Vitamu Tamu Bora Na Vyenye Afya Kwa Mama Mwenye Mimba

Vitamu Tamu Bora Na Vyenye Afya Kwa Mama Mwenye Mimba

Kwa wanawake wenye mimba, ni vyema kuhakikisha kuwa wanakula vyakula vyenye afya. Hata vitamu tamu vyao vinapaswa kuongeza virutubisho mwilini.

Mimba huja na hamu nyingi ya kula vyakula tofauti. Kwa hivyo ni rahisi kwa mama kujipata akitamani kula vyakula vyenye ufuta mwingi na visivyo usaidia mwili wake kwa jambo lolote. Makala haya yana waelimisha mama kuhusu vitamu tamu katika mimba vyenye afya na vitakavyo wasaidia katika kipindi hiki.

Orodha ya vitamu tamu bora katika mimba

Vitamu Tamu Bora Na Vyenye Afya Kwa Mama Mwenye Mimba

Tufaha

Kwa wanawake wenye mimba, ni vyema kuhakikisha kuwa wanakula vyakula vyenye afya. Hata vitamu tamu vyao vinapaswa kuongeza virutubisho mwilini. Tufaha ni tunda linalo sifika kwa faida zake nyingi za kiafya. Tunda hili ni bora ukiwa unatarajia. Ili kulipa utamu zaidi, unaweza paka kijiko kimoja cha siagi ya njugu.

Vibanzi vya tortilla na guacamole

vitamu tamu katika mimba

Kuna mara ambapo mwili wa mama mjamzito una matamanio ya vitu vitamu tamu. Vibanzi hivi vimetengenezwa kwa kutumia nafaka nzima na zina fiber nyingi. Unaweza kula pamoja na guacamole ambapo ni tunda la parachichi limechanganywa na kitunguu na nyanya. Kwa kufanya hivi, mama anapata protini, vitamini B na folate.

Maziwa ya bururu na matunda na njugu

Kula angalau vijiko vitatu vya bidhaa za maziwa zenye ufuta mdogo. Kufanya hivi kuna kusaidia pamoja na mwanao kupata kalisi tosha ya mifupa yako na meno. Maziwa ya bururu yana protini nyingi na kukufanya uhisi kushiba. Una shauriwa kuchagua maziwa ya bururu yasiyo na sukari ya kuongezea. Kisha uongeze njugu na matunda unayo yapendelea zaidi.

Smoothies

chocolate avocado smoothie

Hivi ni vinywaji vinavyo tengenezwa kwa kutumia maziwa ya wanyama ama ya bururu. Una siaga pamoja na matunda kama vile mandizi, parachichi na njugu. Uko huru kuongeza spinachi ili iwe na vitamini zaidi. Fahamu kuwa, unaweza kuongeza aina tofauti za matunda.

Chokleti na matunda

vitamu tamu katika mimba

Tuna habari njema kwako. Usiogope kula chokleti yako mara kwa mara, ina kusaidia kupunguza hatari ya kupata preeclampsia. Hali inayo sababisha shinikizo la juu la damu na kuharibika kwa baadhi ya viungo vya mwili kwa baadhi ya wanawake. Ongezeka mojawapo ya matunda unayo yapenda katika kipindi hiki kisha uifurahie chokleti yako. Maziwa yaliyoko kwenye chokleti yana saidia kuimarisha mifupa ya mtoto wako.

Tuna sandwich

Kulingana na utafiti mpya, wanawake wenye mimba wanaweza kula samaki angalau mara mbili kwa wiki. Kufuatia wingi wa protini na omega-3 fatty acids zilizoko kwenye samaki ama kwa bidhaa za samaki. Zinasaidia pakubwa katika ukuaji wa ubongo wa mtoto. Unaweza ongeza parachichi ama mtama mzima kwenye sandwich yako.

Njugu na popcorns 

Chakula chenye fiber nyingi kinamsaidia mama mwenye mimba kuponya kukosa maji tosha mwilini kufuatia vitamini za prenatal wanazo chukua. Kitu kizuri ni kwamba unaweza tengeneza popcorns nyumbani kwa urahisi bila kununua. Kisha uongeze kiwango kidogo cha njugu.

Soma Pia :Chakula Cha Mimba: Je, Ni Salama Kula Kitunguu Saumu Ukiwa Na Mimba?

Written by

Risper Nyakio