Vipimo Asili Vya Mimba Vya Kubaini Kuwepo Kwa Mimba

Vipimo Asili Vya Mimba Vya Kubaini Kuwepo Kwa Mimba

Kuna aina tofauti ya vipimo vya mimba ambavyo mwanamke anaweza kutumia. Ila kipimo hiki cha kutumia chumvi ni maarufu sana na ni rahisi kufanya

Kuna aina tofauti ya vipimo vya mimba ambavyo mama anaweza kutumia kung'amua ikiwa ana tarajia kumpakata mtoto ama bado. Kuna vipimo asili na vipimo vya kisasa.

Makala haya yana angazia aina ya vipimo asili vya ujauzito

vipimo vya mimba

Kuna baadhi ya wanawake ambao kwa sababu tofauti, hawapendi kununua vipima mimba. Vinavyo patikana kwenye zahanati ama maduka ya madawa. Ama huenda mama akawa hana wakati tosha wa kutoka kutafuta kifaa hiki. Kwa hivyo anafanya uamuzi wa kutumia bidhaa alizo nazo kwenye nyumba kubaini hali yake.

Vipimo hivi ndivyo vilivyo tumika siku za kale kabla ya kuvumbuliwa kwa vipima mimba. Ufanisi wa mbinu hizi unategemea wakati ambapo mama anafanya kipimo hiki na uwezo wake wa kubaini matokeo anayo yapata.

Wakati wote, mama anahimizwa kufanya kipimo cha mimba siku 14 baada ya kujihusisha katika kitendo cha ndoa. Kwa nini? Kwa sababu inachukua siku kati ya 12-14 kwa yai lililo rutubishwa kujipandikiza kwenye kuta za uterasi. Kisha mwili kuanza kutoa homoni ya hCG inayo tolewa na kiinitete baada ya seli za mwili kukitunga. Uwepo na idadi ya homoni hii ndiyo inayo onyesha kuwepo ama kuto kuwepo kwa ujauzito.

Kipimo asili cha mimba kutumia chumvi

vipimo vya mimba

Chumvi ni kiungo kinacho patikana kwa urahisi na ambacho ni muhimu sana jikoni. Kwa hivyo nafasi kubwa ni kuwa kila mtu ana kiungo hiki jikoni mwake. Rahisi sivyo?

Kipimo hiki ni rahisi sana kufanya.

Mahitaji:

Unahitaji kuwa na vitu hivi ili ufanye kipimo hiki cha mimba kwa kutumia chumvi.

  • Kikombe ama chupa nyepesi
  • Kiasi kidogo cha chumvi
  • Mkojo wa kwanza wa siku

Maagizo 

  1. Weka mkojo wa kwanza wa siku kwenye chupa
  2. Kwa kutumia kijiko, ongeza nusu ya kijiko cha chumvi kwenye chupa yenye mkojo
  3. Kisha uchanganye
  4. Ngoja kwa dakika 3 hadi 5
  5. Kisha uangalie mabadiliko yatakayo tokea

Kufahamu matokeo

Ukigundua kuwa mchanganyiko kwenye chupa umeanza kubadili rangi na kuwa rangi ya maziwa, hii ni ishara kuwa una mimba.

Iwapo mkojo utabaki rangi yake asili, huku kuna ashiria kuwa hauna ujauzito.

Kuna aina tofauti ya vipimo vya mimba ambavyo mwanamke anaweza kutumia. Ila kipimo hiki ni maarufu sana na ni rahisi kufanya. Usiwe na shaka tena. Kama uko nyumbani na ungependa kujua hali yako ya mimba, tumia maagizo tuliyo angazia kujua hali yako ilivyo.

Soma PiaVipimo 6 Maarufu Zaidi Vya Kupima Mimba Vya Kinyumbani

Written by

Risper Nyakio