Vipimo Kabla Ya Kupata Mimba: Je, Mama Anapaswa Kufanyiwa Vipimo Gani?

Vipimo Kabla Ya Kupata Mimba: Je, Mama Anapaswa Kufanyiwa Vipimo Gani?

Kufanya vipimo kabla ya kupata mimba ni muhimu sana kwa mama kwani anapata kujua iwapo afya yake iko sawa kuegemeza ukuaji wa mtoto tumboni.

Ni vyema wakati wote kwa mama kufanya vipimo kabla ya kupata mimba. Kwa visa ambavyo mimba ilikuwa imepangiwa. Kufanya hivi kunamwezesha kuwa na msaada kutoka kwa mtaalum na anafahamu anavyo paswa kufanya kuongeza nafasi zake za kuwa na safari ya ujauzito isiyo na matatizo sana.

Katika vipimo hivi, daktari atakuuliza kuhusu vitu hivi:

maandalizi ya kupata mimba

 • Iwapo katika nyanja yako ya kazi unagusana na vitu hatari
 • Hali yako ya afya
 • Afya ya familia yenu na kama kuna magonjwa ya kurithi
 • Iwapo una fanya mazoezi
 • Ikiwa una tatizika kula

Katika swali la afya yako, atauliza mambo yafuatayo, ikiwa una moja kati ya magonjwa haya:

 • Shinikizo la damu
 • Kisukari
 • Kifafa
 • Matatizo ya tezi
 • Maradhi ya kiakili
 • Ugonjwa wa moyo

Ni vyema kumjuza daktari wako mambo yafuatayo

 • Iwapo kwa familia yenu kuna historia ya magonjwa ya kurithi kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Hasa kuhusu sickle cell ama selimundu, ama ugonjwa wa kukosa damu tosha mwilini ama anaemia
 • Kama kuna mbinu za kupanga uzazi unazo zitumia. Na muda ulio anza kuzitumia na kama zimekuwa na athari hasi kwa mwili wako
 • Kama hapo awali umeshuhudia kisa cha kuharibika kwa mimba, mimba ya ectopic ama kutoa mimba

Mama anastahili kufanya vipimo hivi vya kiafya: Vipimo kabla ya kupata mimba

vipimo kabla ya kupata mimba

Ikiwa mama amejihusisha katika ngono bila kinga, anapaswa kufanyiwa vipimo hivi kudhibitisha hali yake ya kiafya:

 • Kaswende
 • Klamidia
 • Homo ya maini
 • Virusi vya ukimwi

Utafanyiwa kipimo cha damu na cha uzazi ili kubaini kama una matatizo usiyo yafahamu.

Chanjo kabla ya kupata mimba

Ni muhimu kwa mama kupata chanjo kabla ya kupata mimba kwani maambukizi ya aina yoyote yana mhatarisha kupoteza mimba. Baadhi ya chanjo ambazo mama hupata ni dhidi ya virusi vya rubella, mwezi  mmoja kabla ya kujaribu kupata mtoto.

Daktari wako atakushauri kuwa makini na lishe yako, kuanza kufanya mazoezi na pia kuanza kutumia tembe za kuongeza virutubisho vya foliki mwilini mwako.

Umuhimu wa vipimo hivi ni kumjuza mkunga wako iwapo utahitaji huduma zaidi kutoka kwa wataalum kutoka nyanja mbali mbali za kiafya. Ili kuhakikisha kuwa unajifungua salama.

Soma Pia: Kupata Mimba Ukiwa Na Uzito Mwingi Kuna Athari Zipi?

Written by

Risper Nyakio