Vidokezo Kwa Wanao Tarajia Kuitwa Baba Katika Chumba Cha kujifungua

Vidokezo Kwa Wanao Tarajia Kuitwa Baba Katika Chumba Cha kujifungua

Mwongozo wa kumsaidia bibi yako kumkaribisha mtoto wenu duniani.

Daktari Jazlan Joosoph, mtaalum wa Obstetrics na afya ya uke katika Kitu cha Wanawake cha Raffles aliwapatia watu ushauri jinsi ya kuwasaidia bibi zao (kuto zirahi!) wanapo wakaribisha watoto wao kwenye dunia hii. Soma vidokezo kwa wanao tarajia kuwa baba.

Je, wewe na bibi yako wa kupendeza mnatarajia mtoto wenu hivi karibuni? Umeamua kuwa sako kwa bako na bibi yako anapo enda katika chumba cha kujifungua na kushuhudia uchungu wa uzazi?

Ila ngoja, na je, kuhusu hadithi hizo za kuogofya na jumbe za kusikitisha ambazo umekuwa ukisikia kuhusu shuhuda za wanawake wengine wanapo pitia uchungu wa uzazi?

Hapa kuna vidokezo 10 vya jinsi unaweza weka hizo hadithi kando na kuzingatia kujifungua kwa mtoto wako na kuwa na kuwa ushawishi chanya kwenye chumba cha kujifungua.

celebrating pregnancy announcement

Vidokezo 10 Kwa Wanao Tarajia Kuwa Baba

1. Kuwa tayari

Mke wako anapo tangaza kuwa ana mimba, ina maana kuwa utakuwa baba.

Kupumua kwa ndani - kutoka wakati mnapo gundua kuhusu ujauzito hadi siku ya kujifungua, mna wakati mwingi wa kusoma kuhusu kila kitu mnacho hitaji kuhusu watoto na kuwa baba mwema.

2. Iwapo ni kujifungua kupitia upasuaji wa C-section, usichungulie

Kuna sababu ambayo umechagua daktari aliye na ustadi. Wacha kila kitu katika mikono ya wataalum na ukae kitako ulipo agizwa ukae na uongee na bibi yako huku ukimfariji.

Kusikia maneno ya kutia moyo kutoka kwako kutamtuliza katika wakati huu wa wasi wasi mwingi.

3. Fanya kazi yako ya ziada kuhusu kujifungua

Bwana anaweza kuwa mwenzi bora zaidi wa kujifungua. Kwa hivyo soma kuhusu kuwa mwenzi wa kujifungua na ujiunge na darasa la kujitayarisha pamoja na mkeo.

Fanya kila kitu kwenye uwezo wako kuzingatia na kuwa chanzo cha nguvu badala ya ficho kwenye chumba cha kujifungua.

Mshangilie bibi yako na uwe karibu yake kum-egemeza. Na tafadhali jaribu kuto zirai - timu ya kimatibabu tayari ina mengi kiganjani mwao!

tips for dads-to-be

4. Kujifungua huwa si dharura ya kimatibabu, kwa hivyo tulia na usiwe na shaka nyingi.

Hiki ni kama kidokezo cha hapo juu. Kumbuka, bibi yako ako mikononi ya ustadi ya daktari wake na wafanyakazi wa hospitali.

Kwa hivyo jaribu kutokuwa chanzo cha kuangaliwa, badala yake zingatie kazi uliyo nayo - kuwa mwenzi wa kuegemeza na kumtie bibi yako nguvu.

5. Usiyachukulie mambo kibinafsi

Kwenye joto ya wakati, ambapo mkeo amezidiwa na uchungu, huenda akatamka matusi kama vile, "Wewe ndiyo wa kulaumiwa...!" kwako.

Tulia na ufahamu kuwa amezidiwa na uchungu. Huenda pia ikawa ni kufuatia mabadiliko ya homoni wakati wa hatua ya mwisho ya kujifungua.

Usiyachukulie kwa ubaya na kumkasirikia. Anahitaji uvumilivu wako, mwelewe kwa sasa, zaidi kuliko hapo awali.

tips dads labour suite

6. Neno la msimbo – Episiotomy

Msimbo huu ni wa "simamisha unacho kifanya na uangalie mbali!" Iwapo wewe ni miongoni mwa watu wanao zirai wakiona damu, nina uhakika hungependa kuona episiotomy ikiendelea.

7. Kuwa kwenye wakati

Kuona kipenzi cha maisha yako kiki jifungua mtoto wako ni mojawapo ya miujiza ya maisha. Dakika hizi hazitendeki kila siku, kwa hivyo, simamisha unacho kifanya na uwe kwenye upande wa bibi yako katika safari hii ya uchungu.

Kwa uwazi, dhibitisha fahari yako na kujivunia kwa hatua hii muhimu ambayo mke wako ametimiza.

8. Kuwa makini unapokata kitovu

Wababa wengi hutikwa jukumu gumu la kukata kitovu. Kwa kweli kitakuwa kipindi ambacho hakita sahaulika maishani mwako na huu sio wakati wa kuwa na hofu.

Kwa hivyo unapo kata kitovu, kuwa na umakini na uangalifu zaidi. Ni vigumu zaidi kuliko unavyo dhani.

9. Usijazwe na kero baada ya kuona placenta ikitoka mwilini.

Tena, kujitayarisha kwa mapema ni muhimu. Soma chochote utakacho pata kuhusu kujifungua na utizama video za kujifungua na mkeo.

Kuwa tayari kwa kusukuma kwa mwisho baada ya mtoto wako kutoka. Hii - placenta - haitakuwa ya kupendeza kama mtoto wako ila ni tofauti yake kabisa. Kwa hivyo itasaidia ikiwa angalau utakuwa umeona picha yake kabla ya wakati huu.

10. Soma kutoka kwa wanao fahamu wanacho kifanya

Utakapo kuwa hospitalini, utapata usaidizi mwingi kutoka kwa wafanya kazi na wauguzi jinsi ya kumshika mwanao. Usikae hapo huku umewaangalia wanavyo shika mtoto - jihusishe pia na uwaulize wakuonyeshe jinsi ya kumshika mtoto, kumtuliza na anavyo stahili kukaa baada ya kunyonya, ili uweze kusaidia anapo fika nyumbani.

Daktari Jazlan Joosoph ni mtaalum wa Obstetrics na afya ya uke kutoka Kituo cha Wanawake cha Raffles katika hospitali ya Raffles, hospitali ya utunzi wa kibinafsi na mkuu wa timu ya matibabu ya Raffles, watunzaji wa afya ya kibinafsi huko Singapore na South East Asia.

 

Soma zaidi: A Dad Dilemma: Should You Take Paternity Leave When You’ve Just Started a New Job?

Makala haya yaliandikwa na Prianka na kuchapishwa tena na idhini kutoka kwa theAsianparent kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio