Vidokezo Bora Vya Jinsi Ya Kujifungua Kwa Urahisi

Vidokezo Bora Vya Jinsi Ya Kujifungua Kwa Urahisi

Kujiunga na wanawake wengine wenye mimba kutakusaidia kupunguza uwoga wa kujifungua, hasa kwa wanawake wanao jifungua kwa mara ya kwanza.

Inapofika kwa kujifungua kwa njia ya kawaida kupitia kwa uke, ni ndoto ya kila mwanamke kuwa kitakuwa kipindi rahisi, cha kasi na kisicho na uchungu mwingi. Baadhi ya wanawake huwa na bahati ya kuwa na vipindi vifupi vya uchungu wa uzazi. Lakini hasa kwa wanawake wanao jifungua mara ya kwanza, huenda kikawa ni kipindi cha kuogofya. Tazama jinsi ya kupunguza uchungu huu na kujifungua kwa urahisi.

Siri za kujifungua kwa urahisi

kujifungua kwa urahisi

  1. Hakikisha una afya nzuri na una fanya mazoezi

Kuwa na afya na kufanya mazoezi ni muhimu sana ikiwa mama angependa kuwa na kipindi kifupi cha uchungu wa uzazi. Kulingana na wakunga, wanawake wanao zidi kufanya mazoezi wakiwa na mimba huwa na vipindi vifupi vya uchungu wa uzazi. Mwanamke mjamzito anaweza fanya mazoezi mepesi kama vile kuogelea ama kutembea. Mazoezi yanamsaidia mama mwenye mimba kupunguza maumivu yanayo sababishwa na mimba na pia mzunguko bora wa damu mwilini.

2. Jiunge na vikundi vya wanawake wanao tarajia kujifungua

Kujiunga na wanawake wengine wenye mimba kutakusaidia kupunguza uwoga wa kujifungua. Hasa kwa wanawake wanao jifungua kwa mara ya kwanza. Jaribu kutafuta kikundi kilicho karibu nawe.

3. Kuwa na watu wanao kusaidia

Kipindi cha ujauzito huwa nyeti na mambo mengi sana hutendeka. Kuwa na watu watakao kusaidia mbali na mchumba wako ni muhimu sana. Msaidizi wako anaweza kuwa daktari wa afya ya wanawake atakaye kujibu maswali yote yanayo kutatiza.

Vidokezo Bora Vya Jinsi Ya Kujifungua Kwa Urahisi

4. Chagua chakula chepesi

Kula chakula chepesi unapo anza kuhisi uchungu wa uzazi ungali nyumbani ni muhimu. Utapata nishati tosha ya kujifungua. Epuka kula chakula kingi, kilicho kigumu kuchakata kwa urahisi, ama chakula chenye ufuta mwingi. Hakikisha kuwa pia unakunywa maji tosha kabla ya kuingia chumba cha kujifungua.

5. Koga kwa maji moto

Maji moto yana kusaidia kutuliza misuli yako na hisia ya kukosa starehe. Pia unaweza mwuliza mchumba wako akukande mwili. Sehemu kama miguu, shingo ama mabega. Wanawake walio pigwa masi kabla ya kujifungua walishuhudia vipindi vifupi vya uchungu wa uzazi.

Soma Pia:Mama Anapaswa Kungoja Muda Upi Kufanya Ngono Baada Ya Kujifungua?

Written by

Risper Nyakio