Vitu Muhimu Vya Kununua Unapo Tarajia Kujifungua Mtoto

Vitu Muhimu Vya Kununua Unapo Tarajia Kujifungua Mtoto

Furaha ya kuwa mama huenda ikakufanya usahau vitu muhimu utakavyo hitaji vya mwanao. Haya ni kweli hasa kwa mama wa mara ya kwanza. Walakini, ili kuhakikisha kuwa una kila kitu tayari wakati ambapo mtoto wako anazaliwa, hapa kuna orodha ya vitu vya kununua unapo tarajia kujifungua mtoto.

vitu vya kununua unapo tarajia kujifungua mtoto

1. Nguo za mtoto - vitu vya kununua unapo tarajia mtoto

Kufanya ununuzi wa nguo ni rahisi unapojua jinsia ya mtoto. Hata hivyo, bado unaweza nunua nguo ambazo zinaweza valiwa na jinsia zote mbili iwapo bado huja jua iwapo unatarajia mtoto wa kiume ama wa kike.

Aina ya nguo za mtoto za kununua ni kama vile:

• Onesies
• Fulana
• singlets
• bodysuits
• Soksi
• Vinyasa
• Shati

2. Vitu muhimu vya kuoga

Mtoto atakuwa na bidhaa za kuoga tofauti na wana familia wengine. Kuna vitu vya kununua unapo tarajia kujifungua mtoto zitakazo ifanya kazi yako ya kumsafisha mtoto rahisi. Vitu vingi vya kumsafisha mtoto huja zikiwa pamoja ama pia unaweza fanya uamuzi wa kununua kitu kimoja baada ya kingine kama vile:

• Hodhi
• Chombo cha kujisaidia ama Potty
• Kikapu cha ngu chafu
• Ndoo
• Bakuli ya sabuni
• Bakuli
• Kiti cha mama cha plastiki
• Pamba za masikio
• Kikombe

3. Bidhaa za usafi wa mtoto na utunzaji wa ngozi

Ngozi ya mtoto ni laini sana ya kutumia bidhaa za watu wazima, kwa hivyo itakubidi kufanya ununuzi wa bidhaa za mtoto kutoka kwa wanunuzi wanao aminika. Hutaki kumwumiza mtoto wako kwa kutumia bidhaa zisizo za sawa ama vitu ambavyo sio salama kwa watoto. Vidokezo vya ununuzi wa bidhaa zinazo faa za utunzaji wa mtoto ni:

• Nunua talc-poda ya mtoto—talc huenda ikawa hatari kwa watoto
• Bidhaa za asili ni bora kwa watoto
• Tafuta bidhaa ambazo hazina paraben ama phthalate, kwani kemikali hizi huenda zika athiri vikali mtoto wako
Kwa usafi na utunzaji wa ngozi, vitu vya kununua unapo tarajia mtoto ni kama vile:
• Mafuta ya kujipanga ya mtoto ama lotion
• Ufuta wa mtoto
• Poda ya mtoto
• Petroleum jelly
• Sabuni ya mtoto ama gel ya kuoga
• Vitambaa vya kujipanguzia vya mtoto
• Diapers
• Diaper rash ointment
• Soft bathing foam ama sponge
• Taulo laini za kuoga
• Shampoo ya mtoto

vitu vya kununua unapo tarajia kujifungua mtoto

4. Bidhaa za kumlisha mtoto - vitu vya kununua unapo tarajia kujifungua mtoto

Vifaa hivi vya kumlisha mtoto wako vita kurahisishia wakati wako wa kumlisha mtoto:

• Kikombe laini cha spout
• Big hot water Flasks
• Bib
• Chupa za kumlisha
• Pampu za matiti (za mama)
• Chombo cha kupasha chakula joto
• Mto wa kumnyonyesha mtoto
• Squeeze feeder na kijiko
• Sterilizer ya vyombo
• Pacifier
• Kitu cha kupasha chupa moto cha sitima

5. Matandiko ya kitanda

A newborn will rob you of your precious night’s sleep. Moms all over the world know that when the baby hasn’t yet grown to the stage of sleeping through the night, the momma will suffer the most. Helping your baby sleep longer will require getting these things to buy when expecting a baby.

Mtoto mdogo atakuibia usingizi wako mwanana. Wamama duniani kote wanafahamu kuwa wakati ambapo mtoto bado hajafika hatua ya kulala usiku, mamake atateseka sana. Kusaidia mtoto wako alale wakati mrefu kitahitaji kununua vitu hivi ambavyo

• Cot
• Net ya mbu ya mtoto
• Godoro la mtoto
• Shuka za kitanda
• Blanketi laini za kufunika godoro
• Blanketi nyepesi za kumfunikia mtoto
• Monitor ya mtoto

6. Vifaa vya kumbeba mtoto anapo toka ama kusafiri

Kuna vitu vya kununua unapotarajia kujifungua mtoto ambazo zitakusaidia unapo mpeleka mtoto hospitalini ama kuwatembelea marafiki na jamaa. Baadhi ya vitu hivi ni:

• Kiti cha gari cha mtoto
• Mkoba wa kusafiri wa mtoto (mkubwa kiasi cha kutoshea nguo, diapers, na chupa za kumlisha)
• Taulo ndogo
• Pram
• Mavuli
• Vifaa vya kujipanguzia

Ni rahisi sana kuzidiwa na mambo unapo fanya ununuzi wa vitu vya mtoto, yenye maana kuwa huenda ukajipata ukinunua vitu ambavyo hauhitaji na kusahau vile ambavyo unahitaji. Ni matumaini yetu kuwa orodha yetu itakuongoza kwa kuanza unapo fanya ununuzi.

Vyanzo: US National Library of Medicine 

WebMD

Soma pia: Would you speak to your baby as though you are speaking to a puppy?

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Julie Adeboye kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio