Wanaume Hawa Kutoka Kenya Waelezea Ufarisi Wao Na Mipango Ya Kando Na Umuhimu Wake

Wanaume Hawa Kutoka Kenya Waelezea Ufarisi Wao Na Mipango Ya Kando Na Umuhimu Wake

These Kenyan men share with us why they have a side chick outside their marital homes, and why they don't plan on stopping any time soon.

Wanaume hawa kutoka Kenya walio kwenye ndoa wameelezea sababu zao kuwa na mpango wa kando nje ya ndoa. Pia, waliweza kuzungumzia kwa nini hawana nia za kutengana nao hivi karibuni.  Sababu zao ni kama vile:

  • Kuridhika wakati wa kufanya mapenzi
  • Uwoga wa ndoa zao kuvunjika.
  • Kudumisha kasumba kuwa wanaume wote hudanganya.

Kwa kweli, wanaume wengi huelewa kuwa, kuwa na mpango wa kando nje ya ndoa, huja na majukumu zaidi. Na wakati mwingine gharama zao huwa ni zaidi ya zile za kudumisha bibi.  Hata hivyo, wanaume kama walivyo hungependa kila wakati kuwa na mwanamke mwingine nje ya ndoa.

Vitubio vya wanaume walio oa kuhusu kuwa na mwanamke mwingine nje ya ndoa

mpango wa kando

Chukua James Ochieng kwa mfano, mkaaji wa mtaa wa Mowlem jijini Nairobi. Licha ya kuwa amemuoa Gladys, James alielezea Standard kwa nini amemweka mke mwingine kando ya bibi yake kwa miaka kumi.

La kupendeza zaidi ni kuwa, Ochieng hufanya kazi ya kuosha magari karibu na hospitali ya Mama Lucy Kibaki. Alidai kuwa mke wa nje aliyeishi mtaa wa Umoja 2 anafahamika vyema na mke wake. “Mke wangu anamfahamu mpango wangu wa kando na haina shida yoyote na hilo,” akasema.

Ochieng alisema kuwa, hapo mwanzoni bibi yake alikuwa mkali alipogundua juu ya tabia zake. “hakutaka kuskia jambo lolote lile kuhusu mpango wa kando. Na angechukua simu na kumtusi kwa majina yasiyo andikika.  Isitoshe, ilifika mahali tukaachana sababu ya hilo jambo la mpango wa kando”.

Ochieng alimkaribisha tena kwani ndiye mama wa mtoto wake kijana wa miaka sita. Alijua baadaye kuwa alishauriwa hivyo nyumbani kuwa haya ndio maumbile ya wanaume.  Na kuwa huwezi shinda kwa hili jambo akiongeza kuwa alirudi kama amebadilika bila maswali yeyote ile.

Alisema kuwa bibi yake ndiye humwambia kila wakati atumie kondomu asije akawaletea maambukizi ya zinaa. Alipoweza kuulizwa jinsi anayakihimu mahitaji yao ya kifedha hukuwa mwenye uwazi.

Kudumisha Kasumba ya mpango wa kando

mpango wa kando

Bwana Justus Mwanzia anayeishi mtaa wa Dandora alikuwa na maoni sawia. Alieleza sababu yake kumwona mwanamke mwingine ilihali yeye ni mwanamme mwenye familia.

Kulingana naye bibi yake huwa na mazoea ya kumtuhumu ata anapojaribu kuwa mwaminifu. “ Nakwambia ni bure kuishi ukiwa mwaminifu wakati bibi yako anajua wanaume wote ni mbwa.”  Aliongeza kwa kusema, “Iwapo u msafi au mchafu ni sawa kwa mwanamke.”

Bwana Mwanzia  hupata mapato yake kutokana na kushona na kupiga nguo pasi. Alitueleza sababu zake kwa kutuuliza hili swali: “kwa nini niwe tofauti wakati wanaume wote huwa na mke zaidi ya mmoja?”

Hata hivyo, Mwanzia alieleza kuwa ni mwenye makini bibi yake asije jua juu ya tabia zake. Asije kumwonyesha kichaa na kuanza ghasia.

Mwanzia anadai kuwa hajawahi kumpa huyo mwanamke mwingine ata senti. Kile ambacho yeye hutaka ni kuridhishwa kimapenzi.  “Huyo mwanamke ana mume kwa hivyo sijukumiki vyovyote vile kifedha. Kwa kweli, kama anaweza kuniitisha pesa inaweza bidi uhusiano wetu uishe kwani sina pesa kwa wakati huu.”

 

Mwanamume mwingine aliye na mpango wa kando

mpango wa kando

Kwa bwana Ainea Wafula, amabaye kwa wakati huu anaishi mtaa wa Kariobangi, sababa yake kuwa na mke mwingine nje ya ndoa ni njia ya kuthubutu. “Iwapo mkosane na bibi yako na aamue kwenda? Wanawake hawawezi kutabirika na hivyo basi lazima niwe na mpango B.

Bwana Wafula, hustler, anasema kuwa mapato yake huwa ya chini sana. Lakini lazima ampe mpango wa kando kitu anapopata kutoka kwa vibarua anavyofanya. “Bibi yangu hana shida kwani ni mwalimu hivyo anaweza kuyakimu mahitaji ya nyumbani,” akafichua.

Hata hivyo, Wafula alisema kuwa bibi yake hajui chochote juu ya mapango wake wa kando. Pia huwa haendi huko wakati hana pesa.

Wafula pia alidai kuwa anapopata pesa, hupenda kumtembelea mpango wake wa kando anayeishi mtaa ulioko karibu wa Dandora kupumzika na kujiburudusha. “Mke wangu hawezi ata kunikanda wakati ninahitaji lakini nikimfariji mpango wangu wa kando anatanifanyia hivyo.”

 

The Daily Standard Kenya

Also read: Meet The Women Behind Senegal's Mistress Of A Married Man

Written by

Risper Nyakio