Watu wana tofauti nyingi, tofauti ambazo husababisha kutosikizana. Ukifuata baadhi ya vidokezo vya kuwa na vita vyenye haki, unaweza kuhakikisha kuwa vita vina isha bila kufanya matatizo yenu yawe mengi zaidi. Ni muhimu kwa wanandoa kuhakikisha kuwa wana vita vya haki katika ndoa kuepuka kuwa na matatizo zaidi katika ndoa. Tazama jinsi ambavyo wanandoa wanaweza timiza haya.
Vita vya haki katika ndoa

- Zungumzia suala linapo ibuka usingoje
Ni muhimu kumjulisha mchumba wako punde tu tatizo linapo anza kukusumbua. Kadri unavyo acha suala likusumbue ndivyo unavyo kasirika zaidi. Unapo amua kuzungumza kuhusu jambo uliloweka moyoni, unaongea kwa hasira na sio haki kwa mchumba wako. Mwongozo mzuri wa kuhakikisha kuwa unazungumzia suala kwa haki ni kuto zungumzia jambo lililotendeka masaa 48 ama zaidi. Zungumzia suala punde tu linapotokea na una nafasi ya kulitatua. Ikiwa mchumba wako hatazungumzia suala hilo, unapaswa kuwauliza watenge muda kwa masaa 24 yajayo ili mlizungumzie. Ikiwa uhusiano huo ni muhimu, wataelewa na watakuwa na furaha kuwa uliibua mazungumzo ya kulitatua.
2. Usiibue mambo yaliyofanyika hapo awali
Unapokuwa na vita na mchumba, fanya kadri uwezavyo usiibue mambo ya awali kwenye vita vyenu. Unapozingatia mada ya vita vyenu, kuna nafasi chache kuwa hisia hazitaumizwa na matatizo zaidi hayataibuka. Matatizo yoyote uliyokuwa nayo hapo awali hayajalishi katika suala lililo mezani. Kuyaibua kutamweka mchumba wako katika hali ya kujikinga na kuingilia mazungumzo yenu.

3. Usisahau suala kuu
Unapozungumzia suala linalohitaji kujadiliwa, hakikisha kuwa hakuna vitu vinavyo kuvuruga na kuingilia mazungumzo yenu. Kuwa na uhakika kusikiliza mchumba wako anachosema na pia lugha ya mwili wake. Kwa njia hii, nyote wawili mnaweza kuelewana kwa uwazi na muweze kutatua masuala yenu kwa njia bora zaidi.
Pia, wanandoa wanaweza kujadili matatizo yao wakiwa wameshikana mikono. Njia hii inasaidia kupunguza hisia za hasira ambazo zinaweza kutokea wanandoa wanapozungumzia matatizo yao. Mazingara haya yanaboresha wanandoa wote wawili kuwa na starehe na kuwa na mazungumzo wazi na maelewano.
Chanzo: Free Articles