu kwa kutembelea daktari wako wa maswala ya kina mama tangu uanze kufanya mapenzi, hivyo basi uke wako na mirija yako ya fallopia ambayo ni muhimu iko katika hali sawa kabisa.

Pia unafaa kuzingatia mtindo wako wa sasa wa maisha kama vile chakula, ratiba ya kazi, kwa vile zinaweza kuathiri safari yako ya uzalishaji bora.

*Makala haya yalichapishwa tena na idhini ya theAsianparent Philippines kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

SOMA: How Tiger Nuts Can Help Men And Women Boost Fertility

Tungependa kusikia kutoka kwako! Tujulishe mawazo yako na uwache ujumbe mdogo kwenye sanduku la maoni hapa chini. Tupe kidole cha gumba kwenye  Facebook na ufuate kurasa yetu ili upate jumbe zote za hivi sasa, Africaparent!

Written by

Risper Nyakio