Vigari Vya Watoto Vya Kutembea: Madaktari Wataka Vipigwe Marufuku

Vigari Vya Watoto Vya Kutembea: Madaktari Wataka Vipigwe Marufuku

In addition to causing bad injuries, baby walkers can also interfere in the development of a baby's motor skills.

Vigari vya watoto vya kutembea vyaweza onekana kama suluhu kwa tatizo la mzazi aliye na wasi wasi. Tatizo hili ni kuwa watoto hujiingiza kwa mambo nyingi kwani wanataka kufumbua kila kitu kila wakati. Unaweza kuwa unawaza ata saa hizi, ni wakati upi mwafaka wa kigari cha mtoto cha kutembea ili kudhibiti hali hii.

Basi wazazi, hakuna wakati mwafaka wa kigari cha mtoto cha kutembea, kama wanavyosema madaktari wa watoto.  Hii ni kwa sababu vifaa hivi vinaweza kusababisha madhara mengi kuliko manufaa kwa watoto.

vigari vya watoto

Hakuna wakati sawa kwa kigari cha mtoto cha kutembea, hakuna faida kwa kukua kwa mtoto

Huko USA na kila mahali pengine ulimwenguni, vyumba vya hospitali vya dharura hutibu maelfu  ya watoto kila mwaka. Kutokana na ajali zinazosababishwa na magari ya watoto ya kutembelea.  Hata kulikuwa na mtoto karibu afe mwaka uliopita huko Hong Kong.

Kulingana na utafiti uliokuwa kwenye jarida la Pediatrics uliochapishwa Jumatatu 17 Septemba, “ zaidi ya watoto 200,000 chini ya umri wa miaka 15 walitibiwa huko USA. Katika wadi za matibabu ya dharura  wakiwa na fuvu  iliyovunjika, majeraha ya ubongo, mifupi iliyovunjika na majeraha mengine yaliyotokana na magari ya watoto ya kutembea kutoka mwaka wa 1990 hadi 2014.

Sasa, baada ya kugadhabishwa na ajali hizi ambazo zinaweza epukika, madaktari wa watoto wanataka zipigwe marufuku mara moja.

Daktari Benjamin Hoffman, ni daktari wa watoto na mwenyekiti katika kamati ya American Academy of Pediatrics on Injury, Violence and Poison Prevention.

Anasema, “Maoni yangu ni kuwa magari ya watoto ya kutembea, ni vifaa vyenye hatari na havina faida yoyote ile, na havifai kuuzwa huku U.S.”

Kigari cha mtoto cha kutembea hufanya nini?

Kigari cha mtoto cha kutembea kimeundwa kumsaidia mtoto ambaye bado hajakomaa kutembea. Vifaa hivi huwa na mwangaza mwingi na migurudumu minne kuviwezesha kutembea.

Ingawaje, kutembea bila usukani kwa migurudumu badala ya miguu yao huwaweka watoto kwenye njia ya hatari. Wengi wao huishia kugonga ukuta ama kingo kali za fanicha ama kuanguka kwenye ngazi.

Hapo nyuma mwaka wa 2010, kamati ya U.S Consumer Product Safety walihimiza sehemu zingine za usalama ziongezwe kwenye hivi vifaa kama vile breki.  Ingawaje, hili lilipunguza ajali bado maelfu ya watoto waliishia kupelekwa hospitalini.

“Bado kuna watoto 2000 kila mwaka ambao hutibiwa kutokana na ajali za magari ya watoto ya kutembea, nyingi zikiwemo ajali kubwa katika idara za dharura,” daktari Gary Smith akasema, mwandishi mkuu wa utafiti Pediatrics.

“Kwa hivyo, tunaunga mkono msimamo wa American Academy of Pediatrics kuwa magari ya watoto ya kutembea hayafai kuuzwa  ama kutumika. Hakuna sababu yoyote ile kwa nini hizi bidhaa zinafaa kuwa zinauzwa. “

Vigari vya watoto vya kutembea huenda vikadhuru ukuaji wa watoto 

Wengine wanaotumia  ama kutetea magari haya wanaamini kuwa yanasaidia mtoto kukua hawsa kutembea.

Lakini kumlazimisha mtoto kutembea kabla ya wakati, inaweza kusababisha kizuizi kwa ukuaji kuliko manufaa.

Daktari wa watoto, David Gellar aelezea kuwa watoto wanaotumia vigari vya watoto vya kutembea, mara nyingi  hutembea mwezi mmoja baada ya wale hawakutumia.

