Mwongozo Wa Vinywaji Vyenye Afya Vya Watoto Kuzuia Uzito Mwingi Kwa Watoto

Mwongozo Wa Vinywaji Vyenye Afya Vya Watoto Kuzuia Uzito Mwingi Kwa Watoto

Wanasayansi wametoa mwongozo mpya wa vinywaji vya afya vya watoto. Baadhi ya vitu tunavyofikiria ni salama kwa watoto husababisha uzito mwingi wa mwili.

Na ongezeko la teknolojia huja ujumbe na maarifa mengi kila wakati. Kilicho onekana kuwa sawa jana huenda kikawa kibaya leo ama kilichokuwa kibaya kikawa kizuri. Unahitajika kuchukua ujumbe unavyokuja. Kikundi cha wataalum hivi majuzi kilitoa mwongozo wa vinywaji vya afya vya watoto.

Ushauri huu wa lishe utachukuliwa kwa makini kwa sababu ulitengenezwa na wataalum wanao ongoza katika nyanja hii. American Academy of Pediatrics, the Academy of Nutrition and Dietetics, the American Heart Association na the American Academy of Pediatric Dentistry walikuja pamoja na kutengeneza mwongozo huo. Utafiti ulihaziniwa na Shirika la Robert Wood Johnson.

Watoto wachanga wanapaswa kunywa nini?

healthy drinks for kids

Kulingana na kikundi hicho cha wataalum, watoto wanapaswa kupata maziwa ya mama ama formula. Lakini, katika miezi sita maji yanaweza ongezwa kwenye lishe yake. Pia, watoto wanao kunywa formula, inaweza badilishwa iwe maziwa ya ng'ombe wanapokuwa na miezi 12. Watoto wana hitajika kunywa maziwa na maji kwa miaka ya kwanza ya maisha yao.

Walakini, kinywaji chochote kilicho na sukari na kemikali za ladha hakipaswi kupatiwa kwa mtoto aliye na umri chini ya miaka mitano. Sio hata vinywaji vya nyumbani vyenye sukari, chokleti ama maziwa yenye ladha, kahawa ama formula zingine za watoto. Kwa wazazi wanao tafuta mbadala wa maziwa ya ng'ombe, wanaweza chagua maziwa ya soy. Vinywaji vyoyote vya mimea kama vile maziwa ya mchele ama oats havipaswi kutumika.

Hili huenda likashtua wazazi wanaopendelea kuwalisha watoto wao sharubati. Kikundi hicho cha wataalum pia kilisema kuwa watoto wanapaswa kunywa chini ya kikombe cha asilimia 100 cha sharubati kwa siku.

Kulingana na daktari Richard Besser, rais na kiongozi mkuu wa Shirika la Robert Wood Johnson, "Tuna ongea kuhusu kalori wazi kupitia kwa vinywaji vya nyumbani na nambari za kalori ambazo watu hupata kutoka kwa vinywaji vilivyo na sukari, hatuongei kuhusu soda peke yake. Sharubati pia ni chanzo cha kalori ambazo ni mbaya kwa lishe.

Vinywaji Vya Afya Vya Watoto Ni Gani? 

Mwongozo Wa Vinywaji Vyenye Afya Vya Watoto Kuzuia Uzito Mwingi Kwa Watoto

 Kikundi hicho cha wataalum kilishauri mwongozo kulingana na vikundi vya umri vya watoto ili watu waelewe vizuri.

  • Kutoka kuzaliwa hadi miezi sita

Kikundi hiki cha umri kinapaswa kunywa maziwa ya mama ama formula ya watoto wachanga. Haupaswi kuwapatia sharubati, maziwa, maziwa yenye ladha ama formula za kuwaanzishia watoto chakula, maziwa ya kukua ama formula ya kufuatilia. Pia, usiwapatia maziwa isiyo ya ng'ombe ama maziwa kutokana na mimea, kahawa, soda ama vinywaji vingine vya sukari.

  • Miezi sita hadi kumi na miwili

Kikundi cha umri hiki kinapaswa kunywa maziwa ya mama na formula. Wanaweza anza maji kidogo wanapo anza kula vyakula vigumu. Epuka sharubati ama maziwa yenye ladha.

  • Miezi ishirini hadi ishirini na minne

Kwa kikundi hiki, wanapaswa kunywa kikombe kimoja hadi vinne vya maji kila siku. Pia, unaweza anza kuwapa maziwa iliyo pasteurized. Kwa siku, hawapaswi kuzidisha ounsi asilimia 100 za sharubati ya matunda.

  • Miaka miwili hadi mitatu

Kikundi hiki kinapaswa kunywa kikombe kimoja hadi vinne vya maji kila siku. Kisha ubadilishe kwa maziwa yasiyo na ufuta. Usiwape zaidi ya ounsi nne za asilimia 100 za sharubati ya matunda. Hawapaswi kunywa kinywaji kingene chochote.

  • Miaka mitatu hadi mitano

Vikombe 1.5 hadi vitano vya maji kila siku vina shauriwa kwa kikundi hiki na visivyo zidisha ounsi sita zenye asilimia 100 ya sharubati ya matunda. Usiwapatia kinywaji kingine chochote.

Walakini, ikiwa mtoto wako amezoea sharubati huenda ikachukua muda mdogo kumkomesha kinywaji hicho. Cha zaidi ni kuwa, huenda ukawa umegundua kuwa na vikundi hivi vyote, hauwezi fanya makosa yoyote na kuwapa maji tu.

Soma pia: Vyakula Vyenye Virutubisho Vya Kusaidia Watoto Kuongeza Uzito

Chanzo: HealthyDrinkHealthyKids

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio