Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Vyakula Muhimu Katika Lishe Ya Mama Mjamzito

3 min read
Vyakula Muhimu Katika Lishe Ya Mama MjamzitoVyakula Muhimu Katika Lishe Ya Mama Mjamzito

Lishe katika mimba ni muhimu katika ukuaji wa mama na mtoto. Virutibisho katika ujauzito ambavyo mama ana stahili kuchukua ni kama vile protini. Soma zaidi.

Chakula ambacho mama mjamzito anakula ndicho kinacho mrutubisha mtoto anaye kua kwenye uterasi yake. Hii ndiyo sababu kwa nini mama ana shauriwa kula lishe yenye afya. Virutubisho katika ujauzito vina saidia pakubwa katika ukuaji wa mtoto tumboni na hata anapo zaliwa. Afya ya mtoto miaka baada ya kuzaliwa huchangiwa pakuu na lishe ya mama anapokuwa na ujauzito. Ikiwa ana tatizika na lishe katika kipindi hiki, ni vyema kuchukua ushauri wa daktari wake ama mtaalum wa lishe.

Epuka kutumia dawa ulizo nunua kwenye duka la madawa bila kushauriwa na daktari. Kuna baadhi ya dawa ambazo zina athari hasi kwa afya ya mama na ujauzito. Unapaswa kuhakikisha kuwa una yasalamisha maisha yako na ya mwanao vyote uwezavyo.

Virutubisho muhimu katika ujauzito

virutubisho katika ujauzito

  • Kalisi

Madini ya aina hii ni muhimu katika kuimarisha ukuaji wa meno na mifupa ya mtoto. Mwanamke ana stahili kuhakikisha kuwa anachukua viwango tosha vya kalisi kutosheleza mahitaji ya mwili wake na wa mtoto. La sivyo, madini yaliyo kwenye hifadhi za mwili za mama hutumika kutosheleza mahitaji ya mtoto.

Kalisi inapatikana katika vyakula kama vile maziwa, bidhaa za maziwa kama vile maziwa ya bururu, mboga za kijani na salmon.

  • Folic acid

Asidi hii ni muhimu sana katika ukuaji wa mtoto. Inasaidia kuepusha kupata ulemavu wa kuzaliwa kwenye akili ya mtoto, uti wa mgongo, kwenye neural tubes. Asidi hii inapatikana kwenye vyakula vilivyo na vitamini B. Ni vigumu kwa mwanamke kupata viwango tosha vya folic acid kutoka kwa chakula. Kwa sababu hii, wanawake wanashauriwa kuchukua vidonge vya kuwasaidia kufikisha viwango vinavyo hitajika vya miligramu 400 kwa siku.

Vyanzo vya folic acid vya chakula ni kama vile: nafaka, mkate, maharagwe, matunda na mboga za kijani.

virutubisho katika ujauzito

  • Protini

Protini ni muhimu sana katika ujauzito. Hata kama wanawake wengi hawatatiziki kufika viwango tosha vya kirutubisho hiki. Inasaidia na ukuaji wa mwili. Wataalum wana washauri wanawake wenye mimba kuhakikisha kuwa wanachukua miligramu 60 kwa siku. Zinasaidia na ukuaji wa viungo muhimu mwilini mwa mtoto kama vile moyo na ubongo.

Protini hupatikana kwenye vyakula kama vile nyama, samaki, mayai, maharagwe na kadhalika.

  • Iron

Madini ya aina hii ya chuma husaidia katika kutengeneza damu zaidi mwilini na kuzungusha hewa kwenye mwili hadi kwa mtoto. Mwanamke mjamzito ana stahili kuchukua miligramu 27 za chuma kwa siku. Kukosa kuchukua viwango tosha vya iron huenda vikamfanya mwanamke kuwa na hali ya anaemia ambapo hana damu tosha mwilini.

Hali inayo hatarisha maisha ya fetusi na kumweka katika hatari ya kupata maambukizi. Vyakula kama nyama laini, samaki, maharagwe yaliyo kaushwa na ndege wa kinyumbani huwa na wingi wa iron.

Soma Pia:Mabadiliko 5 Ya Kushangaza Ambayo Wanawake Wajawazito Hukumbana Nayo Katika Mimba

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Pregnancy
  • /
  • Vyakula Muhimu Katika Lishe Ya Mama Mjamzito
Share:
  • Makosa Ambayo Wanawake Wajawazito Hufanya

    Makosa Ambayo Wanawake Wajawazito Hufanya

  • Vidokezo vya Ujauzito Wenye Afya kwa Mama Mjamzito

    Vidokezo vya Ujauzito Wenye Afya kwa Mama Mjamzito

  • Chakula Bora cha Kujifungua Mtoto Mrembo

    Chakula Bora cha Kujifungua Mtoto Mrembo

  • Makosa Ambayo Wanawake Wajawazito Hufanya

    Makosa Ambayo Wanawake Wajawazito Hufanya

  • Vidokezo vya Ujauzito Wenye Afya kwa Mama Mjamzito

    Vidokezo vya Ujauzito Wenye Afya kwa Mama Mjamzito

  • Chakula Bora cha Kujifungua Mtoto Mrembo

    Chakula Bora cha Kujifungua Mtoto Mrembo

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it