Vidokezo Muhimu Vya Ulezi Kutoka kwa Maisha Ya Marehemu Kobe Bryant

Vidokezo Muhimu Vya Ulezi Kutoka kwa Maisha Ya Marehemu Kobe Bryant

Ni siku iliyo tanda majonzi na simanzi kufuatia kuamkia habari za kuhuzunisha za kifo cha mchezaji mashuhuri wa mpira wa kikapu, marehemu Kobe Bryant. Rambi rambi zetu ziwaendee jamaa na marafiki wa mchezaji huyu. Ingawa kifo chake si huzuni kwa familia yake tupu ila dunia nzima na hasa wanao upenda mpira wa vikapu.

Inasemakana kuwa Kobe na Mwanawe wa miaka kumi na mitatu(13) Gianna Bryant, na watu wengine saba, walihusika katika ajali mbaya ya ndege. Inasemekana kuwa Bryant na mwanawe walikua safarini wakielekea kwenye shule ambapo Bryant alikua kocha wao wa timu ya mpira wa kikapu ya Gianna.

Ajali hii ilitendeka baada ya ndege waliyo kuwa wakisafiria kuanguka karibu na Calabasas, Calif. Kwa kweli marehemu Kobe alikuwa mzazi wa kuigwa.

Vidokezo Muhimu Vya Ulezi Kutoka kwa Maisha Ya Marehemu Kobe Bryant

Makala haya yana angazia vidokezo muhimu vya kuigwa kutoka kwa njia ya ulezi ya marehemu Kobe Bryant

Mchezaji hodari marehemu Kobe Bryant alianza kucheza basketboli kutoka alipokuwa kijana. Baada ya kumaliza masomo yake ya sekondari, aliteuliwa na kuunga National Basketball Association (NBA) alipokuwa anaichezea timu ya Lakers. Kutoka mwaka wa 1996. Kutoka mara alizocheza NBA, 18 kwa hizi 20, aliiletea timu yake ushindi. Alikuwa miongoni mwa wachezaji bora zaidi. Ameshinda medali za dhahabu za mpira wa vikapu kwa mashindano ya olympiki ya mwaka wa 2008 hadi mwaka wa 2012.

  • Kuwapa Motisha

Mtoto wake wa kike Gianna Bryant wenye miaka 13 alizifuata nyuso za babake. Aliupenda mpira wa vikapu na akaingia katika timu ya shule yao. Ambayo Kobe alikuwa kocha wao. Ni wazi kuwa watoto hawafuati maneno ya wazazi wao, ila wanafuata matendo ya wazazi hawa. Msichana huyu amekuwa akicheza mpira huu kwa muda mrefu na kuisaidia timu yake kuibuka washindi. Ni kweli kuwa Gianna alikuwa mtoto wa babake. Ni jambo muhimu kwa kila mzazi kuwatunza wanawe na kuhakikisha kuwa wanatimiza wanachotaka maishani. Iwe katika masomo ama kazi zao.

  • Kutia bidii

Kama babake, aliendelea kutia juhudi na watu walimjua kwa ushindi alio uletea timu yake. Kobe alimsaidia mwanawe kwa kumuunga mkono na kumpa mwongozo wa jinsi anavyopaswa kucheza. Kwa kweli, mzazi ana jukumu kubwa la kuwa na maisha ya kuigwa na wanawe na pia kuwaunga mkono na kuwapa motisha ili watimize malengo yao ya kimaisha. Bidii zake alipokuwa anacheza zilikuwa za wanawe. Wafuate nyoyo zake na pia ili aweze kuyakimu mahitaji yao. Kuwapa maisha bora na wasiwahi kosa chochote walicho taka maishani.

