Utafiti Unadhihirisha Muda Unaofaa Kati ya Vipindi Vya Uja uzito

Utafiti Unadhihirisha Muda Unaofaa Kati ya Vipindi Vya Uja uzito

The study found that it doesn't matter how old you are - getting pregnant too quickly after delivery brings about a lot of risks to both the mum and the unborn baby.

Je, una hamu ya kupata mtoto mwingine? Je, utafiti unadhirisha muda unaofaa kati ya vipindi vya uja uzito? Sio jambo la busara kukimbilia kupata mimba tena, kwani huenda ukapata matatizo ya kiafya. Utafiti wa kisayansi na watafiti wana dhihirisha muda unaofaa kati ya uja uzito ulio bora zaidi kwa afya.

Utafiti unaonyesha muda unaofaa kuzingatiwa kati ya vipindi vya uja uzito.

Shirika kuu la Afya Duniani (WHO) lapendekeza wamama kujipa wasaa kati ya uja uzito kutoka miezi 18-24. Walakini, katika utafiti ulio fanywa hivi karibuni, wanasayansi waligundua kuwa jambo hili si la muhimu.

Walichopata kinaonyesha kuwa wakati mdogo zaidi unaofaa kati ya uja uzito ni miezi kumi na miwili (12). Kungoja mwaka mmoja kabla ya kupata mtoto mwingine, husaidia kuhakikisha kuwa mama na mwanawe hawako kwa hatari yoyote ila kuyapata matatizo ya kiafya.

Kupata mimba tena punde baada ya kujifungua (kabla ya miezi 12) huwa na hatari nyingi. Kama vile kujifungua kabla ya wakati kufika, kujifungua mtoto aliye na uzito mdogo, ama kifo cha mama.

Daktari Wendy Norman ni mwandishi mkuu wa utafiti huu. Ana upata utafiti huu kuwa “habari za kuhimiza” kwa wanawake walio na miaka zaidi ya 35 wanao tamani kupata watoto zaidi.

Kwa mara ya kwanza, wamama walio na umri zaidi “wana ushahidi wa kuwaelekeza kuhusu muda kati ya watoto wao” yuasema daktari Norman. “Kutimiza kipindi baina ya uja uzito mmoja na mwingine, lafaa kuwa jambo linalo weza kutendeka kwa wanawake wengi na ni bayana kuwa lina umuhimu wa kupunguza hatari za kiafya.

vipindi kati ya uja uzito

Nini haswa kilicho patikana katika utafiti huu?

Utafiti huu ulitafiti wanawake 150,000 ambao walikuwa wamejifungua nchini Canada. Uliongozwa na Chuo Kikuu cha British Columbia (UBC) na Harvard’s TH Chan School of Public Health.

Watafiti walichapisha matokeo katika jarida la JAMA Internal Medicine.

Huu ni muhtasari mfupi wa waliyo pata, wamama walipo pata mimba kabla ya miezi 12 kupita baada ya kupata mtoto wa kwanza.

Umri sio wa maana. Kuwa mja mzito tena kabla ya kipindi kinacho hitajika (mwaka mmoja) kupita, kilihusishwa na kuwa na hatari kwa mwanamke wa umri wowote.

Utafiti Unadhihirisha Muda Unaofaa Kati ya Vipindi Vya Uja uzito

Ila, hatari kwa mama zina tofautiana kulingana na umri.

Wamama zaidi ya miaka 35 wana hatari za kupata matatizo ya kiafya wanapo pata watoto kwa kukaribiana kwa sana. Walakini, hatari kwa watoto ambao hawajazaliwa ilitendeka kwa wanawake wote. Ya juu zaidi ikiwa kati ya wenye umri wa miaka 20-34.

Wamama wenye umri wa miaka zaidi 35 walio pata mimba miezi sita baada ya kujifungua, walikua na hatari ya asilimia 1.2 ya kupata majeraha ama kifo. Kuto pata mimba tena kwa muda kabla ya miezi nane kupita. kuli punguza hatari hii hadi asilimia 0.5.

