Vitamu Tamu Vitano Wakati Wa Ujauzito

Vitamu Tamu Vitano Wakati Wa Ujauzito

Ni vyema kwa mama mjamzito kuwa makini sana na vyakula anavyo kula katika kipindi hiki na kuhakikisha kuwa vina afya.

Kutoka jadi, kumekuwa na imani zisizo za kweli kuwa wanawake wajawazito wanapaswa kula chakula cha watu wawili; chake na mtoto aliye tumboni mwake. Na imani hii huenda ndiyo inayo wafanya wanawake walio na mimba kula kila kitu wanacho patana nacho. Kula vyema na uzingatie afya na pia viwango ili kuepuka kupata uzito mwingi ambao huenda ukasababisha matatizo ya kiafya. Hakikisha pia unakula chakula chenye afya na virutubisho tosha ili kuhakikisha mtoto wako ana faidika kutokana na chakula hicho. Tazama orodha tuliyo kuandalia ya vitamu tamu ukiwa na mimba.

Vitamu tamu hivi vyenye afya ni bora ukiwa na mimba

Vitamu tamu hivi vinakusaidia kudhibiti unavyo kula ukiwa na mimba.

  • Tikiti maji

food to last longer in bed

Tunda hili ni rahisi kupata na pia kwa bei nafuu. Asilimia yake kubwa ya maji ni muhimu sana mwilini. Wataalum wanashauri wanawake wenye mimba kula tunda hili mara tatu kwa siku. Lina wingi wa vitamini kama vile vitamini A, B6, potassium, magnesium na vitamini C. Tikiti maji pia ina lycopene inayo saidia kutatua tatizo la ngozi kuharibika wakati wa mimba. Mbali na hayo, tunda hili linasaidia na miguu iliyo fura, kuumwa na misuli, kichefu chefu na kiungulia kwa sababu ya wingi wa maji katika tunda hilo.

  • Cucumber

Cucumber

Tunda hili lina asilimia kubwa ya maji na wanawake wajawazito wanaweza faidika sana. Anuwai ya faida ni kama vile kupunguza uzito, shinikizo la damu na mabadiliko ya ngozi kufuatia ujauzito.

  • Ndizi

vitamu tamu ukiwa na mimba

Potassium ni muhimu sana mwilini na hasa unapokuwa na mimba, unapaswa kuhakikisha kuwa unapata viwango tosha mwilini. Ndizi zina wingi wa potassium. Ina saidia kusawasisha shinikizo la damu wakati wa ujauzito, na kuhakikisha kuwa kiwango chake ni cha kawaida wakati wa ujauzito.

  • Njugu

 

Njugu ni rahisi kutayarisha na kubeba unapokuwa na mimba. Zina wingi wa protini yenye afya, ufuta na fibre. Fibre ni muhimu wakati wa ujauzito kwa sababu ya kusaidia na vyakula vikiwa kwa matumbo, kuepuka kukosa maji tosha mwilini ambayo huwa maarufu sana katika mimba.

Hitimisho

Vitamu tamu vingine vyenye afya katika wakati huu ni kama vile mahindi ya kuchemsha, parachichi, tufaha na karoti. Vyote hivi vina virutubisho tofauti na vitamini vinavyo hitajika mama akiwa na mimba. Vyote hivi maarufu, vya bei nafuu na kupatikana kwa urahisi nchini kote.

Soma PiaVidokezo Muhimu Kwa Mama Mwenye Mimba

Written by

Risper Nyakio