marehemu kobe bryant

Marehemu Kobe Bryant na familia yake

  • Kuwa wazazi wa kuigwa

Katika mwaka uliopita, babake Gigi, jina lake la mkato Gianna, alimsifu mwanawe na kuiambia ‘The Los Angeles Times’ kuwa mwanawe angependa kuichezea UConn(University Connecticut) na baadaye W.N.B.A (Women’s National Basketball Association). Kobe alikuwa amecheza mechi za juu ambazo aliweza kushinda. Jambo hili lilimpea mwanawe nguvu na alitaka kuwa kama babake. Gigi alizidi kuwakumbusha watu kuwa babake, hakuhitaji mtoto wa kijana aendeleze jina lake. Kwani hata kama alikuwa msichana, angeiendeleza legacy ambayo babake alikuwa ametengeneza tayari.

  • Kuwapenda na kuwahimiza watoto wake

Kila wakati, alipokuwa na wasaa zaidi, Bryant alimfunza Gigi, jinsi ya kucheza mpira wa vikapu. Mwanawe alionekana akitumia tactics za babake alipokuwa anacheza na kusaidia timu yake kushinda. Babake pia alikuwa kocha wa timu ya mwanawe. Aliwabeba watoto wake na kuwapeleka kushuhudia mechi za mipira ya vikapu timu mashuhuri zilipokuwa zinacheza. Pia, aliwapa ushauri jinsi ya kucheza na wapinzani wao. Kila mara Gigi alipocheza, babake angetuma video zake kwa meneja mkuu wa timu ya Lakers, Rob Pelinka aliyekuwa babake wa ubatizo.

Kifo chake kilitendeka muda mfupi kabla ya mechi za Mamba Cup Tournament Series ambapo wavulana na wasichana wa kiwango cha masomo kutoka cha 3 hadi cha 8 walihusika. Timu ya Gigi ilikuwa na mechi dhidi ya Fresno Lady Heat. Michezo hizi zote ilighairiwa baada ya kuzipokea habari za kifo cha Bryant na mwanawe Gigi. Wanatimu wake walipiga magoti na kuwaombea wawili hawa baada ya kupata habari za ajali yao.

Vidokezo Muhimu Vya Ulezi Kutoka kwa Maisha Ya Marehemu Kobe Bryant

Familia ya marehemu Kobe Bryant

Maisha ya Bryant yalikuwa ya kuigwa. Alikuwa mpenda watu na familia yake ilisifika kote. Hakuwa mchezaji tu, ila alikuwa mume wa Vanessa Laine Bryant, walio funga pingu za maisha mwaka wa 2000. Na baba wa watoto wao wanne Gianna Maria, Natalia Diamante, Bianka Bella, Capri Kobe. Aliweza kutenga wakati wa kucheza na wa familia yake. Alijihusisha katika maisha ya wanawe katika vyote walivyofanya. Jambo ambalo si wengi wanaoweza kufanya hasa unapokuwa na maisha ya umaarufu.

Jumbe za rambi rambi

Rais ya U.S.A Donald Trump alisema kuwa ” Hataingawa Bryant alikuwa amestaafu, alikuwa ameyaanza maisha yake tu. Na alikuwa na mengi ya kufanya na kukamilisha maishani” Trump alisema. Wasanii wengi kama vile Alicia Keys walituma rambi rambi zao, na kuifungua sakafu ya Grammys 2020, kwa kutuma jumbe zao za pole kwa familia yao. Taylor Swift na wengineo walituma jumbe zao pia. Ni wakati mgumu kwa familia hii. Kupoteza watu wawili wa familia moja katika ajali moja. Ila twawatakia mema na faraja katika wakati huu.

Ni bayana kuwa kila mtoto anahitaji mzazi kama marehemu Kobe Bryant.  Kwa mara nyingine, rambi rambi zetu kwa jamaa na marafiki wa marehemu Kobe Bryant. Mungu amlinde na amlaze mahali pema peponi. Na azidi kuipa faraja familia yake wakati huu mgumu.

 

Soma Pia: kuvunjika kwa moyo

 

 

 

 

 

 

 

Written by

Risper Nyakio