Kwa tofauti, wanawake wachanga waliopata mimba miezi sita baada ya kujifungua, walikua na hatari ya asilimia 8.5 ya kifo cha uzazi ama majeraha. Hatari hii hupungua hadi asilimia 3.7 wanapo pata mimba baada ya miezi 18.

“Mwishowe, ni chaguo la mwanamke”

Laura Schummers, mwandishi mkuu wa somo hilo alisema kuwa utafiti wao, uli ya angazia “hatari zilizo ongezeka kwa mama na mtoto” wamama wanapo kuwa waja wazito punde baada ya kujifungua. Hata kwa wamama wenye umri zaidi ya 35.

Schummer anahimiza kuwa matokeo haya ni muhimu kwa wamama wenye umri zaidi, kwani “kwa mara nyingi, wanapata watoto kwa kukaribiana na mara nyingi sio kwa kusudi”.

Mandy Forrester, mmoja kati ya wakunga wa chuo kikuu cha Royal, alisema kuwa utafiti huu uliunga mkono matokeo ya hapo awali ya kipindi baina ya kupata mimba. Ila anahimiza kuwa:

Mwishowe, ni chaguo la mwanamke, katika umri wowote ule, kuchagua muda kati ya vipindi vya uja uzito wake. Cha muhimu ni kuwa watakua na ushahidi kuhusu kipindi kati ya kupata watoto. Pia, watafanya uamuzi kufuatia habari walizo nazo.

Vipindi kati ya uja uzito: Mbinu zingine za kupunguza hatari ya uja uzito

vipindi kati ya uja uzito

kumtembelea daktari wako ni miongoni mwa utunzaji kabla ya kujifungua.

Vipindi kati ya uja uzito: utunzaji kabla ya kujifungua

 • Kula lishe bora na uyanywe maji ya kutosha. Virutubisho vinavyo faa mwilini, protini, wanga na fibre za kutosha. Chagua wanga zilizo nzima badala ya zilizo safishwa kama vile mchele mweupe. Pia asidi ya folici ni muhimu na mboga zenye matawi. Hakikisha una iron na calcium za kutosha.
 • Epukana na sigara, pombe na madawa ya kulevya.
 • Punguza unywaji wako wa kafeini kama vila chai ama cola, kwani hufanya vigumu kupata mimba.
 • Isipokuwa chai ya kijano.
 • Usijaribu lishe mpya kwani huenda zika athiri ovulation yako na uzazi wako.
 • Hakikisha umepata utunzi kabla ya kujifungua. Kuna madaktari watakao weza kupima hali ya afya yako iwapo kuna matatizo yoyote na kukupa ushauri unaofaa.

Unapo kua mja mzito

 • Hakikisha lishe yako ina vyakula bora kama vile mchicha (folate), matunda (vitamini na fibre), maziwa (calcium) ili kuweka mwili wako katika hali bora zaidi.
 • Hakikisha una tembea kidogo ili mtiririko wa damu uwe mzuri. Pia hewa safi itasaidia kuboresha mhemko wako. Tembea pwani ama kwenye mbuga ili kupata utulivu na akili shwari.
 • Epukana na kazi za kinyumbani zinazo husisha:
 • Kemikali zilizo na nguvu zaidi
 • Kuosha madirisha, dari na pepeo.
 • Kuosha vyombo
 • Kufagia na kuosha sakafu
 • Kubeba vitu mzito
 • Kuosha wanyama wa nyumbani
 • Epukana na vyakula kama vile:
 • Nyama mbichi ama ambayo haijapikwa vizuri (ya ng’ombe, samaki ama ndege)
 • Mayai mbichi na bidhaa zake mayonnaise na hollandaise sauce
 • Samaki wakubwa walio na mercury nyingi kama vile papa, marlin, tuna na mackerel.
 • Matunda na mboga zisizo safi ambazo hazija oshwa vizuri ama zilizo chafu.

References: BBC, JAMA

Written by

Risper Nyakio