Wataalum Wanashauri Kufanya Hivi Ili Kumfanya Mtoto Alale

Wataalum Wanashauri Kufanya Hivi Ili Kumfanya Mtoto Alale

Vidokezo 6 kutoka kwa wataalum vya kumfanya mtoto wako alale!

Kuwatunza watoto waliozaliwa ni kazi nyingi hasa kwa mama wa mara ya kwanza. Na ambaye hawezi ngoja mtoto wake alale ili naye pia apate dakika chache alale. Kwa bahati mbaya, ni vigumu kuwataabiria watoto. Kuna maana kuwa wamama wapya watajipata kwa nafasi ambayo wamefanya yote wawezayo kuwalaza watoto ila hakuna kinacho fanyika. Gundua jinsi ya kumfanya mtoto alale.

Jinsi ya kumfanya mtoto alale kwa dakika chache

Ni kweli kuwa huwezi mlazimisha mtoto kulala wakati wowote unao hisi, ila kuna mengi ambayo unaweza kuyafanya ili kuwasaidia kupata mtindo wao wa kulala. Hapa chini kuna baadhi ya mambo ambayo unaweza fanya kumsaidia mtoto wako kulalal:

kumfanya mtoto alale

  • Tumia mwangaza kwa maarifa

Unaweza tumia mwangaza na giza kama mbinu ya kumfanya mtoto wako alale, njia sawa ambayo mwili wa mtu mkubwa kuanza kujiamsha katika mwanga wa kwanza na kuhusisha giza na kulala. Kulingana na Elizabeth Pantley, mwandishi wa The No-Cry Sleep Solution, "Mwangaza ama sitima husukuma 'kuanza' kwa mtoto. Wakati ambapo giza hufanya ubongo wake kutoa melatonin, ambayo ni homini ya kulala. Kwa hivyo hakikisha kuwa siku ya mtoto wako ina mwanga na usiku una giza ili kumsaidia kulala.

  • Mlaze mtoto wako anapo onyesha dalili

Mlaze mtoto wako kitandani anapo anza kuonyesha ishara za kulala kama vile kusinzia na sio baada yake kulala. Hili hasa sio rahisi kwa wamama wanao nyonyesha. Lakini vitu vitakuwa rahisi kwa mama na mtoto ukiwa makini na wakati. Manufaa ya kufanya hivi ni kuwa mtoto wako ata zoea utaratibu huu wa kuzoea kusinzia peke yake. Kwa hivyo, wakati wowote unapogundua kuwa amenyamaza na ana sinzia, mlaze kitandani na umwache aendeleze.

kumfanya mtoto alale

  • Epuka kumchukua mtoto wako mapema

Mara kwa mara, mtoto wako ataamka kati kati ya usingizi wake na hili ni kawaida. Walakini, epuka kukimbia na kumchukua kila mara unapo sikia akilia. Badala yake, mpe muda atulie na arudi kulala peke yake. Lakini hilo lisipo tendeka baada ya dakika chache, lazima ujaribu na umchukue kwa kasi kabla aendelee kulia kwa nguvu zaidi. Sababu kwa nini unapaswa kuwa makini na wakati huu ni kuwa kumchukua kwa mbio kutamfunza kuamka mara nyingi, wakati ambapo kumwacha kwa muda mrefu kutafanya iwe vigumu kwake kurudi kulala.

  • Epuka kumwangalia mtoto kwenye macho

Watoto huitikia wanapo patana na macho ya mtu, ambayo ni aina ya ishara ya kucheza. Kulingana na Claire Lerner, ambaye ni mshauri mkuu wa ulezi katika Zero to Three, wazazi ambao huwaangalia machoni watoto wanao sinzia, huwafanya watoto waamke. "Unapo zidi kumwangalia wakati wa usiku, ndivyo unavyo mhimiza kuamka," alisema. Kwa hivyo unapo enda kwa mtoto wako usiku, jaribu kuto mwangalia kwa uso, kuongea kwa nguvu ama kuimba wimbo.

how to make a baby sleep

  • Punguza kumbadilisha diaper

Huenda ukahisi haja ya kumbadilisha mtoto wako diaper kila mara anapo amka, jaribu na kuepuka hamu hii. Mtoto wako hahitaji hivi wakati wote na huenda ukam muamsha. Badala yeke, nusa kwanza ili uwe na uhakika kuwa mtoto wako anahitaji kubadilishwa kisha utumie vipanguzio vyenye joto kuepuka kumfanya mtoto aamke.

  • Mlishe mtoto vyema

Kumlisha mtoto wako usiku kunaweza msaidia kulala kwa muda mrefu zaidi. Wakati bora wa kufanya hivi ni kati ya saa nne za usiku na kati kati ya usiku. Ili kufanya hivi, mwinue mtoto kwa upole, kisha umlaze chini na umguse kwa upole ikiwa hajaamka vizuri akule. Baadhi ya wakati huenda ukawa na bahati kugundua kuwa mtoto wako asha amka na ako tayari kula bila kumgusa. Unapo maliza, mwekelee kwenye kitanda chake kwa upole ili asiamke.

Huenda wakati ukafika ambapo mtoto ataanza kuamka usiku, na jambo hili halipaswi kukutia uwoga. Ni kawaida kwa watoto wachanga, hasa kunapokuwa na mabadiliko kwenye ratiba, kutembea ama ugonjwa. Tiba ya hili ni kurdi kwa mambo ya msingi na kufuata ratiba ya kawaida ilivyo kuwa hapo mwanzoni.

Soma pia: Aina 6 Ya Vyakula Vinavyo Tatiza Ukuaji Wa Mtoto Wako

Chanzo: Baby Center, Web MD

Written by

Risper Nyakio