Madaktari Wawashauri Wazazi Jinsi Ya Kuepuka Visa Vya Pediatric Emergencies Nyumbani

Madaktari Wawashauri Wazazi Jinsi Ya Kuepuka Visa Vya Pediatric Emergencies Nyumbani

Kufuatia kusambaa kwa kasi kwa virusi vya corona duniani kote, matembezi ya hospitalini yamepunguzwa kwa kiasi kikubwa ili kueza kushughulikia kesi za dharura. Na unapokuwa na watoto nyumbani, huwezi kosa kuwa na wasiwasi kufuatia visa vya pediatric emergencies kutokea. Kwa sababu, kusema bayana, ajali hutokea. Dr. Titilayo Adesanmi, daktari wa watoto na mkurugenzi wa matibabu ya Lifeforte Children's Medical Centre aliwashauri wazazi jinsi ya kuwaweka watoto wao kwenye usalama na kuepuka visa vya pediatric emergencies kuto tokea. Kuongeza kwa haya, mambo ya kufanya iwapo kisa cha dharura kinatokea.

pediatric emergencies

Jinsi ya kuepuka visa vya pediatric emergencies kuto tokea nyumbani mwako wakati huu wa janga la Covid-19

1.  Zingatia umbali wa muingiliano:

 • Usimpeleke mtoto mahali kuliko na umati wa watu (pahali penye zaidi ya watu 10).
 • Usimpeleke mtoto wako kwenye nyumba ya jirani wako.
 • Usimkubalishe yeyote anaye kutembelea kumbeba mtoto wako ama kumkaribia.
 • Usimkubalishe mwanao aje nawe hospitalini.

2. Weka vifaa vyote hatari mbali na watoto. Vifaa hatari ni kama vile:

 • Vifaa vilivyo na makali kama vile wembe, visu, makasi, na pini za ofisini.
 • Vifaa vidogo ambavyo mtoto wako anaweza weka mdomoni mwake kwa urahisi, mapua, masikio na vidoli vyenye vipande vidogo, shanga na pande ndogo za mapambo.
 • Vifaa vyenye sumu: Hivi ni kama vile dawa, sabuni, sabuni za maji, kerosen na vinginevyo ambavyo si CHAKULA ama VINYWAJI.
 • Vifaa visivyo salama: Hivi ni vifaa ambavyo vinasababisha hatari ya kifizikia kwa mwili wa mtoto wako. Kwa mfano, vipande vilivyo vunjika vya fanicha; sakafu inayo teleza, sehemu za sitima zinazo fikiwa na watoto, sanduku la vifaa (iliyo na vifaa kama vile nyundo, misumari na vinginevyo).
 • Mahali pasipo salama: Mahali hapa ndipo shughuli na vifaa kwenye nafasi hizi zinaweza hatarisha maisha ya mwanao kutokana na ajali za kinyumbani.
 • Kwa mfano, jikoni, mahali pa jenerata, mahali pa mashine ya kufulia nguo, meza ya kupiga pasi mtu anapo piga nguo pasi.

3. Hakikisha watoto wana angaliwa na mtu mzima wakati wote. Wanafikiria kwa kasi kuliko unavyo dhania!

 • Usiweke vifaa ambavyo wanaweza hitaji kutumia mbali sana mahali ambapo hawawezi fikia kwani kuenda jambo hili likawafanya wawe na fikira za kupanda vitu ili wafikie. Huenda wakaanguka wakijaribu kuvifikia. Badala yake, chukua vitu hivyo na uviweke kwenye chumba kingine wasipo kuwa wakiangalia.
 • Kuwa makini jinsi mtoto wako anavyo cheza. Michezo yoyote ambayo inaonekana kuwa hatari kama vile kupinduka, kuruka kutoka kwa kiti kimoja hadi kingine, kurusha vitu ambavyo vinaweza dunga mtu kama vile penseli kunapaswa kukemewa kwa upole.

4. Ongeza idadi ya usafi unao zingatia wa mazingara, chakula, mikono na mwili.

Kwani kwa sasa watu wengi zaidi kuliko hapo awali wako kwa nyumba na masaa mengi, nyumba huenda ikawa chafu zaidi kuliko isivyokuwa kwa kawaida na kwa hivyo inahitaji juhudi zaidi kusafisha. Huwezi wathibiti watoto kugusa vitu tofauti karibu yao, sakafu na nguo zao ikiwemo za watu wazima. Watoto wanaingiza mikono hiyo hiyo kwenye vinywa vyao, na vijidudu vyote walivyo okota wakigusa gusa vitu vyote. Huku kuna ongeza hatari za kuambukizwa katika watoto kama hao. Hii ndiyo maana ya kuhakikisha kuwa usafi unazingatiwa kwa umakini.

