Jinsi Ya Kutumia Vifaa Hivi Vya Nyumbani Kusafisha Nyumba Yako

Jinsi Ya Kutumia Vifaa Hivi Vya Nyumbani Kusafisha Nyumba Yako

Products that can be used in more than one way are great for saving money. Check out these homemade cleaning agents from everyday household items

Kuna baadhi ya vitu tunavyo kuwa navyo nyumbani ambavyo vina matumizi machache ambayo tunajua. Ila, utapigwa na duwaa kujua kuwa vina umuhimu mwingi, hasa inapofika wakati wa kusafisha. Hapa kuna baadhi ya vifaa vya nyumbani vya kila siku vya kusafisha ambavyo vitaisaidia nyumba yako kung'aa na kukusaidia kuhifadhi pesa zako.

Vifaa vya nyumbani vinavyo tumika kusafisha

1. Mafuta ya neem 

Neem ni mtu ulio maarufu sana Kenya na una majina tofauti kulingana na sehemu ya nchi unako ishi. Inapo tengenezwa kuwa mafuta, inaweza tumika kufanya vitu tofauti. Mafuta ya neem husaidia kutoa dandruff, kupunguza uchungu wa mifupa na kuisaidia nywele yako iwe nono na yenye nguvu na pia iwe ndefu zaidi. Ina tumika kupunguza alama za uzee, kuisaidia ngozi yako kuwa laini na ing'ae. Kama kifaa cha kusafisha cha nyumbani, matumizi yake ni kama:

 • Kusafisha jikoni
 • Kufanya vitu vidumu zaidi

2. Sharubati ya ndimu 

vifaa vya nyumbani vya kusafisha

Ndimu ni kitu ambacho watu wengi huwa nacho nyumbani. Na hata kama hauna, ndimu zinaweza patikana kwa urahisi. Watu wengi hawa fahamu umuhimu wa ndimu. Zina saidia kupunguza uchungu kooni, kupunguza alama za uzee na pia kupunguza mashimo ya ngozi yako. Kwa kuongeza, kama kifaa cha kusafisha cha nyumbani, zinaweza tumika:

 • Kutoa uchafu kwa vitu
 • Kusafisha bakuli ya choo
 • Kusafisha kifaa cha kukatia nyama ama mboga
 • Kufanya vitu viwe vyeupe (whitening)

3. Baking soda

homemade cleaning agents

Jiko nyingi za wana Kenya huwa na baking soda, ila mara nyingi inatumika kwa kuoka peke yake. Ila, ikiwa hujui, baking soda huwa na faida nyingi. Upele unao onekana kwa mtoto kufuatia kuvalia diapers huenda ukatibiwa na kifaa hiki. Pia, kinaweza tumika kama dawa ya meno na deodorant. Nyumbani inaweza tumika kusafisha:

 • Oven
 • Kusafisha friji
 • Kuosha tubs za kuogea na kufanya bafu ing'ae zaidi

4. Mafuta ya nazi

vifaa vya nyumbani vya kusafisha

Mafuta ya nazi yanaweza kusaidia kufanya mengi nyumbani na pia mwilini wako. Kuna njia tofauti za kukuna mafuta kutoka kwa nazi. Na mafuta hayo yanaweza tumika kusafisha mbao na kutoa alama za uzee. Pia yanaweza tumika kupunguza maumivu ya kichwa. Na pia kama deodrant na kwa midomo ili iwe laini. Nyumbani yanaweza tumika:

 • Kusafisha mbao

5. Vinegar nyeupe

Vinegar nyeupe ina matumizi mengi. Inaweza tumika kufanye meno iwe nyeupe zaidi, kusaidia mayai yasipasuke unapo yachemsha. Pia, ni njema katika kufanya ngozi yako iwe laini kwa kutoa seli zilizo kufa. Matumizi mengine ya vinegar nyeupe ni kama vile kutoa dandruff kwenye nywele, kutibu unapo umwa na wadudu na kuuwa magugu shambani. Matumizi ya nyumbani ni kama vile:

 • Kutoa madoa
 • Kusafisha oven na friji
 • Kuondoa harufu mbaya
 • Kusafisha bafu
 • Kusafisha CDs and DVDs

6. Mafuta ya olive 

Kuna njia nyingi ambazo unaweza tumia mafuta ya olive kwa mwili wako na nyumbani. Mafuta ya olive yana bei nafuu na yanaweza nunuliwa kwa urahisi madukani. Inaweza tuliza koo inayo uma; kutoa mafuta kutoka kwa nywele yako, na kutoa upele usoni. Mafuta ya olive yanaweza tumika kusafisha nywele, jeli ya kunyoa na kama lubricant ya mlango unaofanya kelele nyingi. Kama kifaa cha kuosafisha unapokuwa nyumbani ni kama vile:

 • Kuosha mikono yenye mafuta
 • Kusafisha vitu vya mbao (Furniture polish)

Soma pia: Everything You Should Know About Viral Gastroenteritis In Children

Chanzo: Healthy Food House

Written by

Risper Nyakio