Mtoto husoma kutembea wakati misuli yake, isawa na ina uratibu na ina nguvu vizuri. Pia kwa kuangalia na kuelewa jinsi miguu hutembea.

Anapokuwa kwenye kigari cha watoto cha kutembea, uwezo wa watoto kuona miguu imekingwa na kile kifaa.  Na hivyo basi kukua vizuri kwa uwezo wa mtoto wa kutembea kunazuiwa.

Kuongezea na uwezekano mkubwa wa ajali, unaelewa zaidi kwa nini madaktari wa watoto wapinga matumizi ya vifaa hivi.

 

vigari vya watoto

Mfunze mtoto wako kutembea bila ya kigari cha watoto cha kutembea

Hivi sasa ni wazi kuwa hakuna wakati mwafaka wa kutumia kigari cha mtoto cha kutembea kumfuza mtoto wako kutembea.

Hapa kunavyo vidokezo vya kuhimiza mtoto kutembea bila ya kifaa hiki:

  • Mwache akae bila ya kusaidiwa

Mwache mtoto wako akae kwenye kiti bila ya kujilaza ama kusaidiwa. Lakini hakikisha uko karibu ili mtoto awe salama. Miguu ya mtoto wako inafaa kufikia sakafu ili aweze kuegemea na kiuno na magoti yakiwa wima.

Anapoweza kukaa katika hii hali, muulize achukue kichezeo kwenye sakafu na kisha kukaa chini kwa kiti. Unaeza weka vichezeo mahali tofauti tofauti ili kuboresha misuli na uwezo wa kifikia vitu.

Anapofanya hivi, mtoto wako anasongesha miguu mbali ili kuwa thabiti. Kwa wakati huo, anatilia mkazo miguu, akiboresha misuli ya miguu, mabega na mgongo.

  • Mwonyeshe vitu vinavyomvutia

Kwa kufanya hivi, mdogo wako anasongeza kichwa na shingo ambazo hutilia nguvu misuli ya mgongo.  Tia akilini kuwa, mbali na misuli ya miguu, misuli ya mgongo ina jukumu la kimsingi kwa kuwasaidia watoto kutembea.

Jambo lingine ambalo wazazi wanaweza kufanya ili kunawirisha misuli ya mgongo ni kulaza watoto chali. Hivyo, watoto watajifunza kudhibiti misuli ikiwawezesha kutembea haraka.

vigari vya watoto

  • Wape vichezeo vya kusukuma ama kuvuta

Vichezeo vya kuvuta ama kusukuma ni zaidi ya vichezeo vya kawaida; husaidia pakubwa katika kumsaidia mtoto kutembea.  Kwa hivi vichezeo watoto husoma kusimama, kutembea na kujidhibiti.

Watoto watafurahia kuvitumia kwani huja na muziki na taa ambazo huburudisha sana.  Mpe angalau kichezeo kimoja ama viwili na utamwona mtoto wako akisimama bila usaidizi na kutembea.

  • Mwache atembee bila viatu

Soksi na viatu hutumika kumkinga mtoto kutokana na baridi na vyombo vinavyoweza kumkwaruza kwenye sakafu.  Lakini iwapo unataka mtoto wako kutembea kwa haraka ni vizuri kuacha miguu yake wazi.

Hii ni kwa sababu miguu ya mtoto wako itaweza kujishikilia kwenye sakafu vizuri kuliko anapovalia soksi na viatu.

Pia, mtoto wako anapovalia viatu, hakikisha unaangalia kama kiatu chake kinamuumiza. Iwapo utagundua ana hisi uchungu ni vizuri kuvibadilisha na vilivyo sawa ili mtoto aweze kuzingatia kutembea bila ya kuhisi uchungu.

  • Msaidie mtoto wako kutembea

Mtoto wako anapoanza kutembea hakikisha kuwa unajua jinsi ya kumsaidia.  Simama nyuma yake na umshike kwenye mikono yake ya juu. Msaidie kusimama kwa kuvuta mkono wake mmoja mbele.

Pindi mtoto wako atakapozungusha kiuno chake kutembea, miguu yake itafuatia yenyewe.  Mara yote zingatia utaratibu huu wakati mtoto wako anapojifunza kutembea mpaka atakapokuwa hahitaji usaidizi tena.

 

References: NPR, Pediatrics

Written by

Risper Nyakio