Vipimo vya nyumbani vya kupima mimba vimekuwa vikitumika kwa muda mrefu. Hata ingawa usahihi wa baadhi ya vipimo hivi hauja egemezwa na Sayansi, vina aminika kuwa na usahihi. Tazama baadhi ya vipimo asili vya mimba ambavyo unaweza kutumia kupima mimba.
Mbinu Tofauti Za Kupima Mimba Nyumbani
- Kupima mimba kutumia chumvi

Kipimo hiki ni maarufu kwa watu wanao taka kufanyia kipimo cha mimba nyumbani. Chumvi ni kiungo cha jikoni kilicho maarufu. Kwa hivyo unapo taka kugundua ikiwa una mimba bila kuvuta uangalifu wa watu wengine, kipimo hiki kitakufaa. Kwa kutumia chupa safi na iliyo wazi, ongeza vijiko viwili vya chumvi. Kisha uongeze mkojo kwenye chupa hiyo. Inapo badilika na kuwa na chembe chembe nyeupe, hiyo ni ishara kuwa kipimo hicho ni chanya. Kusipo kuwa na mabadiliko yoyote, kuna maana kuwa hauna mimba.
- Kipimo cha mimba cha baking soda
Chukua vijiko viwili vya baking soda, weka kwa kontena safi na iliyo wazi. Ongeza kiwango sawa cha mkojo. Kuwa makini kuona mabadiliko yatakayo tendeka. Ikiwa hakuna mabadiliko utakayo yaona, hauna mimba. Ukigundua kuwa kuna mapovu yanayo toka, bila shaka una mimba, hongera!
- Kupima mimba kutumia sabuni
Hata ingawa kipimo hiki haki tumiki sana, kilikuwa maarufu katika siku za kale. Chukua sabuni yoyote ile. Kisha umwage kiwango kidogo cha mkojo. Una shauriwa kutumia mkojo wa kwanza wa siku. Kabla ya kuchukua kiamsha kinywa ama kwenda msalani. Mapovu yakitokea baada ya kumwaga mkojo kwenye sabuni hiyo, una mimba.
- Kipimo cha mimba cha sukari

Mbinu hii ya kupima mimba ilikuwa maarufu kabla ya kuibuliwa kwa vipima mimba vya kisasa. Chukua kijiko kimoja cha sukari uongeze kwenye bakuli. Hakikisha kuwa bakuli hiyo ni safi na wazi, ili uweze kutazama kinacho endelea ndani. Ongeza kiasi kidogo cha mkojo kwenye bakuli hiyo. Tazama kitakacho fanyika. Ukiona kuwa sukari imeanza kuwa chembe chembe nyeupe, bila shaka unatarajia mtoto. Lakini ikiwa bakuli ile itabaki bila mabadiliko, fahamu kuwa hauna mimba.
- Kupima mimba kutumia divai

Kwa chupa ama kontena wazi, weka kiwango cha divai. Kisha uongeze kiwango sawa cha mkojo. Changanya vyema. Wacha chupa hiyo itulie kwa angalau dakika 10. Angalia kuona ama kuna mabadiliko. Rangi ya divai ile inapo badilika, hiyo ni ishara kuwa una mimba.
Hivi ndivyo baadhi ya vipimo asili vya mimba vinavyo fahamika zaidi. Je, unafahamu vipimo vingine asili vilivyo tumika? Tujulishe kwa kuwacha ujumbe mdogo!
Soma Pia: Jinsi Ya Kupima Mimba Kwa Kutumia Kitunguu