Kula Vyakula Hivi 10 Unapokuwa Mjamzito Kutasaidia Kupata Mtoto Mrembo

Kula Vyakula Hivi 10 Unapokuwa Mjamzito Kutasaidia Kupata Mtoto Mrembo

Kuchukua hatua muhimu kuhakikisha kuwa unajifungua mtoto mrembo kunawezekana.

Kwa sasa kwani una mimba, huenda ukahitaji kujua jinsi ya kutengeneza mtoto mrembo. Vitu unavyo fanya unapokuwa na mimba huenda vika adhiri jinsi mtoto wako anvyo kaa. Na hii sio imani za kuchekesha kama vile usile okro unapokuwa na mimba ama mtoto wako atakuwa na kamasi nyingi; ama usile vyakula vyenye pilipili ama mtoto wako atazaliwa na meno. Kwa hivyo tumeweka pamoja vidokezo vya vitu vya kula ili upate mtoto mrembo. Tazama hapa chini:

Hapa ni vitu vya kula ili upate mtoto mrembo

1. Bidhaa za maziwa

what to eat to have a beautiful baby

Unapokuwa na mimba, ni muhimu kula bidhaa za maziwa. Zitakupatia protini zaidi na kalisi unayo hitaji kuegemeza mtoto wako anayekua. Kunywa angalau glasi moja ya maziwa kila siku na unywe maziwa  ya bururu kuhakikisha mtoto wako ana afya.

2. Mayai

vitu vya kula ili upate mtoto mrembo

Mayai ni chakula kizuri. Ni chanzo chema cha vitamini, protini na madini. Protini iliyoko kwenye mayai inayafanya kuwa mazuri kwa mtoo anayekua na kusaidia kukuza na kutengeneza seli za kiinitete. Mayai yana wingi wa choline; ambayo unahitaji kwa ukuaji wa akili wa mtoto wako na mfumo wake wa neva.

Mandizi

what to eat to have a beautiful baby

Ndizi zina wingi wa folic acid, kalisi, potassium na Vitamini B6. Pia zina wingi wa anti oxidants zitakazo kusaidia kupata nishati nyingi. Kwa hivyo ni wazo nzuri kuiongeza kwenye lishe yako.

4. Viazi vitamu

vitu vya kula ili upate mtoto mrembo
Viazi vitamu ni chanzo chema cha beta-carotene, inayo badilishwa na kuwa Vitamini A mwilini. Na ni muhimu kwa ukuaji wa seli na tishu. Vitamini A pia husaidia kuimarisha kinga na kuboresha uwezo wako wa kuona. Kwa hivyo kula viazi vitamu kuna umuhimu kwa mama na mtoto aliye tumboni.

5. Legumes

vitu vya kula ili upate mtoto mrembo
Legumes ni kikundi cha vyakula kinacho husisha lentils, soybeans, kunde, na maharagwe. Ni chanzo kizuri cha fibre inayo tokana na mimea, protini, folate, kalisi na iron na zote ni muhimu sana kwa mama mjamzito. Kuwa na folate tosha kutahakikisha kuwa mtoto wako atazaliwa na afya na kuwa salama kutokana na maradhi na maambukizo siku za usoni.

6. Njugu

what to eat to have a beautiful baby
Njugu zina ladha na zina ufuta wenye afya, na ni hiari njema za kula mara kwa mara unapokuwa katika safari yako ya ujauzito. Zina omega-3 fatty acids zinazo saidia kukuza akili yake, protini, fibres na virutuisho vifaavyo ambavyo ni muhimu kwa ukuaji wa mtoto.

7. Sharubati ya machungwa

what to eat to have a healthy baby

Kutoka kwa chungwa, utapata folate, potassium na vitamini C. Mtoto wako atapata virutubisho vifaavyo ambazo zitasaidia kuepusha ulemavu anapo zaliwa. Vitamini C iliyoko kwenye sharubati ya machungwa itaongeza uwezo wa mtoto wako kutumia iron kwenye mwili. Kwa hivyo glasi ya sharubati ya machungwa kila siku kama kiamsha kinywa chako.

8. Mboga za matawi

vitu vya kula ili upate mtoto mrembo

Mboga zenye matawi zina virutubisho vingi na tunafahamu kuwa zinaweza saidia kuulinda mwili wako dhidi ya magonjwa. Kuwa chanzo bora za antioxidants, kalisi, protini, fibre, folate, potassium, na vitamini, mboga za kijani ni bora kwa lishe yako ya mimba.

