Mtoto Aliyezaliwa Miguu Kwanza: Kuangazia Hatari Za Kutofanya Upasuaji Wa C-section

Mtoto Aliyezaliwa Miguu Kwanza: Kuangazia Hatari Za Kutofanya Upasuaji Wa C-section

Reports say a consultant gynaecologist decapitated a breech baby by pulling on its legs when she should have performed a C-section...

Nini sababu kuu ya vifo vya watoto wachanga? Mama anapoambiwa kuwa mtoto aliyembeba hajakaa vizuri tumboni la uzazi ama atazaliwa miguu kwanza bila shaka atahofia kama kuzaa kutakuwa shwari.

Baada ya yote, watoto wanaozaliwa kichwa kwanza ndio huzaliwa mara nyingi. Mwanamke anayetarajia kuwa mama hujaribu kutuliza woga wake kwa kuongea na daktari wake ama kufanya utafiti juu ya vyanzo vya kufa kwa watoto waliozaliwa miguu kwanza.

Lakini hakuna kiwango cha utafiti ambacho kinaweza kumtayarisha mama kupoteza mtoto na kwa njia moja ya kushtua sana.

Kulingana na jarida la The Guardian, mama wa miaka themanini huko Dundee, Scotland alitiishwa kwa utabibu mbaya uliopita mipaka wakati alikuwa anajifungua.

Mama, aliyefahamika tu kama Mgonjwa A, alikuwa amebeba mtoto aliyekuwa hajakaa vizuri tumboni la uzazi. Angeambiwa kuwa upasuaji ulikuwa ndio njia mwafaka na salama kwake. Ingawaje, ripoti zinaonyesha kuwa daktari alimhimiza kuzaa kwa njia ya kawaida. Ili kuepukana na upasuaji ambao huenda ukasababisha vifo vya watoto wachanga.

mtoto mchanga afa baada ya kuzaliwa

Vyanzo vya vifo kwa watoto waliozaliwa miguu kwanza:  Ripoti zinasema daktari wa wanawake alimlazimisha kuzaa mtoto

Daktari Vaishnavy Laxman, mshauri na daktari wa wanawake aliye na umri wa miaka 41, inasemekana alimwagiza huyo mama kusukuma mtoto ilihali yeye alivuta miguu. Mtoto alikuwa na kunga ya uzazi iliokuwa imetoka mahali pake, hatari ambayo hutokea mara kwa mara.  Kwa vile mtoto alikuwa dhaifu na hakuwa amefikisha wakati wake, hio nguvu ilibandua miguu, mikono na kiwiliwili kutoka kwa kichwa.

Habari za kutikisa zaidi ni kuwa ripoti inasema mama huyo bado alikuwa katika awamu za kwanza za uchungu wa uzazi.  Maji yake yalikuwa tu yamevuja na mlango wa tumbo la uzazi ulikuwa umepanuka sentimeta tatu wakati daktari alijaribu kumsaidia kuzaa mtoto.

Baadaye, ripoti zilionyesha kuwa mtoto alikuwa na mipigo ya moyo iliyopunguka, lakini alikuwa hai yalipotendeka. Charles Garside, wakili katika baraza la General Medical alisisitiza kuwa Daktari Laxman  alifanya  “uamuzi mbaya.”  Alitilia mkazo kuwa daktari “hawafai kuwazalisha watu kwa njia ya kawaida katika hio hali.”

Mama huyo aliyekuwa amefadhaika alielezea katika korti ya madaktari vile alivyo lazimishwa kulala kitandani.  Licha ya yeye kupinga, walijaribu kukata mlango wa tumbo la uzazi mara mbili bila ya kumwambia.  Hakukuwa na dawa za kupunguza uchungu na aliwaambia wazi waache lakini malalamshi yake hayakusikika.

Baada ya kugundua walicho kifanya, madaktari wawili walimfanyia upasuaji ili kumtoa mtoto na kujaribu kuunganisha kichwa cha mtoto na mwili.  Pia walimpa mama mtoto amshike ili amuage kwaheri.

sababu ya vifo vya watoto wachanga

Kama tulivyosema awali, upasuaji wa dharura ungekuwa chaguo mwafaka na salama. Ikizingatiwa kuwa mlango wa tumbo la uzazi wa mama haukuwa umepanuka kikamilifu, upasuaji ungekinga kutokana najanga hili. Kosa moja la daktari liligharimu maisha ya mtoto huyo.

La kuhuzunisha ni kuwa, hii si kasha pekee. Hapo nyuma mwaka wa 2012, mtoto huko Brazil alikatika kichwa baada ya mabega yake kukwama katika njia ya uzazi.  Lakini mtoto hakuwa amekaa miguu kwanza tumboni la uzazi, kwa hivyo sehemu zingine za mwili zilibaki katika tumbo la uzazi. Miaka sita awali, huko Kentucky USA, mtoto alikatwa kichwa wakati wa taratibu ya kutengeneza mlango wa tumbo la uzazi.

Kati ya asilimia 3- 4 za mimba yote, kutakuwa na watoto watakao zaliwa miguu kwanza badala ya kichwa kwanza.  Kuna sababu nyingi kwa nini mtoto hukaa vibaya tumboni la uzazi. Mwanzo, iwapo mama amezaa watoto wengi ama ni mjamzito na mapacha kuna uwezekano wa kuwa na mtoto aliyekaa miguu kwanza tumboni.  Kina mama ambao wamepata watoto kabla ya wakati wao pia wako kwenye hatari ya kupata mtoto aliyekaa miguu kwanza.

kuzaliwa miguu kwanza

Nini husababisha mtoto kuzaliwa miguu kwanza na kina mama wanawezaje kujifungua salama?

Mtoto kukaa miguu kwanza husababishwa na kuwa na maji mengi au kidogo inayomzingira anapokuwa tumboni la uzazi.  Kwa nini? Mtoto ana nafasi kubwa ya kupinda na kutembea mle. Umbo la tumbo la uzazi na hali kama vile Placenta Previa huongeza athari za hili kutokea.

Mbali na kuwa mtoto aliyekaa vibaya kichwa huwa juu kwenye tumbo la uzazi, ni sawa tu na mimba ya kawaida.  Hatari halisi hutokea wakati wa kujifungua. Mtoto anapokuwa amekaa miguu kwanza ana hatari kubwa ya kukwama kwenye njia ya uzazi.  Pia kuna uwezekano kuwa kunga ya uzazi itafinywa ama kukatika mbele ya wakati.

Ili kukinga kutokana na sababu chache na za kuhofisha za vifo vya watoto wachanga waliokaa vibaya, uchunguzi uliofanywa hapo awali ulidai kuwa upasuaji ndio njia salama na mwafaka kwa watoto waliokaa miguu kwanza.

Jarida la British la Obstetrics and Gynaecology liliegemea kwa haya madai.  likisema kuwa ata kama mhudumu wa afya anaweza kuzalisha mtoto aliyekaa miguu kwanza salama upasuaji ndio njia salama katika hii hali.

 

 

Sources: The Guardian, The Huffington Post, Healthline

WATCH: Doctor turns a breech baby while in the womb!

This articles was published with permission from theAsianparent Singapore

Written by

Risper Nyakio