Vidokezo Vya Kuwa Na Uhusiano Wenye Mafanikio Kutoka Kwa Mwigizaji Olu Jacobs

Vidokezo Vya Kuwa Na Uhusiano Wenye Mafanikio Kutoka Kwa Mwigizaji Olu Jacobs

Huenda watu wengi wakakosa kufahamu kuwa Olu Jacobs na bibi yake wamekuwa kwa ndoa kwa miaka 34. Tuna angazia vidokezo vya uhusiano vilivyo wasaidia miaka hii yote.

Inachukua ujasiri kumpa mtu mwingine roho yako, na inachukua mtu kujitolea mhanga kumpenda mtu na kumkubalisha katika nafasi yake kwa miaka mingi. Tuna angazia vidokezo vya uhusiano kutoka kwa mwigizaji mashuhuri kutoka Nigeria, Olu Jacobs.

Vidokezo 9 vya uhusiano wenye mafanikio

Olu Jacobs na bibi yake Joke Silva ni mojawapo wa wanandoa wazee zaidi katika tasnia ya uigizaji Nigeria na wamekuwa kwa ndoa kwa miaka zaidi ya 30. Pia, wata kujuza kuwa haijakuwa jambo rahisi. Kwa hivyo, wame weza kivipi kuwa pamoja muda huu wote? Tuna orodhesha baadhi ya vidokezo vya uhusiano kutoka kwa Olu Jacobs na bibi yake Joke Silva.

olu jacobs and joke silva

  1. Kuto kuwa mbinafsi

Joke Silva ana shauri kuwa ili uhusiano wenu ufuzu, unapaswa kusoma jinsi ya kumtamkia mwenzio mema. Ikiwa unafikiria kilicho bora kwa mwenzi wako naye pia anafikiria kilicho bora kwako, nyote wawili mtakuwa na furaha.

  1. Wekeza wakati wako

Ndoa ni wekezo linalo chukua muda mwingi kupata matunda, kulingana na wanandoa hawa. Nyote mnahitajika kuwekeza wakati wenu, nishati, pesa na wewe mwenyewe.

  1. Kubadilisha mwanya wa tofauti

Olu Jacobs ana shauri kuwa unapaswa kuwa makini kwa sababu, kitu ambacho kinaweza kupendeza huenda kikakosa kumpendeza mwingine. Hata mkiwa mmeoana, wanandoa bado ni watu tofauti walio kua vitofauti. Heshimu maoni ya mwenzi wako kwani mara kwa mara yatakuwa tofauti.

  1. Fahamu kumsamehe mwenzi wako

olu jacobs joke silva

Usipo soma jinsi ya kumsamehe mwenzi wako kwa uaminifu, uhusiano wenu hauta tendeka kwa sababu hakuna mmoja wenu asiye na madoa yake. Pia, ni vyema kuwa mwaminifu.

  1. Jenga pamoja

Wanandoa hawa ni picha nzuri ya watu walio kuja safari ndefu wakisaidiana kukua. Bibi yake Jacobs aliwashauri wanandoa wachanga kuwa na hisia zenye afya kuhusu pesa. "Mna jenga ufalme weny pamoja," alisema.

  1. Usikubali kuingia kwa shinikizo la wanajamii

olu Jacobs family

Shinikizo kwa wanawake kutoka kwa jamii ni nyingi. Kuna mengi yanayo hitajika kutoka kwa wanawake na wasipo timiza, wana hukumiwa vikali. Bi. Silva anawashauri wanawake kujikubali na maisha yao yatakuwa sawa.

  1. Bibi yako ni mpenzi wako sio mtumwa wako

Katika mahojiano, Bw. Jacobs alipo ulizwa siri ya ndoa yake. Alisema:"Ni neema ya Mungu. Na kujifunza kuwa mpole na kuwa marafiki. Bibi yako ni mpenzi wako; sio mtumwa wako. Hauwafanyii wanawake hivyo. Usimfanye ahisi kana kwamba yeye ni mdogo wako. Kama yeye ni rafiki yako, kuwa mpole naye".

  1. Kuwa mpole na mwaminifu

Kitu ambacho kinasaidia wakati wote ni upole. Na kadri inavyo wezekana, jaribu kuwa mwaminifu na mchumba wako, na uaminifu wenye mapenzi. Kuna uaminifu usio jali, wenye makali na wenye mapenzi. Hakumaanishi kuwa hauta kasirika, lakini haupaswi kupitisha mipaka na kumshambulia. Kushambulia mtu sio kifizikia tu; huenda kukawa kihisia pia. Walakini, mwisho wa siku, mwenye umuhimu zaidi ni Mungu.

  1. Mwisho haupaswi kuwa mwisho wa maisha yako

Baadhi ya visa huenda vikapelekea kufika kikomo kwa ndoa, lakini mwisho wa ndoa haupaswi kuwa mwisho wa maisha yako. "Kuna maisha baada ya kutengena na mwenzi wako ama talaka," Bi. Silva alihitimisha.

Soma pia: Je, Mwanao Ana Mchumba? Vidokezo Hivi Vitakusaidia Kumwongoza Katika Uhusiano Wake

The Net

Written by

Risper Nyakio