Vitabu 5 Bora Vya Kusoma Unapokuwa Na Mimba

Vitabu 5 Bora Vya Kusoma Unapokuwa Na Mimba

Want to know how special your pregnancy journey is? This list of 5 spiritual books to be read during pregnancy will help guide you through your pregnancy!

Mimba ni safari njema na ya kupendeza! Na iwapo ungependa kuelewa jinsi safari hii ya mimba ni spesheli, unapaswa kuangalia orodha yetu ya vitabu bora vya kiroho vya mimba.

Kwa sasa kwani una mimba, ni kawaida kwako kununua vitabu vya mimba ili kuelewa mabadiliko unayo yatarajia. Bila shaka unapaswa kuongeza vitabu vya kiroho kwa kitita chako cha vitabu! Utafurahia kupata maarifa zaidi kwenye maisha yako na yale ya mtoto wako.

Hapa kuna orodha ya vitabu bora vya kiroho vya mimba:

1. The Mindful Mother: A Practical and Spiritual Guide to Enjoying Pregnancy, Birth and Beyond with Mindfulness – Naomi Chunilal

mindful mum

Kitabu hiki ni mwongozo bora wa kiroho kwa mama mtarajia. Kitakusaidia kuwa na umoja na mimba yako katika hisia na mawazo. Na kukutayarisha kwa vita na mashindano ya kuwa mama.

best spiritual books to read during pregnancy

Kinatumia mbinu za kuzingatia masharti ya yoga na Buddhist. Masharti haya yatakuwezesha kuona kujifungua kama kitu chanya. Iwapo viwango vya nishati vitapunguka, kitabu hiki kitakuonyesha jinsi ya kupata nishati zaidi na kuifurahia mimba yako. Je, una furaha ya kutengeneza familia ya kupendeza? Kitabu hiki kinapaswa kukusaidia kupata nguvu za kiroho katika safari yako ya mimba!

2. Spiritual Pregnancy: Develop, Nurture, and Embrace the Journey to Motherhood – Shawn Tassone & Kathryn M. Landherr

nurture

Spiritual Pregnancy ni kitabu cha lazima kusoma kwa wamama wote walio na mimba! Utapata ufahamu zaidi kuhusu maisha ya kiroho ya mimba. Hii itakuwa safari isiyo sahaulika kwako na kwa mtoto aliye tumboni mwako! Waandishi ni madaktari walio na vyeti na wataalum kuhusu maisha bora, na wame andika kitabu kitakacho kuongoza katika safari hii. Utakuwa na ufahamu zaidi wa kiroho, kifizikia na hisia kwako na mtoto aliye tumboni. Nunua kitabu hiki kama mojawapo ya vitabu vya kiroho vya kusoma unapokuwa na mimba.

Vitabu bora vya kusoma unapokuwa na mimba: Kuendeleza orodha

3. The Mindful Mom-To-Be: A Modern Doula's Guide to Building a Healthy Foundation from Pregnancy Through Birth – Lori Bregman

vitabu bora vya kiroho vya mimba
The Mindful Mom-To-Be ni njia bora ya kuanza ujauzito wako. Kitabu hiki kitakuhimiza kujua kinacho kufaa wewe na mtoto wako. Bregman ana washauri wamama wote walio na mimba na mazoezi bora ya kihisia na kiroho katika kitabu hiki. Kitabu hiki pia kina matibabu ya kiasili, ushauri wa vyakula, na mbinu tofauti za uchungu wa uzazi na hatua za maendeleo. Bregman ana hiari kuwa sio mtoto wako tu anaye zaliwa. Wewe kama mama, pia utakuwa unapitia kipindi cha kuzaliwa tena. Hiki ni kitabu bora kwa kila mama anaye tarajia kujifungua.

4. The Positive Birth Book: A New Approach to Pregnancy, Birth and the Early Weeks – Milli Hill

the book

The Positive Birth Book ni kitabu chenye maarifa na joto nyingi. Mwongozo huu wa mimba utakusaidia kuelewa zaidi kuhusu mimba, kutunga hadi wiki chache baada ya kuzaliwa kwa mtoto wako. Pata ujumbe zaidi kuhusu mambo unayo taka kujua kuhusu uchungu wa mama, kunyonyesha mtoto, upasuaji wa C-section. Mwongozo huu utakuwa bora zaidi katika kweli hizi!

Kitabu hiki kinakusaidia kuwa na maelezo yanayo faa, na kukusaidia kwani mawazo yako yanaweza kukusaidia kuamua kujifungua ambako unaweza penda kushuhudia.

5. The Natural Pregnancy Book – Aviva Jill Romm

vitabu bora vya kiroho vya mimba

Kitabu cha Romm ni cha wamama wanao tarajia kuwa wazazi wanao taka vitu bora zaidi kwa watoto wao. Kitabu hiki kinakupa ujumbe muhimu kwa njia ya kueleweka kwa urahisi. Mwandishi wa kitabu hiki ni mtaalum wa kujifungua kwa njia asili na anatumia mbinu ya kijumla kwa mwongozo wake wa mimba. Pata ujumbe kuhusu matibabu kwa njia inayo eleweka. Pia utakuwa na maarifa zaidi kuhusu uwoga, ugonjwa wa asubuhi, uchovu na alama za kunyooka. Kitabu hiki kina shauriwa kwa sana kwa wamama walio na mimba.

Kumbukumbu: nhs

Soma pia: Why kids want you to read the same story over and over again

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Julie Adeboye kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio