Vitu Muhimu Vya Kununua Kabla Ya Lockdown Kuanza

Vitu Muhimu Vya Kununua Kabla Ya Lockdown Kuanza

Taharuki iliyo zuka kufuatia kuongezeka kwa idadi ya watu walio na virusi vya corona nchini kuongeza ili wafanya watu kununua vitu vingi. Hali hii bado inazidi kuongezeka nchini kwa hofu kuwa huenda kukawa na lockdown nchini. Wiki ya kwanza baada ya kisa cha kwanza nchini kutangazwa, maduka mengi yalifurika watu kutoka sehemu mbali mbali wakivinunua vitu vya kujaza nyumba zao. Hali ambayo ilifanya maduka mengi kuwa na upungufu wa vitu kama vile mitakasio na tishu na vitu vingine vya kununua kabla ya lockdown kuanza.

Na huku kulazimisha maduka mengi kuweka kanuni dhidi ya kununua vipande vingi vya baadhi ya bidhaa hizi. Huku Kenya, maduka mengi yali wakataza watu kununua zaidi ya vipande vinne vya tishu. Watu pia hawakukubalishwa kununua mitakasio mingi. Ni muhimu tuangalie baadhi ya mambo muhimu ya kufuata tunapo nunua vitu vya nyumba katika wakati huu.

 

vitu vya kununua kabla ya lockdown

Vidokezo vya kuzingatia unapo tafuta vitu vya kununua kabla ya lockdown

 1. Usiwe na wasi wasi na kununua vitu zaidi ya idadi inayo kutosha mwezi mmoja.

Kosa ambalo watu wengi wanafanya katika wakati huu ni kufanya ununuzi wa vitu zaidi ya zile wanazo hitaji. Kufanya hivi kutasaidia kuhakikisha kuwa kila mtu anaye kuja kufanya ununuzi wake, hatakosa kitu chochote kwani kama ilivyo mtindo wa kila mwezi, kila mmoja atanunua vitu ambavyo vitamtosha. Pia ununuzi wa vitu zaidi ya unazo hitaji kunaleta hali ya uwoga nchini.

 1. Usitie shaka ukipata kuwa baadhi ya bidhaa zimekosekana kwenye maduka.

Ukipata kuwa baadhi ya bidhaa zimeisha dukani, haina maana kuwa bidhaa hizi zimepunguka. Ila ina maana kuwa maduka haya yana paswa kuongeza bidhaa ambazo zinahitajika na idadi kubwa ya watu. Pia janga hili linafanya kuwa vigumu kwa maduka haya kupata bidhaa zote wanazo hitaji. Baadhi ya maduka pia huenda wanapunguza bidhaa zao ili wauze bidhaa za kimsingi ambazo ni za lazima kwa kila mtu na jamii yake.

 1. Kuna bidhaa na vyakula tosha kwa kila mtu tukifanya ununuzi usio piku idadi ya kawaida.

Ili kuhakikisha kuwa kila mtu anapata bidhaa anazo hitaji, nunua vitu ambavyo vinakutosha bila kuongezea vya ziada. Kwa njia hii hautakuwa na vitu vingi usivyo hitaji kwa nyumba. Kila mtu akifanya hivi, hakutakuwa na shaka ya kukosa vyakula na bidhaa zinginezo za muhimu.

Vitu Muhimu Vya Kununua Kabla Ya Lockdown Kuanza

 1. Usi sukumane na watu kwa maduka

Unapo enda dukani kununua vyakula na bidhaa zinginezo, hakikisha kuwa unazingatia umbali wa mita moja unusu na watu wengine ili kupunguza nafasi zako kupata virusi hivi hatari vya homa ya corona. Unapo enda mahali ambako kuna watu wengi, haujui nani kati ya hao aliye na virusi hivi. Kwa hivyo kila mtu ana nasihiwa kuzingatia umbali unao hitajika ili kupunguza nafasi zako kupata virusi hivi.

 1. Waheshimu wanao kuhudumu madukani

Huku watu wengi wakiwa makwao na familia zao, wanao kuhudumu madukani wanajitolea mhanga kuhakikisha kuwa unapata vifaa unavyo endea dukani. Ni muhimu kwa kila mtu kugundua jambo hili na kuwa heshimu watu hawa. Wasaidie wakuhudumu vyema kwa kuwapa wakati rahisi. Usiwatatize ama kuibua mabishano nao. Unapokuwa umepumzika nyumbani, wana wahudumia watu wengi. Fuata maagizo yaliyo wekwa ili kila mtu awe na wakati rahisi.

Vyakula

 

Hiki ndicho kitu muhimu zaidi ambacho kila mwananchi anapaswa kuwa nacho kujihami iwapo kutakuwa na lockdown nchini. Kwani, bila chakula itakuwa vigumu kukaa kwa nyumba hasa kwa familia zilizo na watoto wadogo. Tuna angazia vyakula muhimu vya kununua ambavyo vitakaa kwa muda angalau mwezi mmoja.

 • Mchele
 • Spaghetti
 • Pasta
 • Unga ngano
 • Unga wa mahindi
 • Maharagwe
 • Kunde
 • Maziwa ya yaliyo hifadhiwa (urefu wa maisha wa zaidi ya miezi 5)

Vitu vya jikoni

 • Chumvi
 •   Sukari
 • Viungo
 • Mafuta ya kupika
 • Maji ya kunywa naya kupika

Pia iwapo una sehemu ya shamba ambayo unaweza lima mboga, hakikisha umenunua mbegu pia.

Epuka kununua vyakula vingi ambavyo vinahitaji kuhifadhiwa kwenye friji.

 

vitu vya kununua kabla ya lockdown

Dawa

 • Hakikisha una dawa za kutumia kwa magonjwa mepesi kama kuumwa na tumbo ama kichwa. Kwa wanadada, za kutuliza tumbo wakati wa hedhi.
 • Vitu vya usafi wa kijumla na wa kipekee
 • Taulo za hedhi
 • Jik
 • Spirit
 • Sabuni
 • Maji ya kufua

Mazungumzo

 • Kulipia Wifi

Mwangaza

 • Nunua mtungi mmoja zaidi wa gesi
 • Makaa
 • Viberiti
 • Mishumaa

Fedha

 • Hakikisha una pesa za kutosha kwenye simu yako
 • Idadi tosha ya pesa za kutumia kwa jambo la dharura
 • Mipango ya kuhama
 • Kuwa na mahali ambapo unaweza hamia iwapo kuwe na mabadiliko

Bidhaa Zinginezo

 • Nambari za hospitali na watu wa usalama
 • Vitabu
 • Michezo ya mbao ya kucheza kama familia
 • Vinywaji

Written by

Risper Nyakio