Visa Vya Homa Ya Corona Afrika Mashiriki Vyaendelea Kuongezeka!

Visa Vya Homa Ya Corona Afrika Mashiriki Vyaendelea Kuongezeka!

Mtoto wa miezi minane ni miongoni mwa visa vitano vipya vya COVID-19 nchini Uganda vilivyo ripotiwa siku ya juma tano. Nambari ya watu wote walio na virusi hivi nchini Uganda kwa sasa vimefikia visa 14. Inasemekana kuwa babake mtoto huyu alikuwa ametoka ziara yake nchi ya Kenya wiki iliyopita. Je, visa vya homa ya corona Afrika Mashariki vimepungua ama kuongezeka?

Jinsi hali ya homa ya corona ilivyo katika mataifa tofauti Afrika Mashariki.

homa ya corona afrika mashariki

Nchi ya Uganda

Mkurugenzi wa Huduma za kijumla za Afya daktari Henry Mwebesa alielez kuwa miongoni mwa visa hivi vipya ni watu wawili wa utaifa wa Uchina walipotea kutoka mahali walipokuwa wa karantainiwa. Walipatikana huku wamejificha sehemu za nchi ya Congo na Sudan ya kusini. Ambapo walishtakiwa kwa makosa ya kutahadharisha maisha ya wengine.

Wengine walikuwa mvyele wa miaka 63 aliye fika Uganda kutoka Ujerumani. Kufuatia na kuibuka kwa visa hivi, serikali ya Uganda ilichukua hatua za kidharura kuhakikisha kuwa wana wana kabiliana na tatizo la kusambaa kwa maradhi haya. Na kuya thibiti kabla yasambae sehemu tofauti chini. Uganda ilikuwa miongoni mwa nchi ya kwanza kuthibiti ziara za wananchi wake na masafa ya ndege.

Waziri wa Afya wa nchi ya Uganda alisisitiza kuwa watu waliozuru nchi hii kutoka nchi jirani za Afrika ya Mashariki hawangekuwa na budi ila kuji karantini kwa siku 14 kwa gharama yao, kwenye kituo cha serikali ama nyumbani mwao. Nchi hii inasifika kwa kuwa na masharti waliyo weka na kuhakikisha kuwa kila mwananchi anafuata. Walikuwa miongoni mwa nchi zilizo kuwa za kwanza kuweka marufuku ya mikutano ya watu wengi, ibada za kanisa na mahali kuna watu wengi kama vile harusi.

Nchi ya Kenya

Janga la Corona lime chukuliwa tofauti katika nchi tofauti za Afrika ya Mashariki. Visa vya  virusi hivi vya corona Afrika Mashariki vimeendelea kuongezeka, huku serikali za nchi tofauti zikifanya juu chini kukabiliana na tatizo hili. Katika nchi ya Kenya kufikia leo, kuna visa 50 vya watu ambavyo vipimo vyao vilidhibitisha kuwa chanya na virusi hivi. Serikali inaendelea kuweka kanuni za kuthibiti mwendo na muingiliano kati ya watu. Wiki iliyopita, serikali ilianzisha kafyu ya kutoka saa moja usiku hadi saa kumi na moja asubuhi. Mikutano kama vile ya kiharusi, mazishi ama hata kanisa yalipigwa marufuku na waliopatikana wakienda kinyume cha haya kuchukuliwa hatua kali.

Waziri wa Afya nchini Kenya, Mutahi Kagwe alisema kuwa watu 2,050 walio kuwa wame karantainiwa katika vituo tofauti nchini wanaendelea kupimwa ili kudhibitisha iwapo wana virusi hivi ama la.

