Kuelewa vitu ambavyo wanaume hufanya vinavyoharibu uhusiano kutawasaidia kujitenga navyo na kuwa na mahusiano bora zaidi. Tazama baadhi ya vitu maarufu wanavyovifanya visivyofaa na kuathiri mahusiano yao.
1.Kudanganya

Jambo moja ambalo wanaume wengi hufanya kwa ustadi ni kudanganya. Hata kama kutasaidia kutoka kwa tatizo kwa dakika chache, kudanganya huharibu imani kati ya wachumba. Tabia huchangia pakubwa katika kutengana kwa wachumba wengi. Wanaume wanaodanganya wanaongeza nafasi za kuharibu uhusiano wao kwa kasi.
2. Kuvunja imani
Imani ni muhimu katika uhusiano wowote ule. Mwanamke unayempenda atakuamini katika mambo mengi, ila, unapovunja imani yake, ni vigumu kwake kukuamini tena katika lolote lile. Imani inapoisha katika uhusiano, uhusiano huisha.
3. Kutomuelewa mpenzi wako

Kutochukua muda kumuelewa mchumba ni ishara dhahiri kuwa hujali kuhusu hisia ama maisha yake. Ikiwa unampenda mpenzi wako, chukua muda kuelewa vitu anavyopenda na asivyopenda. Sio vigumu kumuelewa mtu. Unapotatizika kuelewa kitu chochote anachofanya, mkalishe chini umwulize kinachoendelea.
4. Kutomzawadi mpenzi wako
Kosa kubwa kuliko kumpa mpenzi wako zawadi ni kumpa zawadi asiyotaka. Machoni mwa mwanamke, mwanamme anapaswa kufahamu zawadi bora ya kumpa. Zungumza na mpenzi wako ufahamu anachotaka. Kwa njia hii, utakuwa na maoni ya zawadi ambazo anaweza furahia katika siku zake spesheli.
5. Kutozungumza vya kutosha naye
Kuzungumza kunaweza kuwa vigumu kwa wanaume na rahisi sana kwa wanawake. Lakini mazungumzo ni muhimu katika kudumisha uhusiano hasa wa kimapenzi. Usipozungumza na mpenzi wako, ataona kana kwamba una watu wengine unaozungumza nao ama hutaki kujua kinachoendelea maishani mwake. Chukua muda kila siku kumpigia mpenzi wako simu kujua kinachoendelea.
6. Kumfanya akose kuhisi salama

Mwanamke kuhisi kuwa ako salama na mpenzi wake ni muhimu ili uhusiano kustawi. Mwanamke anapohisi ako salama, itakuwa rahisi kwake kumwamini mchumba wake na kumweleza kinachomsumbua. Mazungumzo hupungua na mwishowe mapenzi kudidimia. Mwanamme asipompatia mwanamke nafasi ya kuhisi salama ni chanzo cha uhusiano kuisha.
7. Kutotimiza ahadi zako
Mwanamme anayetimizia ahadi yake huaminika na mpenzi wake. Kutotimiza ahadi zako kwake huwa ishara kuwa hujali kuhusu hisia zake. Kuwa neno lako haliwezi kuaminika na kumfanya mara nyingi kushuku unachomwambia.
Vitu vinavyoharibu uhusiano ambavyo wanaume hufanya ni kama kudanganya, kuvunja imani, kutomuelewa mpenzi wake, tukozungumza vya kutosha na mpenzi wake, kukosa kumfanya kuhisi salama na kutotimiza ahadi.
Soma Pia: Je, Nitaweza kubaini vipi kati ya Mapenzi Bandia na ya Kweli