Taarifa Kuhusu Virusi Vya Corona

Taarifa Kuhusu Virusi Vya Corona

Virusi vya corona vimeendelea kusambaa na ku athiri maisha ya watu wengi

Virusi vya homa ya corona vili ripotiwa kwa mara ya kwanza Wuhan huko Uchina. Kisa cha kwanza kilikuwa mwezi wa Disemba mwaka wa 2019. Kwa wakati huo hakuna aliye dhani kuwa maradhi haya yangefika nchi za Afrika. Ila kufikia kwa mwezi wa pili, kisa cha kwanza cha virusi vya corona kili ripotiwa Kenya na katika mwezi huo, maradhi haya yali ripotiwa kuwa janga duniani kote.

virusi vya corona

Athari za virusi vya corona

Kufuatia uwezo wa kuambukizwa kwa maradhi haya kwa urahisi na kwa kiwango kikubwa kwa watu, watu wengi wali shauriwa kukaa nyumbani. Safari za ndege zilipigwa marufuku na kusababisha maafa makubwa katika kazi za watu. Idadi kubwa ya watu walio kuwa wakifanya kazi katika sekta ya utalii walishuhudia kupunguka kwa pesa walizokuwa wakipata. Huku wafanya kazi katika hoteli tofauti wakalazimika kukaa nyumbani kufuatia kupunguka kwa kazi. Sekta ya usafiri wa barabarani pia ulishuhudia kupunguka kwa mapato yao kwani watu wengi waliamua kuenda sehemu za mashinani. Walio baki mijini hawakuruhusiwa kutembea mara kwa mara ama hata kwenda kazini ili kupunguza nafasi za kupatana na mtu aliye na virusi hivi na kuambukizwa. Kufuatia kupunguka kwa watu waliotoka nje ya nyumba zao na walio fika mijini, biashara nyingi zilifunga kazi na watu wengi kupoteza namna ya kupata pesa.

virusi vya corona

Maendelezo ya athari za homa ya corona

Idadi kubwa ya watu ulimwenguni wameambukizwa virusi vya homa ya corona. Iwapo watu wengi wame weza kupona, baadhi yao waliya poteza maisha yao. Kwa sasa, watu 92 wame yapoteza maisha yao nchini Kenya. Na uchumi wa nchi kuendelea kudidimia kila siku. Hali ime endelea kudidimia kila siku na imekua jambo la lazima kuvalia barakoa unapokuwa kwa umma. Sheria zime pitishwa na yeyote anaye onekana akitembea kwa umma bila kuvalia barakoa atishikwa kwani ana ya hatarisha maisha yake pamoja na ya watu anao ishi nao.

Kila mtu anashauriwa kufuata kwa makini maagizo kutoka kwa serikali na wizara ya afya kuhusu usalama wanapokuwa miongoni mwa watu ama hata kutoka manyumbani mwao.

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio