Umuhimu Wa Vidoli Vya Ngono Vya Wanandoa Na Umuhimu Wake Katika Ndoa

Umuhimu Wa Vidoli Vya Ngono Vya Wanandoa Na Umuhimu Wake Katika Ndoa

Vidoli vya ngono havijakubalika sana katika bara la Afrika. Ila je, ni ukweli kuwa vinasaidia kuboresha utangamano kati ya wanandoa?

Wakati mwingi hatuangalii vidoli vya ngono vya wanandoa kama kitu kizuri nchini Kenya, kufuatia jamii yetu inayo kuwa na imani za kale. Sio wakati mwingi ambapo tunapata na watu walio pata masomo ya ngono mbali na tisho, “iwapo mwanamme atakugusa, utapata mimba” kutoka kwa wazazi wao. Mtazamo huu umekuwa sababu kuu wa jinsi tunavyo tazama ngono na mahusiano.

Kwa hivyo watu mashuhuri wanapo ongea kuhusu umuhimu wa wanawake kuwa na vidoli vya ngono kama vile vibrators kama hatua ya kujua zaidi kuhusu miili yao, nili tarajia kuona watu wakitoa maono hasi. Walakini wakati mwingi ni watu wachache tu ambao hawakubalini nao. Kisha, kura zilipangwa kupata maono na hisi za watu iwapo walikuwa na kitu chochote dhidi ya vidoli vya ngono na maono mawili yalikuwa ya kipekee, mtu mmoja hakuona umuhimu wa wanandoa kuwa na vidoli vya ngono ambapo mwingine alisema kuwa hakuna kitu ili jambo njema mashuhuri.

sex toys in marriage

Picha: Pixabay

Ila, ingekuwaje kama tunge angazia vidoli hivi kama kifaa cha kuboresha na kutajirisha uzoefu wa ngono kati ya wanandoa badala ya upinzani?

Licha ya kibali cha machapisho kama haya, ilikuwa dhahiri kuwa bado kuna imani zisizo za kweli kuwa vidoli vya ngono vinatumika badala ya mwenzi wako.

Vidoli Vya Ngono Vya Wanandoa

Olivia Sose

Picha: Olivia Sose, Owner of Ohlive Pleasures

Olivia Sose, mwenye duka la mtandao la vidoli vya ngono, Ohlive Pleasuresina maarifa zaidi jinsi ya kutumia vidoli vya ngono na vinavyo athiri utangamano kati ya wanandoa.

Mtazamo Kuhusu Vidoli 

Sidhani tuna mazungumzo wazi kuhusu ngono bado. Nchi kama Nigeria na Kenya bado haziko tayari kwa mazungumzo haya. Hivi karibuni ama baadaye, utaitwa majina mabaya kwa kuji eleza ki mapenzi kama mwanamke. Watu siku hizi hawani tusi kwa kuuza vidoli vya ngono. Haina maana kwamba wamekubaliana na jambo hili, wamegundua tu kuwa hawani babaishi, kwa hivyo wananiwacha niwe.

Nina imani kuwa vidoli vya ngono vinaweza kuiboresha uhusiano kati ya wanandoa. Hii ni kwa sababu kuna kiwango kipya cha mazungumzo ambacho kina tendeka kati ya watu wawili wanao tumia vidoli vya ngono. Wana tosheka zaidi, wako huru na kila mmoja anaamini mwingine. Wameweza kutengeneza mazingira ambapo hakuna mmoja kati yao anaweza mhakimu mwingine na jambo hili lina boresha uhusiano wao.

Vidoli vyema zaidi kati ya wanandoa

Vidoli vilivyo bora zaidi kwa wanandoa vinapaswa kuwa vile ambavyo havifanyi mmoja kati yao kuhisi amebaki nje ama mdogo wa mwingine. Ninge shauri vidoli ambavyo havifanani na moja wapo ya viungo vya mwili kwa njia yoyote ile. Vidoli ni kama bullets, finger vibrators, penis rings, magic wands na vinginevyo. Vidoli hivi kwa ujumla vinatumika kuchochea sehemu za nje ya mwili ambavyo vinaweza tumika kwa jinsia yoyote. Pia inaweza tumika wakati wa ngono kwenye chuchu ama uke ambalo ni jambo chanya kwa sababu litakuwa jambo ambalo mwenzi wako hatasahau.

Vidoli vya ngono wakati wa lockdown ya coronavirus

Nili viuza vidoli vyote nilivyo kuwa navyo katika msimu huu na kwa sasa naongeza vingine. Katika wakati huu, wanandoa wanapaswa kuhakikisha kuwa wana viosha vidoli vyao kwa kutumia maji na sabuni. Na kuvi hifadhi katika pahala pasafi palipo kauka.

Umuhimu Wa Vidoli Vya Ngono Vya Wanandoa Na Umuhimu Wake Katika Ndoa

Vitu 3 vya kutilia maanani kabla ya kuanzisha vidoli vya ngono katika chumba chenu cha kulala

Iwapo ungependa kuanzisha vidoli vya ngono katika chumba chenu cha kulala, hapa kuna vitu ambavyo unapaswa kuzingatia;

  • Usimshtue mwenzako

Mnapaswa kuwa na mjadala na mwenzako kabla ya kuanzisha vidoli vya ngono. Hakikisha kuwa unapata maono kutoka kwa mwenzao iwapo wanataka kujaribu vitu vipya nawe. Hata kama wamekuwa wakivitumia wakiwa peke yao, kuvitumia na mwenzi wao ni jambo jipya kwao.

vidoli vya ngono vya wanandoa

  • Tafuta kifaa ambacho nyote mko huru kutumia

Unapo chagua kidoli cha ngono, Olivia aliwashauri watu watafute kitu ambacho wanandoa wote wawili wanafurahikia na kutumia wote. Kwa njia hii, hakuna anaye hisi kana kwamba amebaki nje ama hatoshelezwi.

  • Ongea, ongea, ongea

Mazungumzo ni jambo muhimu sana katika kila uhusiano. Kuweni na mazungumzo kabla ya kutumia vidoli vya ngono, mkivitumia na baada ya kuvitumia kama njia ya kupata maoni ya mwenzako.

 

Soma pia11 Ways To Turn Your Wife On Before Having Sex

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Lydia Ume kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio