Kupata kipindi cha hedhi ni jambo la kawaida na la kibiolojia linaloashiria kuwa na afya. Hutoa shaka kwa mwanamke iwapo alifanya mapenzi bila kinga, kwani ni ishara kuwa hana mimba. Licha ya kuwa na mazuri haya, kipindi hiki huandamana na mhemko wa hisia, kuhisi maumivu na kufura tumbo. Zote ambazo zinamfanya mwanamke kukosa starehe kwa siku tatu ama tano anaposhuhudia hedhi. Kufahamu vitu vya kuepuka katika hedhi kunamsaidia mwanamke kuwa na kipindi cha hedhi kilicho rahisi zaidi.
Orodha ya vitu vya kuepuka katika hedhi
1.Kunywa kaffeini nyingi

Kunywa kaffeini wakati wa hedhi hakushauriwi kamwe. Huchangia katika ongezeko la uchungu, kufanya chuchu ziwe laini na kuongeza kiasi cha damu kinachotoka.
2. Kula chumvi
Chakula kilicho na chumvi nyingi katika kipindi hiki huwa na athari hasi kwa maumivu ya hedhi. Kinachangia pia katika uchungu wa hedhi kuongezeka, kukosa starehe na kufura tumbo.
3. Kunyoa fudhi
Unapokuwa na kipindi cha hedhi, jitenge na kunyoa fudhi ama kuzipunguza kwa njia yoyote ile. Kufanya hivi katika kipindi hiki huwa na uchungu mwingi na kukosa starehe. Huenda ukapata majeraha ama maambukizi. Ngoja hadi baada ya kipindi chako cha hedhi kuisha.
4. Kuvalia pedi moja siku nzima

Ikiwa unatumia pedi, hakikisha kuibadilisha baada ya kila masaa 3 ama 5 kulingana na uzito wa hedhi. Kuvalia pedi siku nzima kunaongeza nafasi za kupata upele wa ngozi na harufu mbaya siku nzima. Dumisha usafi katika kipindi hiki.
5. Kufanya mapenzi bila kinga
Ni kawaida kupata ongezeko la hamu ya kufanya mapenzi katika hedhi. Kufanya mapenzi katika kipindi cha hedhi sio jambo mbaya, ila, kufanya mapenzi bila kinga hakushauriwi. Hasa ikiwa hauko tayari kuanzisha familia. Kujikinga katika ngono kunalinda dhidi ya kupata maambukizi ya kingono.
6. Kuvuta sigara
Kuvuta sigara kuna athari hasi kwa afya. Kuvuta sigara katika hedhi huongeza uchungu wa hedhi. Jitenge na uvutaji wa sigara katika kipindi hiki.
7. Kutokula chakula

Kutopata lishe tosha na bora katika kipindi cha hedhi kutachangia katika kukosa nishati. Kutokula chakula kutakupa matamanio ya kula vitamutamu. Vingi ambavyo vina wingi wa chumvi, kemikali na sukari na kukufanya uvimbe tumbo na kukosa starehe.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Hedhi Isiyo ya Kawaida: Utambuzi, Ishara na Jinsi ya Kulinda Dhidi ya Vipindi vya Hedhi Visivyo vya Kawaida