Vinywaji Bora Vya Detox Vya Kupunguza Uzito Wa Mwili!

Vinywaji Bora Vya Detox Vya Kupunguza Uzito Wa Mwili!

Vinywaji vya detox vya kupunguza uzito vinakusaidia kutimiza lengo lako la kiafya. Lakini ni vyema kuzungumza na daktari wako kabla kuanza utaratibu wowote ule wa kupunguza uzani.

Vinywaji vya detox ni njia maarufu ya kupunguza uzito. Kuna aina nyingi za chai zinazo kuahidi kutoa sumu mwilini na kukata uzito kwa kipindi kifupi cha wakati. Lakini vinywaji vya detox asili vya kinyumbani ni bora kwa afya yako. Pia, unaweza kuzitumia kwa kipindi kirefu.

Kisicho na afya kuhusu baadhi ya chai za kununuliwa kwenye maduka ili kupunguza uzito wa mwili ni kuwa unapunguza uzito kwa kasi sana na kwa kiwango kisicho na afya. Mara nyingi, una shauriwa kujitenga na chakula na vinywaji na unywe chai hizi peke yake ili kupata matokeo bora.

Kwa hivyo badala ya kuchukua detox za aina hizi, zilizo tengenezewa nyumbani ni bora zaidi. Pia, unapo husisha na lishe yenye afya, utaona matokeo kwa kasi.

Vinywaji vya detox ni nini hasa?

Vinywaji hivi vinatengenezwa kutokana na vitu asili vinavyo saidia kutoa sumu mwilini mwako. Unapokula chakula, kinabadilishwa kuwa nishati. Halafu kuna cha zaidi ambacho mwili wako hauhitaji, na hii huenda ikamaanisha uzito zaidi. Detox ni kutoa chakula zaidi ambacho maini hayawezi kutoa.

Aina tano ya vinywaji vya detox vya kupunguza uzito

Maji ya ndimu, cucumber na mint

Tunda la cucumber lina asilimia 95 ya maji. Inakusaidia kuhakikisha una maji tosha hasa kunapo kuwa na joto. Wakati ambapo ndimu inakusaidia na vitamini C kila siku. Pamoja, cucumber na ndimu ni detox asili ambazo zinaweza toa sumu mwilini mwako kuboresha uchakati wa chakula.

Ginseng

Ginseng, vinywaji vya detox vya kupunguza uzito

Ili kupunguza uzito, unaweza toa maji yaliyoko kwenye ginseng na uyanywe kila siku. Chemsha angalau vikombe viwili vya maji kisha yapoe. Chukua kiwango kidogo cha ginseng na uongeze kwenye maji. Yape dakika chache kisha ukamue maji yawe tayari kunywiwa. Hakikisha una koroga vizuri kabla ya kunywa.

Lakini kama una poda ya ginseng, tumia angalau gramu mbili mara mbili kwa siku, ziwe 10 kwa siku moja. Lakini baada ya wiki mbili, unapaswa kupunguza hadi ziwe gramu mbili.

Hibiscus

Hibiscus flower zobo

Ili kupunguza uzito, kunywa angalau vikombe viwili vya hibiscus kila siku. Unaweza tayarisha mwenyewe badala ya kununua mitaani. Chemsha matawi ya hibiscus kwa dakika 15 kisha uyape muda yapoe. Kamua maji kwenye glasi na uyanywe. Unaweza ongeza ladha na nanasi ama tunda lingine.

Vinywaji vya detox vya kupunguza uzito vinakusaidia kutimiza lengo lako la kiafya. Lakini ni vyema kuzungumza na daktari wako kabla kuanza utaratibu wowote ule wa kupunguza uzani.

Soma Pia:Lishe Na Mazoezi Haya Yatakusaidia Kupunguza Uzito Wa Mwili Kwa Kasi

Written by

Risper Nyakio