Baadhi Ya Vita Vinavyo Tendeka Mara Kwa Mara Katika Miaka Ya Kwanza Ya Ndoa

Baadhi Ya Vita Vinavyo Tendeka Mara Kwa Mara Katika Miaka Ya Kwanza Ya Ndoa

Ndoa ikiwa bado changa inakabidhiwa na changamoto tofauti. Vita vya mara kwa mara vina shuhudiwa. Kufuatia kuto kubaliana kwa mambo ya kimsingi kama vile utumizi wa pesa na sababu zinginezo.

Changamoto nyingi zinazo ipuka mara watu wawili wanapokuja pamoja yanaweza kuleta matatizo mengi na kuingilia uhusiano wao na pia fedha. Hizi husababisha vita vya mara kwa mara kati ya wanandoa miaka ya mwanzo katika ndoa.

Idadi kubwa ya watu huingia kwenye ndoa na tarajio kuwa watapata mwenzi mwema asiye na doa. Ila uhusiano unapo fanywa rasmi, ukweli unaanza kuwa dhahiri- ndoa si rahisi kama tunavyo dhani. Na kuleta pamoja familia, husiano, vitu vya kibinafsi, fedha, matatizo na shida zina ibuka.

Mtaalam wa uhusiano wa Marekani anaamini kuwa vita hivi vya wana ndoa hutendeka mnamo mwaka wa kwanza wa ndoa. Pia wana peana ushauri wa jinsi ya kutatua matatizo haya.

 

Angalia Baadhi Ya Vita Vya Mara Kwa Mara Kati Ya Wanandoa

Vita vya kipesa

Hii ni mada inayo jadiliwa sana kati ya wanandoa wengi- hasa waliofunga pingu za maisha hivi karibuni na wameanza kuleta fedha zao pamoja, wameanza kununua vitu vya nyumba pamoja kwa wakati wa kwanza ama wanafikiria kuhusu kuanza familia pamoja. Wanapo kuwa na uchumba, ama pia wanapo anza kuishi pamoja, inaweza kuwa rahisi kuficha fedha zako. Wanapo funga pingu za maisha, wenzi wengi hufahamu ukweli kuhusu mambo kama deni mchumba wake alizo nazo, ama kufahamu kuhusu tabia za utumizi pesa hata kama hawakubaliani nazo.

Muwe waaminifu, wepesi na mkiri hisia zenu za fedha kati yenu. Baada ya hapo mje pamoja na mkuze wazo ambavyo mta songa mbele na maisha yenu mapya ya kifedha pamoja.

Vita vya kimapenzi

Baadhi Ya Vita Vinavyo Tendeka Mara Kwa Mara Katika Miaka Ya Kwanza Ya Ndoa

Ni rahisi kupoteza hamu ya mapenzi mliyo kuwa nayo na kuipuuza. Unaweza fikiria kuwa kuendelea kufanya mapenzi ni jambo la kawaida ambalo halite hitaji bidii. Ukweli ni kuwa wanandoa wengi hupitia zamisho katika maisha yao ya kimapenzi katika mwaka wa kwanza wa kuoana. Maisha ya kimapenzi inayo didimia inaweza leta tofauti kati yenu. Hasa iwapo mwenzi mmoja anapo jaribu kuuwasha moto uliokuwa hapo awali. Na mwengine anaona haya hayatoshelezi mahitaji ya kimapenzi ya mpenziye.

Ni kawaida moto uliokuwa wa mapenzi kudidimia punde baada ya harusi na wawili wenu kuto furahishwa na maisha ya mapenzi yenu. Mna paswa kuwa na majadiliano mwafaka kuhusu kufanya mapenzi. Chunguza hamu zako na ukabiliane na hisia za kuumizwa, hasira na hatia.

Vita vya mipaka

Huenda ikawa ni marafiki wanao tembea bila ya kusema. Mara nyingine ni wakwe wanao uliza maswali ya umbeya. Na wakati mwengine ni mwenzi kufanya uamuzi wa mambo ya kifamilia bila kumhusisha mwengine. Mipaka mibaya na wanafamilia inaweza kutatiza ndoa. Ni muhimu kuwa na uhusiano mwema na Marafiki na wanafamilia baada ya kufunga ndoa. Iwapo muda kwa muda kuwapa wengine kipao mbele na kutupilia mwenzi wako itatatiza uhusiano wenu.

Kuwa makini kwa mahitaji ya mpenzi wako kila siku na wanahitajika kufanya hivyo pia. Nyinyi ni wazima na watu wazima wana uwezo wa kueka mipaka panapo faa. Iweke ndoa yako na mpenzi wako kwanza. Vita vitakua iwapo mpenzi mmoja anaipa familia na marafiki zake kipao mbele na kutupilia mahitaji ya mpenzi wake.

Vita vya kugawana kazi

Kuamua jinsi ya kugawana kazi za nyumba hukua changamoto punde baada ya kuoana. Una epukana na kumfanya mwengine kuhisi wao ndio wanao fanya kazi zote. Ila ni muhimu kwa afya ya uhusiano wenu. Utafiti wa hivi punde ulionyesha asilimia 56 ya watu walio oana wana maoni kuwa kugawana kazi za nyumbani ni muhimu kwa fanaka ya ndoa.

Iwapo kazi na majukumu mengi ina kuwa kwa mwenzi mmoja, chuki huanza kuibuka na hoja zisizo isha. Katika pande ya dunia tunapo ishi, wanawake ndio wanao fanya kazi nyingi za familia ila sio wakati wote. Unafaa kuwa na mjadala na mpenzi wako na muwe na makubaliano. Jambo hili ni muhimu ili kuwa na kiwango cha familia ambacho nyote mnafaa kufuata.

 

Read Also: Challenges That Childless Couples Face And How To Respond To Them

Written by

Risper Nyakio