Katika mambo ya kuzingatia usafi wa kibinafsi:

 • Huku kunamaanisha kumbadili mtoto diaper mara kwa mara.
 • Kumsafisha vyema baada ya kuenda haja ndogo ama kubwa (hasa kwa wasichana).
 • Kumsafisha mwili mara kwa mara (angalau mara moja kwa siku, huku watoto wachanga waki simamiwa)
 • Kumsugua meno na kuhakikisha mdomo wake ni safi wakati wote.

5. Hakikisha kuwa mwanao  anakula lishe bora yenye afya na kupata usingizi tosha.

pediatric emergencies

Pediatric emergencies: Jinsi ya kutambua na mambo ambayo unaweza fanya

Hapa ni baadhi ya ishara kuwa mwanao anahitaji matibabu ya dharura:

 • Joto jingi: Mvue mwanao nguo, mpapase kwa kinguo kilicho rowa kwenye maji, kisha umpe mwanao paracetamol (fuata maagizo yaliyo andikwa kwenye kijisanduku cha dawa). Kisha umpeleke mwanao kwa daktari wako bila kusita aweze kukaguliwa.
 • Convulsions (Seizures)/kulia kwingi kusiko kwa kawaida: Usiwekelee vifaa vyovyote kwenye mdomo, mapua, ama masikio ya mwanao, toa vifaa hatari karibu na mwanao, toa nguo zake, mlaze kwa upande kisha uelekee kwenye hospitali iliyo karibu nawe kuhakikisha mwanao anakaguliwa ifaavyo.
 • Matatizo ya kupumua: Toa nguo zote ili kusiwe na vizuizi vya kupumua vyema. Hakikisha kuwa kichwa chake kimeinuliwa, epuka kumlisha vitu kwa mdomo hadi pale ambapo daktari wake atakapo mpima. Hakikisha unatembelea hospitali iliyo karibu zaidi nawe iwapo daktari wa mtoto wako hayuko karibu.
 • Kupumua kwa kasi
 • Kupumua kwenye kelele
 • Kutapika mara kwa mara: Koma kumlisha vyakula ama vinywaji kisha uelekee kwenye hospitali iliyo karibu zaidi nawe.
 • Kinya kilichojaa unyevu nyevu (kunya mara tatu ama zaidi kwa siku): Mpe Oral Rehydration Solution (ORS) kadri mtoto wako awezavyo kuchukua, kwa vipindi visivyo tengana sana, mpe tembe za oral zinc (fuata maagizo yaliyo andikwa kwenye upande wa nyuma wa kijisanduku cha dawa hizo), kisha umpeleke mwanao akaguliwe na daktari wake ama kwenye hospitali iliyo karibu zaidi nawe.
 • Kushuhudia kudhoofika kwa mwili wote: Kitembelee kituo cha matibabu kilichoko karibu zaidi nawe bila kusita.
 • Kutoa damu kutoka sehemu yoyote ya mwili: Wekelea shinikizo kwenye sehemu hiyo kwa kutumia kitambaa kisafi (hasa cha kuchemulia) kisha uelekee kwenye hospitali iliyo karibu zaidi nawe. Wajulishe watu wengine wazima walio karibu nawe iwapo unaona kana kwamba maisha ya mwanao yamo hatarini. Wajulishe unavyo taka wakusaidie.
Tahadhari za kuzingatia unapo enda hospitalini wakati wa janga la Covid-19
 Ni vigumu kuepuka visa vya dharura katika baadhi ya manyumbani. Kwa hivyo tia maanani tahadhari zifuatazo unapo mpeleka mwanao hospitalini.
 • Usiwabebe watoto wengine nawe ambao si wagonjwa, unapoenda hospitalini.
 • Mmoja ama wawili kati ya watu wazima wanapaswa kumpeleka mtoto hospitalini.
 • Angazia umbali kati ya watu kadri uwezavyo unapo fika hospitalini.
 • Epuka kugusa vitu ambavyo hauhitaji kugusa.
 • Nawa mikono mara kwa mara unapokuwa hopsitalini.
 • Nawa mikono muda tu kabla ya kutoka hospitalini.
 • Punde tu unapofika hospitalini, vua nguo zote (jambo hili ni kwa kila mtu aliye enda hospitalini) na uzitenge kando) (Zinapaswa kuoshwa kando na nguo zingine).

pediatric emergencies

Kwa kuyataja haya yote, bila shaka kuna baadhi ya vitu ambavyo lazima viwe kwenye sanduku la huduma za dharura za kwanza. Vitu hivi ni:

 • Paracetamol syrup na tembe (za watoto wenye umri mwingi)
 • Oral Rehydration Salt (ORS)
 • Tembe za Zinc
 • A packet of white handkerchiefs
 • Plaster
 • Antiseptic solution (kama vile Savlon) ama Methylated spirit
 • Pamba

Soma pia: What Are The Signs Of Dehydration In Children?

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Syreeta Akinyede kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio