Vyakula 6 Bora Vya Kumpa Mtoto Aliye Na Joto Jingi

Vyakula 6 Bora Vya Kumpa Mtoto Aliye Na Joto Jingi

These foods are packed with nutrients that will help your child recover faster.

Hakuna jambo la kusikitisha kwa wazazi kama kuona watoto wao wachanga wakiugua na kupata joto. Huu ni wakati wa kuhuzunisha kwa mzazi kwani mtoto anakosa nguvu, ngozi inakuwa moto zaidi, na macho yenye jotojoto. Na kuongezea kwa mambo haya ni pale ambapo mtoto anapokosa kula na kumfanya mzazi ashangae vyakula atakavyo mlisha mtoto anapokuwa na joto. Je, nini unachomlisha mtoto aliye na joto jingi? Tutachunguza vyakula vya joto jingi unavyo paswa kumlisha mwanao.

Vyakula 6 Bora Vya Kumpa Mtoto Aliye Na Joto Jingi

Ni kawaida kwa mzazi kushangaa vyakula vya kumlisha mtoto aliye na joto jingi

Joto jingi (fever) ni nini?

Wazazi wanapaswa kufahamu na kuweka akilini kuwa na joto sio ugonjwa. Mbali ni dalili ya ugonjwa na ni dalili kuwa kinga ya mwili ya mtoto iko shwari kabisa.

Wastani wa kipimo cha joto  kwa mwili huwa  digrii 37C(98.6 F). Joto ni kitu chochote juu ya hii.

Maambukizi kwa mara nyingi husababishwa na bakteria ama virusi. Kwa wakati mwingi, huongezeka mwilini wako unapokuwa katika vipimo vya joto vya kawaida. Wakati mtoto wako anapata joto, ina maana kuwa mwili wake unajaribu kuua viini vinavyo sababisha magonjwa. Kinga ya mwili ya mwanao pia inaweza kuamilishwa katika hali hii.

Baada ya kufahamu kuwa joto sio ugonjwa, mtoto aliye na joto  atakosa starehe haswa kama kuna dalili zinginezo  kama vile kuumwa na koo  na mafua. Pia ni muhimu kuhakikisha kuwa joto haifikii viwango vya juu zaidi, kwani jambo hili linaweza sababisha febrile fits katika watoto wengine.

Isitoshe, kuna uwezekano mkubwa kuwa hamu yake ya chakula ita athirika pia. Japo hili ni jambo la kawaida, wazazi wengi huwa na wasi wasi kuhusu vyakula vya kumlisha mtoto aliye na joto.

Ilihali unaweka akilini kuwa ni sawa kwa mtoto wako aliye na joto kula vyakula vyake vya kawaida, iwapo mtoto wako mchanga anasumbua, vyakula vya joto jingi vitakavyo msaidia mwanao kupona mbio.

Vyakula 6 Bora Vya Kumpa Mtoto Aliye Na Joto Jingi

  1. Maziwa ya mama

Iwapo mtoto wako bado ananyonya, mkubalishe anyonye kwa mara zaidi anapokuwa mgonjwa. Matiti yako huweza kujua mtoto wako anapokuwa akipigana na maradhi (kupitia kwa mate ya mtoto). Maziwa yako yatageuka na kuwa na kingamwili za kupigana na maradhi na kuishusha joto. Pia kunyonyesha huleta starehe kwa mtoto wako mchanga na kumsaidia kupumzika anapokuwa magonjwa.

  1. Supu ya kuku

Iwapo mtoto wako ameanza kula vyakula vigumu, huenda mboga na supu ya kuku ni chakula bora kumlisha mtoto mwenye joto.  Huwa na mizani sawa ya vitamini, madini na protini ambazo zinahitajika na mwili wa mtoto kwa vipimo vikubwa anapougua.

Mdogo wako pia atapata maji na elektroliti anazohitaji kutoka kwa supu ya kuku zitakazo msaidia kupigana na maambukizi hivyo kupunguza joto. Ikiwa mdogo wako ana joto kutokana na mafua, basi ule mvuke wa supu utaondoa kufungana.

