Kwa mwanamke anayeanzia safari ya ujauzito, vidokezo hivi vya mimba yenye afya vitakuwa na manufaa kwake.
Vidokezo vya mimba yenye afya
- Kudumisha afya katika ujauzito

Kuwa na afya bora katika mimba ni muhimu kwa afya ya mama na mtoto. Chakula chenye afya, protini, mboga za kijani na nafaka nzima. Maji na fiber ni nzuri katika kipindi hiki kuepusha dhidi ya kuvimbiwa. Vileo na sigara huwa na athari hasi kwa fetusi, mama mjamzito anapaswa kujitenga navyo.
2. Chukua vitamini za kabla ya kujifungua

Kwa wanawake wanaopanga uzazi, wanaweza kuchukua vitamini hizi wanapoanza juhudi za kushika mimba. Ikiwa mama atapata mimba asipotarajia, anapaswa kuanza kuchukua tembe hizi mara tu anapopata ujumbe kuwa ana mimba. Ni muhimu katika kumwepusha mtoto dhidi ya magonjwa kama neural tube ama matatizo ya uti wa mgongo.
3. Mazoezi mepesi

Wanawake wengi huwa na shaka iwapo ni salama kwao kufanya mazoezi wanapokuwa na mimba. Mazoezi ni muhimu katika kuwa na mimba yenye afya. Hata hivyo, mazoezi katika mimba inapaswa kuanzilishwa na kibali kutoka kwa daktari. Kwa wanawake wanaofanya mazoezi magumu kabla ya kupata mimba, wanaweza kufanya mazoezi, na ambayo hayawashinikizi. Kwa wanawake ambao hawakuwa wakifanya mazoezi hapo awali, wanaweza kufanya mazoezi mepesi.
4. Jielimishe zaidi

Kusoma mambo mapya kila mara kuhusu mimba humpa mama ujasiri wa safari ya mimba. Mama hasa wa mara ya kwanza huenda akawa na shaka nyingi kuhusu safari hii mpya. Mwili wake unabadilika na anakipitia kipindi kipya asichokuwa na ujumbe wowote kukihusu. Ikiwezekana, zungumza na wanawake walio na watoto kupata ujumbe zaidi kuhusu mambo ya kutarajia.
5. Nunua mavazi ya mimba
Mwili wa mama hubadilika anapokuwa na mimba. Uchovu kufuatia uzito zaidi wa fetusi huenda ukamfanya afure miguu na kuumwa na mgongo. Viatu visivyo mshinikiza pamoja na mavazi mapana ni bora katika kipindi hiki.
6. Pumzika vya kutosha

Sote tunajua kuwa mama halali siku za kwanza baada ya kujifungua. Kwa hivyo sasa hivi kabla ya mtoto wako kuwasili, hakikisha kuwa unachukua kila dakika ya zaidi unayopata kupata usingizi zaidi.
7. Badilisha kazi za kinyumbani
Kipindi cha ujauzito huwa nyeti na mwanamke anapaswa kuwa makini na mambo anayoyafanya katika muda huu. Ikiwa mama anafanya kazi kwenye mazingira yaliyo na kemikali nyingi, ni vyema kubadilisha. Kemikali hizi zina athari hasi kwa mama na mtoto. Koma kufanya kazi zinazohusisha utumiaji wa kemikali, kusimama kwa muda mrefu, kutembea kwa kipindi kirefu ama kupanda ngazi.
Soma Pia: Sababu 3 Kuu Za Maumivu Ya Tumbo Katika Mimba