Barua Wazi Kwa Wanawake: Kwa Nini Vijana Walio Karibu Na Mama Zao Huwa Mabwana Bora

Barua Wazi Kwa Wanawake: Kwa Nini Vijana Walio Karibu Na Mama Zao Huwa Mabwana Bora

Ukweli fiche kuhusu wanaume wanao dekezwa na mama zao na iwapo ni vyema kufunga ndoa na wanaume wa aina hii.

Maarufu kama 'mama's boy', wanafahamika sana kama vijana walio na uhusiano wa karibu na mama zao. Nina uhusiano wa karibu sana na mamangu, mwanamme mmoja alisema. Na wakati wote amenifunza kuwaheshimu watu hasa wanawake maishani mwangu. Alinifunza umuhimu wa kukumbuka siku za kusherehekea kuzaliwa. Na jinsi kila siku ya kuzaliwa ninavyo paswa kuja na zawadi. Nilisoma umuhimu wa kadi na maua. Na umuhimu wa kupendeza wakati wote. Pia kutofanya zaidi ya niwezacho. Na kilicho muhimu zaidi, alinifunza kuwa na heshima, ukweli na mwaminifu wakati wote- vitu muhimu sana katika kila uhusiano. Kwa hivyo bila shaka sio wanaume wote walio karibu na mama zao walio dekezwa.

Barua Wazi Kwa Wanawake: Kwa Nini Vijana Walio Karibu Na Mama Zao Huwa Mabwana Bora

Vijana Walio Karibu Na Mama Zao

Utafiti tofauti ulio fanyika umedhihirisha kuwa vijana hawa wanakua na ndiyo waume bora zaidi, hata kama watu wengi. Utafiti nilio patana nao muda mfupi uliopita ulidhibitisha kuwa vijana wana uhusiano wa karibu na wenye nguvu na mama zao na huenda wakawa wana tangamana vyema, kufanya wake zao wawe na furaha na kushuhudia ndoa zenye mafanikio zaidi.

Wanawake wenzangu, msiwe na hofu ya kuingia katika ndoa na vijana walio karibu na mama zao. Hata kama najua kamusi inatueleza kama wavulana wanao dekezwa zaidi na mama zao. Lakini mwanamme kuwa karibu na mama yake ni jambo nzuri. Walakini mwanamme anaye tawaliwa na mama yake sio mfano wa kijana aliye karibu na mamake. Bila shaka kutakuwa na matatizo katika ndoa yenu, kwani wanawake wawili hawawezi ongoza nyumba. Mke wa mvulana huyu na mama mkwe wake wata korofishana. Na iwapo mwanamme lazima amjulishe mama kila jambo analo fanya, huo sio mwanamme, huyo ni mtoto.

vijana walio karibu na mama zao

Ni asili kwa hilo kutendeka kwa sababu unafikiria uelewano wa kwanza kuhusu wanawake na jinsi ya kuwa heshimu hutoka wapi? Kwa mama zetu bila shaka! Kwa hivyo unapaswa kuwa ukiimba nyimbo za shukrani iwapo mchumba wako anamheshimu mamake. Wamama husaidia kujenga jinsi vijana watakuwa wanapokuwa na mwanamke maishani mwao, bila shaka wana weledi katika hilo. Kwa nini unafikiria mimi huvalia badgi yangu ya 'mummy's boy'?

Cha zaidi ni kuwa wana uwezo wa kuwa na uhusiano wa karibu na kihisia, yote kwa sababu mama zao waliwasaidia kufanya hivyo. Hatuna uwoga wa kuonyeshana udhaifu wetu, na bila shaka tuta kulinda.

 

mummy's boy

Mimi husikia mara nyingi wanawake wakiongea kuhusu wanavyo tafuta wanaume watakao waheshimu, kuwa dhamini na kuwaelewa. Wanaume wanaokuwa na uhusiano na upande wao wa kike. Wanawake, mnatafuta vijana walio karibu na mama zao.

Abubakar Tafawa-Balewa ni mwanasheria na mshauri wa mitindo. Yeye ndiye mwanzilishaji na mchapishaji wa jarida la Mode Men Magazine - jarida linalo ongoza la mitindo Nigeria.

Soma pia: 10 Signs Your Mother-In-Law Is Jealous Of You And How To Deal With Her

Written by

Risper Nyakio