Barua wazi kwake Vanessa Bryant: Kuishi kwa dunia bila ya Kobe na Gianna

Barua wazi kwake Vanessa Bryant: Kuishi kwa dunia bila ya Kobe na Gianna

Mpenzi Vanessa Bryant, dunia imempoteza shujaa wa mpira wa vikapu na aliyetengeneza hadithi, lakini umempoteza mwenzi wako wa maisha na aliyekuwa na roho yako tangu umri wa miaka 17. Mlikuwa timu ya kufana – Kobe na Vanessa, mkilea wasichana wenu warembo pamoja.

Inaumiza sana kujua mdogo Capri hatakuwa na baba yake karibu akisherehekea mwaka wake wa kwanza wa kuzaliwa, na unamfanyaje kuelewa kuwa baba hatakuwa anarejea nyumbani tena? Na pia kuna hatua nyinginezo ambazo msichana huwa nazo maishani ambapo baba kuwa karibu ni muhimu. Sherehe za kuzaliwa, kuhitimu masomo na harusi. Nyinyi wote wawili mlifaa kushuhudia haya. Kuona  mlichoumba kikikua na kuwa huru maishani.

vanessa bryant after deaths of kobe and Gianna

GiGi, mtoto wako wa upinde, aliyekuwa anafuatia katika nyayo za babake, angeendeleza urithi wa Bryant  katika uwanja wa mpira wa vikapu- kwa majivuno – kama mwanamke. Angeonyesha dunia kuwa urithi hauna mipaka ya jinsia. Tunaheshimu nguvu, uaminifu na ushupavu wa Gianna. Tunayasherehekea maisha yake.

Oh Vanessa, hili linaweza kuonekana kama ndoto na lini litaisha hakuna anayejua. Huweza kukamilika kweli? Kila wakati tunapo amka ni ukumbusho wa wale hawako nasi tena. Tunahisi kutokuwepo kwa mguzo wao, tabasamu na joto lao. Mazungumzo nao, ubishi na upendo. Kila wakati tunapumua nikama mshale kwa nyoyo zetu. Tunahisi wao hawako tena. Twatambua kuwa Vanessa Bryant after deaths of kobe and gianna mambo mengi yata badilika.

vanessa bryant after deaths of kobe and Gianna

Mfalme hayuko tena, lakini malkia wake bado anatawala na sasa itabidi umemwonyesha binti mfalme jinsi ya kuishi. Jinsi Kobe alivyosema, “kila jambo hasi – mkazo, changamoto – zote ni nafasi kwangu kupaa.” Na utapaa Vanessa, wakati utakapowadia, lakini mpaka hapo, lazima utembee kwa hii barabara ya huzuni ambayo haina mwanzo au mwisho kamilifu. Hakuna masharti ama upeo lakini kuna majonzi, uchungu, mahangaiko, hasira na maumivu mengi. Lakini pia yote yatapita na utatabasamu na kucheka tena kwani Kobe na Gianna wangependelea hivyo.

vanessa bryant after deaths of kobe and Gianna

Tunaomboleza nawe, Vanessa Bryant, na tunakuombea Mungu azidi kukumbatia kwa upendo akikufariji wewe na familia yako katika hiki kipindi cha huzuni, pia tunamkumbuka John na Keri Altobelli na binti yao, Alyssa. Payton Chester na mamake, Sarah Chester. Kocha, Christina Mauser na rubani, Ara Zobayan.

Vanessa Bryant after deaths of kobe and gianna hata kuwa sawa na hapo mbeleni. Ila twamtakia faraja katika wakati huu. Mioyo yao ikapumzike mahali pema.

Read also: A Practical Guide To Dealing With Loss And Grief

Written by

Risper Nyakio