Vidokezo Muhimu Kwa Wanawake Walio Na Watoto Mapacha

Vidokezo Muhimu Kwa Wanawake Walio Na Watoto Mapacha

Kwa wanawake wanao tamani kuwa na watoto mapacha ama zaidi, na kwa wanao tarajia, ni vyema kufahamu mambo wanayo paswa kuwa tayari kupitia katika safari yao ya kulea mapacha.

Kwa wanawake wanao tamani kuwa na watoto mapacha ama zaidi, na kwa wanao tarajia, ni vyema kufahamu mambo wanayo paswa kuwa tayari kupitia katika safari yao ya kulea mapacha.

Vidokezo vya wanawake vya kulea mapacha

Vidokezo Muhimu Kwa Wanawake Walio Na Watoto Mapacha

  • Kuwa tayari kulea mapacha

Kuwa tayari kwa uwezekano wa kujifungua watoto wako kabla ya wakati ulio watarajia; na huenda wakawa kwenye kitengo cha utunzi spesheli kwa wakati mfupi pia. Kutunza watoto walio zaliwa kabla hawaja komaa huwa na changamoto zake. Hakikisha una watu wa kukusaidia na majukumu mengine ili upate wasaa tosha wa kuwa na watoto wako wanapo wasili duniani.

  • Ratiba za watoto mapacha

Kuwa na ratiba kutasaidia, hata kama sio jambo rahisi unapo anza. Jaribu kuweka dokezo la kila mtoto. Kuna applications tofauti ambazo zinaweza kusaidia kufanya hivi. Haijalishi ulivyo choka, utaweza kujua walipo lala, walipo kula na walipo badilishwa. Unapokuwa na ratiba ya lishe, wakati wa kulala usiku na mchana, jaribu kuifuata vyema uwezavyo, hata wikendi. Na kubadili mara kwa mara watoto wanapo ugua. Na wanapo hisi vyema, rejelea ratiba ile.

  • Kuwalisha

Kuna wezekana kuwalisha mara nyingi, hata kama unahitaji msaada kutoka kwa mkunga na wanafamilia wa karibu. Lakini japo unavyo kuwa na watoto wengi, ndivyo ulivyo na uwezekano mdogo wa kuwanyonyesha peke yake. Kuwalisha watoto wengi mara moja huhifadhi wakati, lakini huenda ikawa vigumu mwanzoni. Baada ya muda, utafahamu jinsi kunyonyesha kunavyo fanya kazi kwako na watoto wako. Kunywa maji mengi, kwani kunyonyesha kuna kufanya uhisi kiu. Wakati wote, hakikisha kuwa una kinywaji mkononi unapo nyonyesha na jaribu kinywaji kingine kati ya vipindi vya kunyonyesha. Na kumbuka kujilisha, chakula chakula rahisi na kilicho kasi kutayarisha.

Vidokezo zaidi vya kulea watoto mapacha ama zaidi

kulea mapacha

  • Msaada zaidi

Kubali kuwa huwezi jifanyia kila kitu. Mwulize rafiki yako ama mwanafamilia akusaidie kufanya majukumu fulani; ikiwa ni kupika chakula cha usiku, kufua nguo ama kununua vyakula. Marafiki na familia yako huenda wakawa na shaka kuwa wana ingilia maisha yako na kukosa kukusaidia. Hiyo haimaanishi kuwa hawako tayari kukusaidia unapo omba msaada.

  • Usivalie mavazi

Unapo jifungua watoto mapacha ama zaidi, hautaweza kufanya kila kitu, ama hata kitu chochote kwa wiki za kwanza. Kabla ya watoto wako kuwasili, nunua mavazi ya kulala ambayo unaweza valia kwa urahisi. Kwa angalau wiki za kwanza chache, usiwe na shaka ikiwa utavalia mavazi haya mchana wote. Hakuna mgeni wako ambaye atagundua, watakuwa makini kwa watoto. Ikiwa lazima utoke nyumbani kisha ugundue kuwa umevalia mavazi haya, usiwe na shaka. Kumbuka vipau mbele!

  • Lala

Wanawake walio jifungua watoto mapacha ama zaidi hupata hulala muda mdogo ikilinganishwa na wanawake wengine walio jifungua. Ikiwa una bahati tosha kuwafanya watoto wako walale wakati sawa, chukua muda huo kulala pia. Kazi za nyumbani zinaweza ngoja. Watoto hawatajua kazi zisipo fanywa, lakini watagundua mama aliye choka.

  • Jipe muda

Miezi ya kwanza michache huwa ngumu zaidi. Kila kitu, kutoka kuwalisha watoto na kutoka kwenye nyumba huenda ikachukua muda. Huenda ukawa umechoka zaidi ya ulivyo tarajia. Lakini usiwe na shaka kwani mambo huzidi kuwa rahisi na wakati.

Chanzo: KidsHealth Today

Soma Pia:Mambo 5 Unayo Paswa Kujua Kuhusu Mimba Ya Mapacha

Written by

Risper Nyakio