Nchi ya Rwanda

Kwa umbali huu, nchi ya Rwanda imetangaza kuwa visa vya homa ya corona nchini ni 60. Katika tangazo lake wiki iliyopita, rais Paul Kagame alisema kuwa wanafanya vyote wawezavyo kuhakikisha kuwa familia zisizo jiweza zina chakula wanapo enda katika wakati wa lockdown nchini kote. Hatua hii itaathiri pakubwa watu wanao ishi miji mikuu ya Rwanda wasio kuwa na kazi za mwezi. Kwa hivyo watu wote maskini nchini wasio na uwezo wa kununua vyakula vyao watapatiwa vyakula na serikali.

homa ya corona

Nchi ya Tanzania

Nchi ya Tanzania ina idadi ya watu 19 walio na virusi vya homa ya corona. Bado serikali inafanya mikakati kudhibitisha watu wote walio ingiliana na watu hawa 19. Serikali ya Tanzania inafanya juu chini kuhakikisha kuwa watu wana mask za uso, kunawa mikono kwa kutumia mitakasio ya vileo vifaavyo na kuangalia umbali wa muingiliano. Ikilinganishwa nan chi za jirani ambazo zimekomesha usafiri, katika nchi ya Tanzania, usafiri bado unaendelea na watu bado wanaungana katika ibada za kanisa na kuenda mazishi. Jambo ambalo linahofiwa huenda likasababisha nchi kupata idadi kubwa ya watu walio na virusi hivi.

Sababu zinazo fanya visa vya maradhi haya kuongezeka katika nchi zinazo kua.

Idadi Kubwa ya kutosoma. Kuna tabiriwa kuwa idadi ya visa hivi vitaendelea kuongeza hasa katika Afrika ya Mashariki kwa kufuatia idadi kubwa ya kutosoma. Jambo ambalo linawafanya watu wengi kupuuza virusi hivi na kuvitupilia mbali kana kwamba ni maradhi ya kawaida. Hata baada ya serikali nyingi kufanya jitihada kuhakikisha kuwa wana kabiliana na kusambaa kwa virusi hivi, wananchi bado wanaendelea kutangamana kwa vikundi vya watu na kuenda kinyume cha matakwa ya serikali.

Umaskini mwingi katika mataifa haya ni jambo ambalo litafanya watu wengi katika mataifa haya kuadhirika na maradhi haya. Ikilinganishwa na nchi zilizo endelea kama vile Uchina na Ulaya, nchi za Afrika ya Mashariki hazina teknolojia iliyo imarika kukumbana na janga la covid-19. Pia nchi hizi zina tatizika kifedha kwa hivyo waki piga marufuku watu kutoka na kubaki manyumbani kwao, itakuwa vigumu kuwapatia wananchi wake msaada tosha wa vyakula. Kuwakimu kipindi wanacho faa kubaki manyumbani mwao. Pia nchi zinazo endelea hazina pesa tosha kununua mavazi maalum yanayo hitajika na madaktari katika wakati huu.

Visa Vya Homa Ya Corona Afrika Mashiriki Vyaendelea Kuongezeka!

Nchi zilizo endelea zina teknolojia inayo wawezesha kufuatilia na kuonyesha watu walio athirika na virusi vya homa ya corona. Kwa kupitia teknolojia hii, ni rahisi kwa wanao ishi sehemu tofauti kuwa makini na  kujua kinacho endelea. Idadi ya watu wasio na rununu ambazo zinaweza kuingia kwa mtandao katika nchi zinazo endelea ni kubwa sana. Inakuwa vigumu sana kuwajuza wananchi kinacho endelea.

Ni muhimu kwa kila mwananchi kuhakikisha kuwa anafuata maagizo na kanuni zilizo wekwa na wizara ya afya nchini mwao kuhakikisha kuwa tunakumbana na janga hili la virusi vya homa ya Corona Afrika Mashariki. Pia kuwa makini iwapo unashuhudia dalili zozote za corona kama vile kukohoa, joto jingi na ugumu wa kupumua, wasiliana na wizara ya afya nchini mwako.

Chanzo: Africanews, The East African

Written by

Risper Nyakio