Uzito Wa Wastani Wa Mtoto Katika Miezi Ya Kwanza Mitatu

Uzito Wa Wastani Wa Mtoto Katika Miezi Ya Kwanza Mitatu

Watoto hutofautiana na uzito na urefu wake utakuwa tofauti. Hata hivyo, kuna vipimo jumla vya kutarajia katika mwaka wao wa kwanza maishani.

Ni kawaida kwa mzazi kushangaa iwapo mtoto wake anakua ipasavyo na kama ana afya. Watoto wenye afya huwa wa saizi tofauti, ila mwendo wa ukuaji huwa ni rahisi kutabiri. Unapo enda kukaguliwa hospitalini, daktari atampima mtoto kuona kama anakua ipasavyo na iwapo urefu na uzito wake uko unavyo stahili kuwa. Tazama mwongozo huu wa uzito wa mtoto wa miezi mitatu.

Uzito wa kuzaliwa

uzito wa mtoto wa miezi mitatu

Shirika la Afya Duniani lime dhihirisha vipimo vya watoto na ukuaji wao. Uzito wa wastani wa watoto ni kati ya kilo 2.5 na 3.4. Kwa watoto walio zaliwa wakati walio tarajiwa ama baada ya kukomaa kabisa. Kwa watoto wanao zaliwa kabla ya wakati, huenda wakawa na kilo chini ya 2.5 na walio zaliwa wazito zaidi kuwa na kilo zaidi ya 3.5.

Sababu zinazo athiri uzito wa mtoto:

  • Wakati mama anapo jifungua: Watoto wanao zaliwa kabla ya kukomaa vyema huwa wadogo, huku wanao zaliwa baada ya wakati wanao tarajiwa wakiwa na uzito zaidi.
  • Uvutaji sigara: Mama anaye vuta sigara katika safari yake ya mimba hujifungua watoto wadogo.
  • Lishe ya mama: Lishe bora na uzito mwingi huenda kukasababisha kujifungua mtoto mkubwa, huku lishe duni ikimfanya ajifungue mtoto mdogo.
  • Historia ya familia: Kuna watoto wanao zaliwa wakiwa wadogo ama wakubwa na huenda ikawa ni historia ya familia yao.
  • Jinsia: Kwa kawaida, wasichana huzaliwa wakiwa na uzito wa chini ikilinganishwa na watoto wa kiume.
  • Mimba ya mtoto zaidi ya mmoja: Ukiwa na mimba ya mtoto mmoja, nafasi kubwa ni kuwa atakuwa na uzito mwingi, ila, unapokuwa na mimba ya watoto mapacha ama zaidi, watoto hawa watakuwa na uzito mdogo.
  • Kisukari cha gestational: Mama kuwa na kisukari katika mimba huenda kukasababisha kujifungua mtoto kubwa kuliko ilivyo kawaida.

Uzito wa mtoto katika mwaka wa kwanza

uzito wa mtoto wa miezi mitatu

Watoto hutofautiana na uzito na urefu wake utakuwa tofauti. Hata hivyo, kuna vipimo jumla vya kutarajia katika mwaka wao wa kwanza maishani.

Wiki za kwanza mbili

Katika siku za kwanza chache za maisha yao, ni kawaida kwa watoto kupoteza uzito. Haijalishi kama ana lishwa kupitia kwa chupa ama kunyonya. Na huenda wakapoteza hadi asilimia 10 za uzito wao. Na katika wiki mbili zinazo fuata, watoto huwa wame rejesha uzito wao zaliwa nao.

Mwezi wa kwanza

Watoto wengi huongeza nusu kilo katika mwezi wa kwanza wa maisha yao. Wanapo fikisha mwezi mmoja, wana punguza muda wanao lala kwa siku na kuanza kuwa na ratiba dhabiti ya kula.

Uzito wa mtoto wa miezi mitatu

Katika mwezi wao wa tatu maishani, watoto huwa na uzito wa kilo 6.4 kwa watoto wa kiume na uzito wa kilo 5.8 kwa watoto wa kike.

Hitimisho

Ukilinganisha ukuaji wa mtoto wako na wengine, huenda ukawa na shaka ukigundua kuwa wao ni wadogo ama wazito kuliko wanarika wao. Badala yake, mpeleke hospitalini afanyiwe vipimo na daktari wake kuhakikisha kuwa anakua kwa njia inayo faa.

Soma Pia: Ukuaji na Hatua Muhimu Kwa Mtoto wa Miezi Minne

Written by

Risper Nyakio