Kwa wakati huo, kuku huwa na amino asidi inayoitwa Cysteine. Hii huwa na viini vya anti-viral na viini ambazo husaidia kudhibiti joto.

Vyakula 6 Bora Vya Kumpa Mtoto Aliye Na Joto Jingi

  1. Matunda yaliyogandishwa ama maziwa yaliyo ganda

Kama unawaza juu ya nini cha kumpa mtoto wakati ana joto jingi jaribu hivi vyakula vilivyogandishwa. Bana matunda mbichi, mwaga kwenye umba za popsicle kisha ugandishe. Vyakula hivi viwili huwa na viini na madini mengine ambayo yatamsaidia mtoto wako kupigana na joto jingi vizuri. Pia, hio baridi itapoza mwili wa mdogo wako. Pia ni tamu!

  1. Maji ya nazi

Katika tamaduni za  Asia, maji ya nazi kwa kiasili imedhaniwa kuwa na viini vya kupoza. Na iwapo mtoto wako ana joto utafanya kila jitihada kupunguza joto mwilini mwake. Pia, maji ya nazi ni chanzo mwafaka cha elektroliti iwapo joto ya mtoto wako imetokana na tummy bug. Pia utamu wake unafaa kuwa mzuri kwa wanaosumbua kula (ambao watasumbua ata zaidi wanapougua).

  1. Asali

Asali safi ya kiasili huwa imejaa kampaundi za kuua viini.  Kuna ushahidi wa kisayansi kuwa asali inaweza kuchechemua mfumo wa kinga. Utafiti pia unaonyesha kuwa asali inaweza kuwa na ufanisi mkubwa katika kutuliza kikohozi kuliko dawa za kukohoa. Ina ifanya chaguo mwafaka kumpa mtoto wako iwapo joto yake imesababishwa na maambukizi kwenye koo.

Onyo la kiusalama: Usiwahi mpa mtoto wa chini ya mwaka mmoja asali juu ya hatari ya ubotuli.

Honey

6. Shayiri

Kuna jambo tu la kutuliza  juu ya bakuli la shayiri lilo na mvuke. Haya kando, shayiri ni chanzo kizuri cha vitamini E, inayoboresha mfumo wa kinga. Isitoshe, huwa na viini vya polyphenol na nyuzi za beta-glucan ambazo husaidia mfumo wa kinga.

Jiepushe na shayiri iliyotengenezwa  viwandani ilihali tumia shayiri kamili kwa matokeo mazuri.

Kile ambacho hufai kumlisha mtoto aliye na joto

Wazazi, ni vyema kujiepusha na aina hizi za vyakula wakati mtoto wako ni mgonjwa.

  • Vinywaji vilivyo na kafeini.

Ilihali mtoto wako anaweza kuwa hanywi chai au kahawa, vinywaji vingine kama soda huwa na kafeini.  Vinaweza kukausha maji mwilini iwapo atakunywa na huwa na sukari nyingi sana.

  • Chakula kigumu au kilichongoka

Ikiwa joto la mtoto wako limesababishwa na maambukizi ya koo, ni vyema kujiepusha na vitu kama biskiti, chengachenga  na vyakula venye kukwaruza. Hivi vinaweza kughadhabisha koo.

  • Vyakula vilivyotengenezewa viwandani.

Huwa na virutubishi vya kiwango cha chini, na wingi wa mafuta na sukari. Hivi vyakula havitafanya kitu kusaidia kupigana na maambukizi yanayoleta joto. Jiepushe navyo kabisa.

Tafadhali kumbuka kuwa mtoto anafaa kulishwa chakula kigumu baada ya umri wa miezi sita (vyakula vya joto jingi vilivyo hapa juu ila tu asali ambayo hutumika baada ya mwaka mmoja).

Iwapo mtoto wako ataugua huku ana joto, zidi kumnyonyesha ama kumpa maziwa yaliyogandishwa.

 Kwa kawaida, unapaswa kushauriana na daktari wako wa mtoto akupe mawaidha.

Also read: Govt Explains Ebonyi Yellow Fever Status, Clarifies Number Of Deaths

References: Medline Plus, MedicineNet

This article was published with the permission of theAsianparent Singapore

 

Written by

Risper Nyakio