Kupata virutubisho muhimu kunamsaidia mama kudumisha afya yake baada ya kujifungua na kuhimiza mtoto kukua ipasavyo. Kumbuka kuwa mtoto anategemea virutubisho ambavyo mama anapata kupitia kwa maziwa ya mama. Kwa hivyo ni vyema kwa mama kuhakikisha kuwa ana kula chakula chenye afya na tosha kustahimili afya yake na ya mtoto anaye mtegemea. Unafahamu virutubisho muhimu kwa mama anaye nyonyesha? Soma zaidi.
Virutubisho muhimu kwa mama anaye nyonyesha

Kalisi
Inasaidia katika kuongeza nguvu kwenye meno na mifupa. Na ina jukumu kubwa katika kuwa na mfumo mzuri wa kuzungusha damu, neva na misuli. Kalisi inapatikana kwa wingi kutoka kwa bidhaa za maziwa, sharubati ya machungwa na mchicha. Mwanamke anaye nyonyesha anapaswa kupata miligramu 1,000.
Fiber
Fiber inasaidia kupunguza kukosa maji tosha kunako andamana na kujifungua mara nyingi. Zinapatikana kwenye nafaka nzima kama vile mkate wa hudhurungi, nafaka na mchele wa hudhurungi. Matunda, mimea ya kundi la protini na mboga.
Folic acid
Ina saidia na ukuaji wenye afya wa akili ya mtoto na uti wake wa mgongo. Pia inatumika kutengeneza seli za damu mwilini. Mwanamke anahimizwa kuchukua tembe za folic acid mwezi mmoja kabla ya kupata mimba na kuendeleza baada ya kushika mimba. Ni muhimu katika kumwepusha mtoto kutokana na matatizo ya kuzaliwa ya uti wa mgongo ama ubongo.
Inapatikana kwenye nafaka, mboga za kijani, matunda, njugu na maharagwe. Pia mama anaweza kutumia tembe zake ili kufikisha kiwango kinacho stahili cha kila siku hasa katika mimba.

Iodine
Inasaidia thyroid gland mwilini kutengeneza homoni zinazo saidia na ukuaji wa viungo tofauti kama ubongo. Mwanamke asipo pata iodine tosha, mtoto ako katika hatari ya kuwa na matatizo katika ukuaji wake wa kiakili na pia thyroid yake kuwa na matatizo.
Inapatikana kwenye tembe ambazo daktari anamshauri mama kuchukua. Kiwango cha kila siku cha iodine ni microgramu 150.
Wanga
Wanga ni muhimu katika kuupa mwili nishati wa kuendeleza ukuaji na maendeleo, ya mama na mtoto. Mama anaye nyonyesha anastahili kula wanga, nafaka nzima, matunda na mboga za kijani ili apate wanga tosha.
Soma Pia: Kunyonyesha Kuna Faida Zipi Kwa Mama?