9. Oatmeal

vitu vya kula ili upate mtoto mrembo

Oatmeal ina aina faida tofauti za kiafya. Kula wanga ni muhimu kwa sisi wote, hasa wanawake wajawazito kwani itakupatia nishati ya kufanya kazi za kila siku. Oatmeal ni chanzo kizuri cha wanga, selenium, vitamini B, phosphorous na kalisi. Kwa hivyo ile wakati wa kiamsha kinywa unapokuwa mjamzito.

10. Salmon

Salmon ina winga wa omega-3 fatty acids ambayo ni nzuri sana kwa afya ya moyo. Kuwa na omega-3 tosha kwenye lishe yako ni muhimu kwa wanawake wajawazito kwani inasaidia na ukuaji wa ubongo na macho ya kiinitete. Salmon ni njia muhimu ya kupata vitamini D, ambayo ni muhimu kwa afya ya mifupa na mfumo wa kinga.

Vidokezo muhimu vya vitu vya kukula ili upate mtoto mrembo

Orodha hii ya mambo ya kufanya unapokuwa mjamzito kupata mtoto mrembo ina vitu vilivyo jaribiwa na kuaminika kukupatia mtoto mrembo na mwenye afya.

Hapa ni vitu unavyopaswa kufanya:

  • Kula lishe iliyo na matunda na mboga nyingi
  • Kunywa maji mengi
  • Weka mazingara yako yakiwa masafi
  • Vitu vya kula ili kupata mtoto mrembo
  • Mazoezi machache
  • Enda ufanyiwe vipimo mara kwa mara
Ili kupata mtoto mrembo, epuka kufanya mambo yafuatayo unapokuwa na mimba

Kwa sasa kwani unajua unachopaswa kufanya unapokuwa na mimba kupata mtoto mrembo, hapa kuna vitu vichache ambavyo unapaswa kuepuka.

1. Kuvuta sigara

Uvutaji sigara ni hatari kwa afya yako na afya ya mtoto wako. Kuna kemikali 4000 katika kila sigara, yenye maana kuwa huenda ukaathiri mtoto aliye tumboni mwako kwa kumfunua kwa moshi wa sigara. Sigara ni hatari sana kwani zinaweza punguza kiwango cha oxygeni ambacho mtoto wako anapata. Mbali na hatari za mtoto wako kuzaliwa kama hajakomaa, kumfunua kwa moshi wa sigara kuna weza sababisha matatizo ya kula, ya moyo ama ya kupumua.

2. Vileo

Vileo ama pombe huenda vikaathiri jinsi mtoto wako anavyo kaa ama ukuaji wake. Iwapo ungetaka kujua cha kufanya unapokuwa mjamzito ili upate mtoto mrembo, kutupilia mbali vileo ni hatua muhimu. Vinywaji unapokuwa na mimba huenda vikaathiri mtoto wako sana na kumfanya azaliwe na Fetal Alcohol Syndrome (FAS). Watoto walio na FAS hukua na ulemavu wa uso na kitabia na pia wa maendeleo.

3. Dhiki

Kulingana na WebMD, dhiki sugu wakati wa ujauzito huenda yakabadili jinsi ubongo wa mtoto wako unakua. Huenda ukathibitisha matatizo ya kitabi ama matatizo ya kusoma mtoto anapo zaliwa. Dhiki hizi huenda zikatokana na kazi yako, uhusiano ama kutokana na maisha yako. Usikubali kitu chochote kikutatize unapokuwa na mimba. Pumzika kwa wingi. Itisha msaada unapohisi una mambo mengi zaidi.

4. Kukula zaidi

Matamanio ya chakula wakati wa ujauzito ni kawaida. Homoni zako nyingi mwilini zitakufanya uwe na hamu ya kula vitu ambavyo kwa kawaida huwezi gusa. Kula zaidi huenda kukasababisha uzito mwingi zaidi, kubaki na maji mengi mwilini, na kuumwa.

Kuwa na mtoto mrembo mwenye afya kuna wezekana. Unahitaji kujua cha kufanya unapokuwa na mimba ili kupata mtoto mrembo. Ukifuata vidokezo vilivyo kwenye makala haya, nafasi nyingi ni, mtoto wako atakuwa na kukushukuru!

kumbukumbu: WebMD

MedicineNet

Soma pia: Baby upper teeth first myth: Nigerian Culture

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Julie Adeboye na kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio