Kila mwanamke angependa kujua vitu vinavyowavutia wanaume kwao. Kwa njia hii, atafahamu vitu vya kufanya ama kutofanya ili kuwavutia wanaume.
Kwa kawaida, watu hudhania kuwa wanaume wanafurahishwa na wanawake wenye shepu za kiafrika, sura ya kupendeza na mavazi ya kuvutia. Ila, baada ya kufanya udadisi zaidi, wanaume wanapendezwa na vitu zaidi.
Mbali na vitu vya kawaida, baada ya kuwauliza wanaume maswali na kufanya utafiti zaidi, tumegundua kuwa kuna vitu zaidi vinavyowapendeza wanaume. Kuna vitu vya kiajabu vinavyowapendeza wanaume ambavyo mabinti huenda wakawa hata hawafahamu.
Tazama vitu vya kiajabu vinavyowapendeza wanaume

- Kumtegemea mwanamme
Wanaume hupenda kuhisi wanahitajika. Wanataka mwanamke anayewahitaji kwa njia moja ama nyingine. Mwanamke anayempigia mwanamme na kuomba msaada anapokumbana na matatizo madogo madogo humnasa mwanamme. Anahisi kuwa yeye ni mwanamme na jambo hili linawapendeza.
2. Mwanamke mkaidi
Hili ni jambo la kiajabu ambalo watu wengi hawatarajii. Ila ni ukweli, wanaume wanavutiwa na wanawake wakaidi. Wasio fanya kila kitu wanachoambiwa ama kinachotarajiwa kutoka kwao. Mwanamke mwenye msimamo wake na asiyebadilishwa mawazo kwa kasi.
3. Kuvalia miwani

Wanaume wengi huvutiwa na wanawake wanaovalia miwani. Miwani humfanya mwanamke apendeze zaidi. Hata kama wanawake wanaovalia miwani huenda wakawa na shaka kuwa watu hawapendelei wanaovalia miwani. Haufahamu jinsi unavyopendeza ukiwa na miwani!
4. Wanawake wasiovalia vipodozi
Napendelea mwanamke anapohisi ako salama kando yangu kiasi cha kutovalia vipodozi. Pia, mwanamke asipovalia vipodozi ni ishara kuwa anajiamini. Baadhi ya wanaume wanapendelea hivi. Hata hivyo, kumbuka kuwa wanawake huvalia vipodozi kujipendeza wenyewe na wala sio watu wengine. Kuna wanaume wanaopendezwa na wanawake wanaovalia vipodozi wakati wote pia.
5. Alama za kunyoosha
Wanawake wengi huwa na shaka kuhusu kuwa na alama za kunyoosha. Wengine hutafuta dawa za kuondoa alama hizi mwilini ili wawe na ujasiri zaidi kuhusu sehemu fulani za mwili. Usiwe na shaka tena! Kulingana na utafiti, wanaume wengi wanapenda wanawake wanaokuwa na alama hizi mwilini. Usione haya kuvalia kaptura na rinda fupi kwa hofu kuwa alama hizo zitaonekana.
Chanzo: Africaparent
Soma Pia: Mambo 5 Ya Kufanya Baada Ya Kufanya Mapenzi