Chumba cha kulala kinapaswa kuwa mahali pa kupumzika baada ya kuwa na siku ndefu na kupata usingizi wa kuupumzisha mwili. Kuwa na vitu visivyofaa kuwa kwenye chumba hiki hufanya iwe vigumu kupata usingizi wa kutosha ama kuzingatia ratiba ya kulala. Tazama orodha ya vitu visivyofaa kuwa chumbani cha kulala
Vitu visivyofaa kuwa chumbani cha kulala
- Runinga/Televisheni

Mwangaza wa buluu unaotoka kwenye runinga huharibu mfumo wa kulala. Kutazama runinga dakika chache kabla ya kulala hufanya iwe vigumu kupata usingizi. Pia, kuna jaribio la kuendelea kutazama runinga kwa muda zaidi. Kuweka runinga kwenye chumba cha kulala kuna athiri kwa njia hasi lengo la chumba kile.
2. Simu

Wataalum wa afya wanashauri kutotumia simu dakika chache kabla ya kulala. Kuwa na simu chumbani cha kulala huingilia mchakato wa kulala. Simu inapolia inaathiri usingizi wako unapoamka kuipokea ama kuizima. Mbali na hayo, kuna jaribio la kutumia simu kuangalia kinachoendela kwenye mitandao ya kijamii. Kutumia simu usiku kunakuweka katika hatari ya kuitumia kwa muda zaidi badala ya kupata usingizi.
3. Chakula

Haupaswi kula ukiwa chumbani cha kulala kisha kutazama runinga ama kutumia simu. Mabaki ya chakula huchafua kitanda na hakuna anayepata usingizi mzuri kwa chumba kichafu. Unapojipata ukikula chakula chumbani cha kulala, hakikisha kuwa unaondoa vyombo vichafu.
4. Vifaa vya mazoezi
Kuweka vifaa vya mazoezi hujaza nafasi kwenye chumba cha kulala. Vyumba vilivyo na nafasi ndogo huonekana kujaa, na kana kwamba hewa tosha haifiki. Pia, chumba kinaonekana hakina usafi. Epuka kufanya mazoezi kwenye chumba cha kulala.
5. Dawati ya kufanya kazi

Kutofautisha kati ya wakati wa kupumzika na wa kufanya kazi ni muhimu. Hata kama unafanyia kazi nyumbani, sio jambo la busara kufanyia kazi kwenye chumba cha kulala. Kwani mara nyingi huenda ukapata unafanya kazi zaidi badala ya kulala ama kulala zaidi baada ya kufanya kazi. Badala yake, weka dawati lako sebuleni.
Soma Pia: Mazungumzo 5 Muhimu Kabla ya Kufunga Ndoa Kati ya Wachumba