Habari Za Sasa Hivi Kuhusu Covid-19: Vitu Muhimu Vya Kununua Kabla Ya Lockdown

Habari Za Sasa Hivi Kuhusu Covid-19: Vitu Muhimu Vya Kununua Kabla Ya Lockdown

Ni vyema kwa kila familia kujihami na chakula tosha huku siku za karantini ziki ongezewa.

Huku Afrika, nambari za watu walio na ugonjwa wa korona vime endelea kuongezeka. Na watu wengi kupoteza maisha yao na watu kupata hofu. Shule nyingi zimefungwa na wanafunzi kushauriwa wabaki nyumbani hadi pale ambapo visa vya corona vitapunguka nchini. Wazazi pia wameshauriwa kubaki nyumbani na kufanyia kazi kutoka nyumbani. Huku kuna maana kuwa kila familia inapaswa kujihami na vyakula tosha wakati huu. Tuna angazia vitu vya kununua wakati wa karantini na jinsi ya kuzihifadhi ili zidumu kwa muda mrefu.

Huku Italy ikiweka lockdown nchini kote ili kupunguza kusambaa kwa virusi vya corona, nchi zingine zimefuata jambo hili. Na kulingana na mambo yalivyo, huenda kipindi hiki cha karantini kisiiche wakati wowote hivi karibuni. Ni vyema kujihami na vidokezo hivi vya kununua na kuhifadhi chakula chako.

Jinsi ya kupanga vitu vya kununua wakati wa karantini

grocery shopping

Chanzo: Shutterstock

Tengeneza orodha

Una nini sasa hivi, na una kiwango kipi? Ikiwa na kitu muhimu cha jiko yako, unahitaji kuwa na uhakika una vya kutosha ili kutosheleza familia yako yote kwa muda wa wiki mbili ama mwezi. Kabla ya kwenda kufanya ununuzi wa vitu vya jikoni, tengeneza orodha. Ukifahamu muda ambapo viungo vya friji yako vitadumu, utajua vitu ambavyo utahitaji na kiwango cha kila kiungo. Kisha uanze kufanya ununuzi.

Utahitaji viungo vya kawaida: mchele, maharagwe, mihogo, ndizi, nafaka na oats. Ni viungo muhimu vya kutengeneza lishe yako wakati mwingi na haviharibiki kwa urahisi. Unapo nunua ndizi, ni vyema zaidi kununua ndizi mbichi. Zina ladha na afya zaidi na zitadumu kwa muda zaidi, ikilinganishwa na ndizi mbivu.

Tengeneza ratiba ya chakula ya wiki mbili
Jambo la busara la kufanya ni kuhakikisha kuwa lishe zako zote kwenye ratiba yako zina viungo sawa. Kwa njia hiyo, chungu kikubwa cha supu kwa mfano unaweza kula kwa mkate ama mihogo kama kiamsha kinywa chako; wakati wa chamcha na chajio, supu hiyo unaweza ila na wali, sembe ama chapati. Supu ni muhimu sana katika kipindi hiki. Ikiwa una bakula za supu na rojo kwenye friji yako, unahitajika kuchemsha kitu utakacho kila pamoja na supu hiyo. Tengeneza ratiba itakayo kufaa pamoja na familia yako.
Jambo muhimu la kufahamu unapo tengeneza chakula ni kutengeneza kingi kiwango ambacho unaweza kula angalau mara tatu kisha uhifadhi kwenye friji. Kwa njia hii, umepunguza wakati wa kupika chakula wakati utakapo hisi njaa. Ukifanya hivi mara kwa mara, utagundua kuwa wakati wote kuna kitu cha kupasha moto kutoka kwa friji na ambacho familia yako itafurahia.

Vitu vya kununua kabla ya lockdown, friji yako itakufaa zaidi, na jua pia.

grocery shopping for a quarantine

Unafahamu jinsi vidokezo vya hapo juu vilihusika na friji? Itakusaidia sana katika kuhifadhi vyakula vyako. Kwa mfano matunda na mboga ambazo zinaharibika kwa urahisi vitaishi zaidi kwenye friji. Unaweza pika mboga hizi mara nyingi kwa mwezi. Pia unaweza hifadhi maziwa yako. Ila iwapo unajitayarisha kwa lockdown, maziwa ya poda ni bora zaidi.

Tusijidanganye, sio kila mmoja wetu aliye na friji. Baadhi ya wakati huenda sitima zikapotea kwa muda mrefu hadi unasahau kuwa una friji. Ila, walisema kuwa mazingira asili yana fadhili. Kwa sababu jua iko hapo kukusaidia kuhifadhi nyama, samaki na mboga zenye majani. Samaki na nyama iliyo kaushwa vyema itakaa kwa muda mrefu. Ni wakati uanze kutumia baraka hizi kabla msimu wa mvua uanze.

Kukausha kwa moshi ni mojawapo ya njia bora zaidi za kuhifadhi nyama na samaki. Hata kama huchukua wakati, kufanya hivi kutasaidia nyama na samaki yako kudumu kwa muda mrefu.

Vidokezo muhimu wakati wa karantini

bookie

  • Tafuta vitabu unavyo vipenda zaidi na sinema
  • Iwapo bado unafanya kazi, tafadhali fanyia kazi nyumbani
  • Usijumuike na watu walio katika vikundi kama vile sokoni
  • Hifadhi mitungi mingi ya maji na unywe maji kwa wingi kila siku
  • Nunua vyakula vya kontena
  • Nunua tishu, sabuni na vitakasio vya mikono vya kutosha
  • Iwapo unachukua matibabu, hakikisha umechukua za mwezi mmoja na kuziweka nyumbani.
  • Anza kufanya mazoezi nyumbani
  • Isafishe nyumba yako

HuffPost  WashingtonPost

Soma pia: The World Health Organisation Calls On Countries To Prepare For A Coronavirus Pandemic

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio