Vitu Unavyo Paswa Kununua Unapo Tarajia Mtoto

Vitu Unavyo Paswa Kununua Unapo Tarajia Mtoto

Hakikisha kuwa chumba cha mtoto wako kinavutia, ila kisiwe na rangi kali sana kama manjano. Kinapaswa kuwa na rangi iliyo tulia.

Mara tu unapo gundua kuwa una mimba, una fahamu kuwa watoto wanahitaji vitu vingi. Ikiwa una hisi kuzidiwa, usiwe na shaka. Tume kuandalia orodha ya vitu vya kumnunulia mtoto wako. Kuna bidhaa nyingi zinazo patikana lakini kuwa na orodha muhimu ya vitu vya kununua unapo tarajia mtoto itakusaidia sana.

Orodha ya vitu vya kununua unapo tarajia mtoto

vitu vya kununua unapo tarajia mtoto

 

 • Mavazi ya mtoto

Bila shaka mavazi ya mtoto yana pendeza na huenda ukajipata ukinunua mavazi mengi na kuzidisha bajeti uliyo kuwa nayo. Jidhibiti kwa sababu kuna vitu vingi utakavyo hitajika kununua. Tazama vitu utakavyo hitaji kuwa navyo na kuweke kwenye begi lako la uzazi unapo elekea hospitalini kujifungua.

Mavazi ya mtoto kama pajamas, rompers, suruali, nguo za kulala na blausi nusu, soksi, na fulana. Hakikisha kuwa nguo za mtoto zinafuliwa kwa kutumia sabuni isiyo nukia.

 • Chumba cha mtoto

Hakikisha kuwa chumba cha mtoto wako kinavutia, ila kisiwe na rangi kali sana kama manjano. Kinapaswa kuwa na rangi iliyo tulia kwani mtoto bado hajazoea kuwa nje mwa tumbo. Hakikisha kuwa chumba chake kina vitu hivi:

 • Kijitanda chake
 • Kifaa cha kuangalia kinacho tendeka chumbani
 • Godoro la kijitanda chake
 • Meza ya kubadilisha diaper
 • Can ya kutupia takataka
 • Meza ya kumbadilishia nepi
 • Mahali pa kuhifadhi mavazi ya mtoto

Kumsafisha mtoto na utunzaji wa mtoto

 

vitu vya kununua unapo tarajia mtoto

Una stahili kuwa na vitu hivi vya kumsafisha mtoto wako.

 • Mafuta ya kumpaka isiyo na harufu
 • Kifaa cha kumkata kucha
 • Beseni la kumkogeshea mtoto
 • Sabuni spesheli ya mtoto
 • Taulo safi za mtoto

Kumlisha mtoto wako

Watoto hukua kwa kasi, na una stahili kumlisha vyema ili akue kwa kasi. Huenda baadhi ya vifaa hivi ukanunua baada ya kuzaliwa kwake.

 • Pedi za chuchu
 • Pampu ya kukamua maziwa
 • Mto wa kutumia unapo mnyonyesha
 • Sindiria za kunyonyesha
 • Pacifier ya mtoto

Diaper ama nepi

Baada ya mtoto kukula, atapitisha chakula hicho na utahitajika kumbadilisha. Utahitaji:

 • Wipes za mtoto
 • Diapers

Mbali na hizo, utahitaji vifaa vya kumbebeleza mtoto alale kama vidoli. Hakikisha kuwa ni vitu vikubwa ambavyo haviwezi toshea kwenye mdomo wake. Vidoli pia vinasaidia na ukuaji wa akili yake.

Inapofika wakati wa kutoka kwenye nyumba, utahitaji vitu vya kumbebea mnapo toka shumbani. Kama vile kiti cha gari cha mtoto, carrier ya mtoto, mkoba wa diaper na stroller.

Ikiwa bado kuna baadhi ya vitu ambavyo hujanunua unapo tarajia kuwa na mtoto, huu ndiyo wakati bora wa kufanya hivyo. Je, wakati wa kwenda hospitalini una karibia na kuna baadhi ya vitu ambavyo hujanunua bado? Usitie shaka, utapata wakati wa kununua ama umtume mchumba wako kukununulia vitu hivi.

Soma Pia: Kupata Mtoto Katika Umri Wa Miaka 50: Mambo Muhimu Ya Kufahamu

Written by

Risper Nyakio