Visa Vya Vita Vya Kinyumbani Vyaongezeka Duniani Kufuatia Lockdown Ya Corona

Visa Vya Vita Vya Kinyumbani Vyaongezeka Duniani Kufuatia Lockdown Ya Corona

Kumekuwa na ongezeko la vita na vurugu za kinyumbani kufuatia watu kuwa nyumbani kufuatia lockdown ya janga la corona.

Kumekuwa na ongezeko la ripoti kuhusu vita vya kinyumbani tangu lockdown kufuatia mlipuko wa virusi vya corona. Duniani kote, miungano inayo saidia waathiriwa wa vita vya kinyumbani imeripoti ongezeko la visa vya vurugu za kinyumbani na watu kutoka sehemu duniani kote waliobaki manyumbani na wanao wadhalilisha kufuatia janga la corona. Mahali kama Berlin, Paris, Madrid, Rome, Bratislava na Lagos zote zime shuhudia ongezeko katika ripoti za vita vya kinyumbani kutoka pale ambapo lockdown ilianza.

Vita Vya Kinyumbani Wakati Wa Lockdown Ya Corona

a man's clenched fist

Kulingana na German Federal Association of Women's Counselling Centres and Helplines (BFF), vikwazo vinavyo sababishwa na kutengwa kijamii vinazidi na kuongezeka "hatari za kudhalilishwa kingono na kinyumbani dhidi ya ya wanawake na watoto."

Shirika la haki za wanawake, Weiping imeripoti ongezeko la mara tatu katika ripoti za vurugu dhidi ya wanawake. Wakati Spain, mama wa miaka 35 mwenye watoto wawili aliuliwa na mwenzi wake.

Katika nchi ya Nigeria, anaye wasiliana na timu ya mwito ya vurugu za kinyumbani na kudhalilishwa kingono, Bi. Titilola Vivour-Adeniyi aliwaambia wana ripoti kuwa kumekuwa na ongezeko la nambari za simu wanazo pata kila siku.

Hali ilivyoko inaweka timu za mwito katika hali dharura. Wafanyakazi wengi wa huduma za kijamii wako nyumbani na wanashindwa kuwa fikia waathiriwa na iwapo waathiriwa wanatolewa manyumbani mwao, kuna hiari chache sana za watakako enda.

domestic violence during coronavirus

Wanawake wametupigia na kutuambia kuwa wanashuhudia vita nyumbani. Wanauliza: Nitaenda wapi? alisema Canan Gullu, kutoka Shirika za Wanawake za Turkey.

Ili kuwapatia waathiriwa hiari huko Ujerumani, Franziska Giffey ameita manispa kupanga vituo tofauti za kuwa karibisha watu hawa iwapo inatakikana. Austria inatoa mahala salama katika makimbizi ya wanawake ama kutoa wanafamilia wanao zua vurugu kutoka kwa familia. Wakati huko Uitaliano, nchi iliyo na lockdown zinazo zingatiwa zaidi, waadhiriwa wanaweza toka manyumbani mwao bora wame beba hati zinazo dhibitisha kwa nini wanatoka.

Je, mji wa Lagos unawafanyia nini waathiriwa?

Nigeria domestic violence hotlines

Kati ya mataifa ya Nigeria, Lagos ina idadi ya juu zaidi ya visa vilivyo dhibitishwa, na ndiyo sababu kwa nini serikali kuu imeagiza kudhibiti kwa mwendo kabisa maalum kama complete lockdown. Kwa hivyo Lagos State Domestic and Sexual Violence Response Team (DSVRT) inatarajiwa kutumia teknolojia kusaidia waathiriwa wa vurugu za kinyumbani na kudhalilishwa kingono.

"Lazima tutumie vyema teknolojia kadri tuwezavyo. Tumeenda kwa mtandao kwa sasa, tuna wasiliana na wateja wetu kupitia kwa barua pepe, mitandao ya kijamii ama simu zetu". Kulingana na Bi. Titilola Vivour-Adeniyi, wanaegemeza kupitia kwa wanajamii na kwa vituo vya polisi. Pia wana wapatia huduma za ushauri. " Tunafanya ushauri mwingi, tuna wana sykolojia wetu wa maabara wanao ongea na waathiriwa, ila tuna shauri usalama. Iwapo mtu yeyote anahisi ako katika hatari ya vurugu za kinyumbani, anapaswa kumwambia angalau mwana familia anaye mwamini," alisema.

Kuongezea zaidi, ali wahimiza marafiki na wanafamilia kuwa angalia wapendwa wao katika kipindi hiki. Walakini, alihimiza kuwa inapaswa kufanywa kupitia kwa kupiga simu ama kwa ujumbe wa simu ama pia kwa WhatsApp.

 Iwapo unakumbana na vurugu za kinyumbani ama kudhalilishwa kingono, wasiliana na wizara ya afya kwa kutumia nambari hii +254-20-2717077, 0729 471 414, nambari sare: 0800721316 ama barua pepe: [email protected]

Soma PiaDomestic Violence In Kenya: The Home No Longer Safe For Kenyan Women?

Chanzo: Herald

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Lydia Ume kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio