Uwazi katika uhusiano na mchumba wako ni muhimu. Kunawawezesha kuaminiana na kuboresha utangamano wenu. Hata hivyo, kuna mifano ya hali ambapo ni sawa kutomweleza mchumba wako kila kitu. Kuna vitu ambavyo mchumba wako hapaswi kujua kukuhusu. Kufahamu baadhi ya vitu huenda kukamfanya akose imani kwako na kuleta utata katika uhusiano wenu. Kwa hivyo badala ya kumweleza vitu vitakavyo mwumiza moyo, ni vyema kujiwekea habari zingine.
Vitu ambavyo mchumba wako hapaswi kujua kukuhusu

- Wapenzi wako wa hapo awali
Hata kama mna urafiki wa ndani zaidi na mchumba wako, hakuna anayetaka kusikia kuhusu wachumba wako wa awali. Mliyoyafanya na habari za undani. Hata anapokuuliza, ni vyema kuweka ujumbe huu siri. Nafasi kubwa ni kuwa ujumbe huu utatumika kuzua vita siku za usoni.
2. Watu wanaokutaka kazini
Ni vigumu kwa mwanamke kutokuwa na watu wanaomtamani popote pale aendapo. Ikiwa una mwanamme anayekutaka kazini na mara kwa mara anakusumbua kuwa angependa muwe na uhusiano. Mweleze rafiki yako na wala sio mchumba wako. Kwani huenda akawa na shaka za imani. Kila unapoenda kazini, huenda akadhania kuwa utamwacha siku moja na kuwa na mchumba wa kazini.

3. Watu uliohusika kingono nao
Wanawake, ujumbe huu, ni wako wa siri. Mbali na daktari wa afya ya kike, wengine hawapaswi kujua nambari hii. Hata kama unamwamini mpenzi wako sana, huenda akatumia ujumbe huu kukuumiza.
4. Unapokuwa na crush
Kumpenda mtu kwa dhati hakumaanishi kuwa hautapendezwa na watu wengine mara kwa mara. Na ni kawaida. Ila, unapokuwa katika uhusiano na mtu, ni vibaya kujaribu kuingia katika uhusiano na mtu mwingine. Unapokuwa unapendezwa na mtu mwingine, epuka kumjuza mchumba wako.
5. Hupendi wazazi wake
Kutowapenda wakwe zako na familia ya mchumba wako sio jambo geni. Hasa wanapojaribu kuingilia maisha yenu, huenda ukahisi kuwa wamekiuka mipaka na ukakosa kuwapenda. Hata hivyo, epuka kumweleza mchumba wako kuwa unawachukia wazazi wake ama familia yake. Badala yake, mweleze vitu ambavyo familia yake inafanya visivyo kupendeza.
Chanzo: Africaparent
Soma Pia: Je, Kuna Madhara Hasi Ya Kufanya Mapenzi Katika Mimba Kwa Mama Mjamzito